Je, Ni Lazima Mpenzi Ajue Password ya Simu Yako?

Je, Ni Lazima Mpenzi Ajue Password ya Simu Yako?

Miss Halima

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
221
Reaction score
479
Wapo wanaosema kwamba mpenzi anapaswa kujua password ya simu ya mwenzake kwa sababu mahusiano yanajengwa juu ya uwazi na uaminifu. Kwa mtazamo wao, mtu asiye na jambo la kuficha hana sababu ya kukataa kushiriki password yake.

Lakini wapo wanaopinga hoja hiyo wakiamini kuwa kuwa kwenye mahusiano hakumaanishi kupoteza haki ya faragha. Password ya simu ni sehemu ya usalama wa taarifa binafsi, na kuitunza haimaanishi kuwa mtu anasaliti au ana siri.

Je, kweli kukataa kumpa mpenzi password ni ishara ya kutokuwa mwaminifu, au ni haki ya kila mtu kulinda maisha yake binafsi?

1785948141252.png
 
Kama amekununulia sawa tu.

Umeshinda kulinda privacy ya UCHI ila unataka kulinda ya simu.

TUTAFATILIA
 
Kwenye Mahusiano kina personal privacy ila ndio wanasema hivyo
 
Password kwenye simu ni dalili ya uwepo wa vimeo au makandokando kwenye mahusiano. Ni mara chache mtu anakuwa na password halafu akose makandokando.
Lazima tu kuna upendo utakuwa unagawanywa kwa mtu/watu wa nje.
 
Katika simu zangu zote tatu, hakuna hata moja niliyoiwekea paswords, nimeshaipangilia tu michepuko yangu muda na saa za kunitafuta, na wote nimewasave majina ya kiume.
 
Wapo wanaosema kwamba mpenzi anapaswa kujua password ya simu ya mwenzake kwa sababu mahusiano yanajengwa juu ya uwazi na uaminifu. Kwa mtazamo wao, mtu asiye na jambo la kuficha hana sababu ya kukataa kushiriki password yake.

Lakini wapo wanaopinga hoja hiyo wakiamini kuwa kuwa kwenye mahusiano hakumaanishi kupoteza haki ya faragha. Password ya simu ni sehemu ya usalama wa taarifa binafsi, na kuitunza haimaanishi kuwa mtu anasaliti au ana siri.

Je, kweli kukataa kumpa mpenzi password ni ishara ya kutokuwa mwaminifu, au ni haki ya kila mtu kulinda maisha yake binafsi?

View attachment 3643910
kuna mambo mkiyakaribisha yawe sehemu ya mahusiano au ndoa yenu ni lazima patokee changamoto ambayo hulegeza uaminifu na kushusha uimara wa mapenzi baina yenu. Ni vizuri kuyakataa katika hatua za mwanzo kabisa za mahusiano yenu na itapendeza zaidi.

na mkiyakaribisha na yakakomaa na kua ni sehemu au utamaduni wa mahusiano yenu, jambo hilo la password haliepukiki 🐒
 
Back
Top Bottom