Pasco na waandishi wenzako...


Hiyo ban kampige mkweo! mi sioni kosa langu hapo.
 
Mkuu Lunyungu, nimepandisha thread ya majibu haya.


Mkuu Pasco umepandishia wapi mie natafuta majibu sioni .Unaweza nimwagia link ya majibu yako mkuu nijionee mwenyewe ?
 
Mkuu Pasco mzee wa majungu bado uko msibani huko Arumeru njoo utupe maelezo ya mapenzi yako na bahasha unazo gawa tafadhali .
Mkuu Lunyungu, kweli wewe ni wa kuniita mimi mzee wa majungu!, of all the people hata wewe?!. Anyway baada ya thread hii kuchafuka kwa kumchanganya member mwingine isiyehusika, nimepandisha thread maalum ya waandishi na bahasha na wewe ukiwa ndio mchokoza mada!.
 

Mkuu Lunyungu,

Shalom.

Sikubahatika kabisa kukuona hapa, kwa vile haya yamewatokea waandishi huko Arusha, na Matinyi ni rafiki yangu, nasikitika sana kwa hayo, tembelea hapa ili tuumalize huu mjadala. https://www.jamiiforums.com/habari-...a-sio-kila-bahasha-ni-rushwa-pasco-wa-jf.html

leo nitamalizia.

Pasco.
 
Kazi ya uandishi wa habari ni kazi ya wito, kama ualimu, commitment yetu ni kuihabarisha jamii na sio kazi ya maslahi, waandishi wa ukweli usafiri wetu ni daladala, hakuna mwandishi wa ukweli mwenye tamaa ya mkoko achilia huo wa bei juu, na nyumba za kupanga ndio nyumba zetu!
 
Nasikia kuna waandishi wa habari wamekamatwa kwa rushwa huko Arusha, je pasco siyo mmoja wao???
Taja, ni kweli mimi ni mmoja wao!.
Taja sikulaumu kuuliza hivyo kwa ukikua utaelewa!.
 
Nimefuatilia hii topic kwa umakini mkubwa na bado sijaelewa, kwamba tuhuma hizi ni za Pasco kama Pasco ama Pasco ametumiwa tu kufikisha ujumbe. Ni kweli kwamba tuna waandishi ambao wanafahamika kuwa ni "waandishi wa bahasha" na wapo waandishi makini wanaofanya kazi zao kwa kuzingatia maadili.

Hivyo si sahihi kuwachanganya wote kapu moja. Tuangalie pia sekta nyingine, wapo polisi ambao hawawezi kukufungulia RB au kwenda kumkamata mtuhumiwa bila kuwapa chochote, lakini kuwapo kwa polisi wa aina hii hakumaanishi kuwa hakuna polisi wanaofanya kazi zao kwa kuzingatia mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi.

Ni vyema wakati tukijadili tutumie maneno ya "baadhi" au "wengi wao". Na suala la specialization si suluhisho la mtu kupokea hongo. Walioingia mikataba mibovu kwa kupewa 10% ni wasomi waliobobea tena wengine wana mpaka PhD. Kwa hiyo suala la ukiukwaji wa maadili ni la mtu na si taasisi au kundi zima.
 
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 
Nawatakia waandishi wenzangu wote wa habari, maandimisho mema ya siku hii ya kimataifa ya uhuru wa habari.
P.
 
Mkuu Lunyungu kwanza pole kwa hii, yote usemayo ni kweli mimi kama mwanahabari, nimeisha vipokea sana hivyo vibahasha na mpaka hapa nilipofika sasa mimi ndio navigawa hivyo vibahasha.
Wanabodi
Leo ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa HabarI, hii ni makala yangu ya pongezi kwa Waziri wetu wa habari,Mhe Paul Makonda kwenye gazeti la Nipashe la Jumapili ya leo. Leo ni Siku ya Uhuru wa Habari:Pongezi Waziri Makonda Kuusema Ukweli Mchungu!,Pesa Ndio Kila Kitu,Hakuna Uhuru Bila Pesa!Waandishi Tafuteni Pesa!.

Nimempongeza Makonda kwa kuusema ukweli mchungu kuhusu tasnia ya habari ya kisasa,hakuna kitu cha bure!kila kitu ni pesa!,pesa ndio kila kitu,hakuna uhuru wa habari,bila uhuru wa kiuchumi,hakuna uhuru bila pesa!,ametutaka waandishi wa habari tutafute pesa!.

Nawapongeza waandishi wenzangu wote wa habari kwa siku yetu hii ya kimataifa ya uhuru wa habari,kwa msisitizo wa alichokisema Waziri Makonda,kuwa siku hizi,hakuna kitu cha bure!,kila kitu ni pesa,hata habari ni pesa, hivyo waandishi tutafute pesa!。

Mungu Mbariki Waziri Makonda
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…