Pata hadithi mbalimbali za zamani hapa

Pata hadithi mbalimbali za zamani hapa

Nahitaji kitabu Cha usiku wa balaa kimeandikea na S.S Bawji unaweza kuw nacho?
 
Bujibuji Simba Nyamaume naomba kama una kitabu cha ndoto za alinacha
Mkuu kwa ninavyofahamu ndoto za Alinacha ni hadithi fupi kwenye kitabu kimojawapo kati ya matoleo ya vitabu vya "Alfulela u lela".

Hadithi hiyo fupi ni kama ifuatavyo ( kwa ninavyokumbuka) nikipata wasaa nitaitafuta ni- scan na kutuma hapa maana ina page mbili au tatu tu.

Alinacha alizaliwa kwenye familia ya kimasikini, wakati wa kufa baba yake hakukua na urithi wa maana kwa ajili ya Alinacha, bali shilingi hamsini tu ambazo ni akiba zote za baba yake Alinacha.

Baada ya kumzika baba yake Alinacha alichukua hizo fedha na kununua vikombe vya udongo kwa ajili ya kuviuza ili apate faida na kufanya biashara zingine kama kukodi chombo na kuchuuza bidhaa kwenda bara.

Akiwa barabarani kusubiri wateja Alinacha alipitiwa na usingizi. Akiwa usingizini akaanza kuota: Nitauza vikombe, kisha nitapata faida, nitaongeza bidhaa na kufungua duka kubwa! Nitakodi chombo na kuuza bidhaa bara! Nitakua mfanyabiashara mkubwa kiasi cha kusujudiwa na kila mtu ikiwemo mfalme.

Kisha nitaoa binti mfalme na kuanza kumnyanyasa!!! Mfalme atakuja kunipigia magoti, tafadhali Alinacha usimnyanyase binti mfalme! Nitampiga mfalme teke! Akiwa ndotoni alinacha akarusha teke lililovunja Vikombe vyake vyote! Alinacha akabaki kuwa masikini maisha yake yote.

Huu ndo msingi wa msemo maarufu Tanzania wa NDOTO ZA ALINACHA.

Hata hivyo sifahamu kama kuna kitabu kinaitwa NDOTO za Alinacha. Hiyo nimeisoma kwenye Alfu lela u lela miaka mingi imepita. Muktadha ni huo japo nikirejelea hadithi kuna namna wanaandika inanoga zaidi.
 
Nashukuru, sikuwahi kujua kama ni kastory kadogo ndani ya masimulizi hayo
 
Hii ni thread maalum ya kukuunganisha na mastory mbalimbali ya zamani, nyingi zikiwa ni zile tulisimuliwa na Deborah Mwenda akisaidiwa na Eddah Sanga kwenye kipindi cha Mama na mwana, Radio Tanzania Dar es Salaam.

Zifuatazo ni hadithi ntakazozileta wiki hii, wiki ya uhasishaji wa usomaji wa vitabu duniani.

Najua kupitia hadithi hizi tutaunganishwa wapenzi wa majukwaa mbalimbali ya JamiiForums.

1. SAFARI SABA ZA SINBAD

Safari 7 za Sinbad

2. ALADIN NA TAA YA AJABU

3. ALIBABA NA WEZI 40

4. MASIMULIZI KAMILIFU YA ALFU LELA U LELA AU SIKU ELFU MOJA NA MOJA

5. MASHIMO YA MFALME SULEIMAN

6. ADILI NA NDUGUZE:- RIWAYA YA SHAABAN ROBERT

7.HEKAYA ZA ABUNUWASI

Interesting

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom