Password nisizozijua kwenye Simu ya Mke wangu!

Password nisizozijua kwenye Simu ya Mke wangu!

We ni mwanaume tena uliyejiweka wazi kwake tumia nafasi ya uanaume wako kumuambia yafuatayo kwa busara:"Mpenzi kwa nini unakosaa uhuru kwenye simu yako?" akikana muulize mbona password zimezidi kwenye simu yako? Unamalizia na kusema hivi basi nitolee hizo password ili niachane na doubt alafu kaza moyo uikague kila kitu maana inaonesha kuna uwepo wa ex wake usije kuta hata mimba sio yako kwa hiyo ex wake anafuatilia maendeleo ya mimba.Narudia tena kagua simu yake hata kwa lazima kwa sababu huyo ni mkeo mambo u private ya nini ila kama hutaki kufanya nilichokuambia jiandae na kukosa amani ya moyo atakutoa confidence zote kwa hiyo doubt uliyonayo kwake LIWALO NA LIWE kuliko kujijibu maswali wakati marking scheem anayo mkeo.
 
Jamani naomba saana ushauri wa dhati. Natamani kujua mke wangu anasiri gani kwenye cm mpaka password na tulikuwa wawili nyumbani likizo nzima mwezi moja akijiandaa kujifungua.

Kaniulizia kama nimeiona cm yake nimekataa. Nataka nitumie usiku wa leo kuweza kujua kilichofichwa ndani.

La sivyo nazidi changanyikiwa mwenzenu nahisi nisipo jib mpakua asabuioi ntakua mwehu!

Kwani niliitoa laini yake ya pembeni nikaweka kwenye cm yangu ikataa kuwaka mpaka pini nimejaribu mpaka mara mbili nikienda ya tatu tu inabrok. Imebaki lain moja ya ndani kwenye cm. Kwani cm yake ni nokia double line. Na kuna meseji imeingia yani wasi wasi tupu ata raha ya mtoto sipati jamani.

Dah tuko tofauti sana hadi amekuwa mkeo bado unashindwa kumwambia unaitaji kujua password za simu yake na bado unaogopa uanaume wako uko wapi sasa?? huyo ni mkeo kitandani mnaenda peku bado mnashindwa kuwa open kwa mabo kama hayo hapo usibembeleze ww mwambie akupe password full stop
 
kumbuka sijawahi kuigusa kwa zaidi ya miezi sita toka nimnunulie. Leo tu tena kwasababu alikuwa anajifungua na mtu alipiga nilipoipokea alikaa kimya akuongea lolote.

Kwenda kuangalia kwenye call log nijue ni nani nichukue namba nimtaalifu mkewangu kajifungua kalazwa ndo nakuta pass word

kumbuka huyu ni mke we umeoa kweli?

mmmh kaka mi ni mwanamke lkn nimeumia sn kwa hii thread yako. Ni km upo shimoni unalia upate mtu wa kukuokoa.
Mpk hapo ulipofikia, sikushauri uache kuichunguza maana hutakaa kwa amani na hutamwamini tena mkeo.
Ebu kaa chini na mkeo muulize kwa utaratibu siri ya cm yake, ww ni mtu mzima naamini utaelewa akiwa anadanganya au anasema ukweli. Ukiona hatoi ushirikiano mtishie kidogo kuwa unaenda kuiflash hiyo cm ili upate ukweli uone reaction yake.
Mkeo ana tatizo hapo kaka jitahidi uling'amue mapema kabla hujazidi kuchelewa.
Mungu akupe hekima ktk hili na akulinde kakangu. Naamini ukweli utadhihirika tu.
 
mleta mada pole pole sana kwa kujidumbukiza kwenye bwawa la NDOA CHETI. jitahidi uogelee fasta utoke kabla hujashuhudia makubwa. God bless you.
NDOA CHETI ndio mtindo unaotumiwa na mabinti wengi kwa sasa, hasa ukiingia kichwakichwa. Ukizubaa mnaunganishwa mtu 3 au 4 kulea 'MJANJA' mmoja
... halafu akileta zake usisahau mambo ya DNA pale TBS.
 
Uzoefu wangu wa mapenzi na ndoa unaonyesha hivi: Ulidanganywa, umedanganywa, unadanganywa na utaendelea kudanganywa kama hutaamu kwa makusudi kuchukua maamuzi ya kiume. Mchunguze huyo mtoto hakika utarudi hapa na thread nyingine yenye siri nzito. Simama kiume amua kuongea wazi wazi na huyo so called mkeo hakika utagundua siri nzito na mwisho naujua. Imewahi kunitokea the same incident kwa aliyetakiwa kuwa wife wangu kabla ya kuja kugundua siri nzito saa 12 kabla ya harusi. So sad aliamua kunywa sumu na akafariki saa chache kabla ya harusi na nilipata matatizo mengi mno na mamlaka ya usalama, but now naishi very peacefull with my new wife. Please take action on this cause kuna something very bad itatokea kwako. Am very sorry for you.
 
Get to your senses buddy...i can smell something fishy in your marriage..
Mwanamke gani wa kulock kila item?...tafakari chukua hatua.....
 
Get to your senses buddy...i can smell something fishy in your marriage..
Mwanamke gani wa kulock kila item?...tafakari chukua hatua.....

jaman mbona hamuelewi mwenzenu? mwenye ujanja wa kuzichakachua password amsaidie huyu best apate ukweli wa matendo ya mkewe...m-pm jamaa anaitwa sharobaro humu anaweza toa msaada, i feel bad unavyotendewa, ol the best na tujulishe matokeo ili tujifunze kitu
 
ukiona vinaelea jua vimeumdwa! ukweli ni kwamba cm ya mkeo si yako hutakiwi kuigusa mpaka akuruhusu lkn kwa jinsi alipofika mkeo unapaswa kuwa na mashaka!
 
Uzoefu wangu wa mapenzi na ndoa unaonyesha hivi: Ulidanganywa, umedanganywa, unadanganywa na utaendelea kudanganywa kama hutaamu kwa makusudi kuchukua maamuzi ya kiume. Mchunguze huyo mtoto hakika utarudi hapa na thread nyingine yenye siri nzito. Simama kiume amua kuongea wazi wazi na huyo so called mkeo hakika utagundua siri nzito na mwisho naujua. Imewahi kunitokea the same incident kwa aliyetakiwa kuwa wife wangu kabla ya kuja kugundua siri nzito saa 12 kabla ya harusi. So sad aliamua kunywa sumu na akafariki saa chache kabla ya harusi na nilipata matatizo mengi mno na mamlaka ya usalama, but now naishi very peacefull with my new wife. Please take action on this cause kuna something very bad itatokea kwako. Am very sorry for you.

Ni kweli mkuu nakubaliana na wewe,unajua wanaopata shida ni dada zetu,ktk matukio kama hayo,katembeaaaa weeee,sasa alikuwa ana hamu ya kuolewa kaolewa bt ma ex wake waliokuwa wanamfanyia mamboz ambao mara nyingi huwa sio waooaji ndo anapagawa nao,mwanaume ukiamua kuoa ni umeamua pia hutakuwa na woga auwasiwasi kwasababu wewe ndo umemtangazia nia ya kumuoa hivyo huna wasiwasi na nafsi yako,na wengi wadada wa sasaivi under 25yr wako hivyo na hivyo vitabia,ulipaswa kumchunguza kabla hujamuoa bro...Ndoa kuna baadhi ya uhuru unatoweka bt wao hawataki kulikubali hilo,unakuwa chini ya mtu,unakuwa chini ya mtu,Thats why unaitwa Mrs.Monaco,nae Mr.Monaco,huu ni mfano tu....
 
....umeanza nae tangu chuo,umegundua mapungufu yake,bado umeng'ang'aniaa...
Labda shida ilianza hapo, mapenzi ni uchizi flani hivi!. Hatusikii, hatuambiwi, tukisgakua pale kati! By the way kwa kuwa jamaa ndo kamuoa huyo binti basi tumsaidie ushauri!
 
Kaka, kwani wifi akiweka password kwenye simu yake wewe utaona poa tu? Manake shem wako akiweka password kwenye sijui kinokia lumia chake, naweka password kwenye mchina wangu hadi ya charger. Yaani ukitak kuichaji inaprompt password. Afu sikilizia mziki wake!
ndugu Mushumbusi simu ya MKE unaitakia nini? GROW UP dude...hayo sio mambo ya kufatilia kabisa...kama mwanaume u have more to work and worry for sio mambo hayo yatakuletea matatizo usiyoyatarajia bure!
 
Get to your senses buddy...i can smell something fishy in your marriage..
Mwanamke gani wa kulock kila item?...tafakari chukua hatua.....

kama ni mtiani ndo umeshanikuta jamani!

Mke wangu alikuwa kaokoka. Tena ni mtoto wa mchungaji kabisa. Hivyo ndivyo vitu vilivyonifanya nimuamini sana. Na kuja kwangu bila cm kwa wakati huo niliamini labda hana watu wa kuongea nao, hana mambo mengi na alihisi inampotezea muda.

Sasa ndo najiuliza zaidi. Pamoja na kuokoka kwake Mbona nilitembea nae kabla ya ndoa. Pili ndoa tuliipanga haraka haraka tukihofia mimba changa aliyonayo isionekane.

Nilikuwa nafumba macho usingizi hauji. Nimesinzia kidogo naota ndoto mbaya sana.

Mungu nisaidie
 
Haaaaaa! Nyie ndio wale never mind.....kila mtu ana "mpango wa kando" nje ya ndoa........! Kuwa makini shetani yu kila mahali
 
kama ni mtiani ndo umeshanikuta jamani!

Mke wangu alikuwa kaokoka. Tena ni mtoto wa mchungaji kabisa. Hivyo ndivyo vitu vilivyonifanya nimuamini sana. Na kuja kwangu bila cm kwa wakati huo niliamini labda hana watu wa kuongea nao, hana mambo mengi na alihisi inampotezea muda.

Sasa ndo najiuliza zaidi. Pamoja na kuokoka kwake Mbona nilitembea nae kabla ya ndoa. Pili ndoa tuliipanga haraka haraka tukihofia mimba changa aliyonayo isionekane.

Nilikuwa nafumba macho usingizi hauji. Nimesinzia kidogo naota ndoto mbaya sana.

Mungu nisaidie

Asee...
Pole mkuu.
Ukiacha simu, hujawahi kumhisi ubaya? Ulokole ni kichaka kibaya kabisa cha waovu...
 
mulika mwizi mkuu hapo hakuna cha kusubiri
 
Back
Top Bottom