Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,712
22,297
Pascal Mayala(CCM) alipopata uwakili nilimuuliza kama atakuwa wakili wa wanaccm tu na mwanachadema ambaye siku zote ana hasira naye ataweza kumtetea? Swali langu lilitokana na dunia kuwa duara, tenda ulitendalo lakini kuna siku utakwama na kuwarudia unaowachukia.

Pasikali asiyewapenda wanachadema leo anawaomba watanzania wote(sijui kama wanachadema nao ni watanzania) bila kujali tofauti zao wamchangie pesa aweze kugombea ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki!

Huyu Paskali anachohitaji pesa tu za kumuwezesha kugombea ubunge tu na atakapoupata atawashukuru wanaccm na viongozi wake, Pascal atajipambanua yeye ni mbunge kupitia CCM na si watanzania, tukumbuke hii ni EAC.

Pascal ajue umchukiae kesho atakuja kukufaa na siasa hazihitaji chuki za binafsi.
 
Tumsapoti tu, show luv, adui siku zote mwache aone Miujiza ya Mungu juu yako. Akifa hataona makuu yanayotendwa na Mungu baba
Hajawahi kupiga magoti na kutambaa kama nyoka kwa kujifanya mnyenyekevu kisa pesa, angekuwa nazo asingekuwa mnyenyekevu, ananitia mashaka kuwa akifanikiwa chuki itaongezeka dhidi ya Chadema kwani atajiona yeye ni mbunge wa CCM.
 
Me nadhani tumchangie kaa Mtanzania akipata sawa ni watanzania wamepata akijifanya ni mwamba as mwanaccm basi tunatunza daftari kwani kesho bado kuna maisha.

👉🏾Naendelea kujifunza tabia ya binadamu.
Sijasema tusimchangie, kumbuka hata misibani watu husimangwa na wengine kususiwa chakula kutokana na matendo yao.
 
Pascal Mayala(CCM) alipopata uwakili nilimuuliza kama atakuwa wakili wa wanaccm tu na mwanachadema ambaye siku zote anahasira naye ataweza kumtetea? Swali langu lilitokana na dunia kuwa duara, tenda ulitendalo lakini kuna siku utakwama na kuwarudia unaowachukia.

Pasikali asiyewapenda wanachadema leo anawaomba watanzania wote( sijui kama wanachadema nao ni watanzania) bila kujali tofauti zao wamchangie pesa aweze kugombea ubunge wa Jumuia ya Afrika Mashariki!

Huyu Paskali anachohitaji pesa tu za kumuwezesha kugombea ubunge tu na atakapoupata atawashukuru wanaccm na viongozi wake, Pascal atajipambanua yeye ni mbunge kupitia CCM na si watanzania, tukumbuke hii ni EAC.

Pascal ajue uumchukiae kesho atakuja kukufaa na siasa hazihitaji chuki za binafsi.
wewe kama unataka kumchangia mchangie tu haya mengine yanatoka wapi?kwani chadema ni nini?na nani alikuambia Pasckali ni wakili wakati aliishawambia yeye hajapractice hiyo taaluma.acheni roho mbaya ukitaka kumsaidia mtu msaidie uchama unatoka wapi.mtakuja hata kubaguana kwenye familia.vyama hivi havina msaada wowote.
 
Kwani watu hawabaguani kwenye familia! Leo ndiyo unajua vyama havina msaada! Swala la uwakili rejea mabandiko yaliyomo humu na simulizi zake.
 
Back
Top Bottom