Partner kwenye biashara, anataka twende mbali zaidi

Partner kwenye biashara, anataka twende mbali zaidi

Kama humpendi mwache na biashara ya pamija mvunje, maana hamtaweza kukaa pamoja kama utaoa mke mwingine. Mchukue huyo partner ndiyo mke atakae kufaa. Ukudharau basi fanya upendavyo
Kuvunja sio tatizo tatizo ni mzunguko wa biashara lazima utayumba kwa kila pande na hiyo inaweza pelekea mmoja wetu kupotea ki biashara na lazima utamsaidia maana mmetoka mbali ngumu kumuacha,Ahsante nimeuzingatia huo ushauri wako mkuu
 
Good luck mkuu..... bila shaka mna vya kujadili na kukubaliana kabla ya kufikia kuoana. Lazima mkubaliane mambo ya msingi.
 
muulize huyo patna why now? wekaneni wazi ndiyo uamue. na muweke plan jinsi biashara itakuwa na mambo ya hisa. msije chinjana huko mbele.
 
Siku nikiambiwa KikulachoChako nakupenda sana.....nahisi nitazimia hapo hapo kwa masaa yasiyo pungua matatu....na nikizinduka nitazimia tena kwa mshangao.....na nikizinduka nazimia tena kwa wasi wasi.....

Kuna watu wanabahati huko duniani.....yaani kabisa katoto ka kike kanakuambia live NAKUPENDA
Hahaha mpwaaaaaaaaaaa
 
Mkuu huoni nitakuwa nimeidhurumu nafsi ya binti wa watu kuwa mwezi wa 7 namtolea posa afu kwa tabia za mabinti lazima atakuwa tayari ameshazinyetisha hizo habari kwa baadhi ya ndugu Ake

Piga moyo konde mkuu...kamata partner kwa raha zakoo.....
 
Haahaha mkuu "eti huko duniani..
Mkuu huyu binti hatujajuana ki mjini mjini ni miaka 6 ujue afu wote mnajuana kwenye mazingila ya hatari,
Magendo na wale Askari wa mpakani unaweza kujikuta unanyang'anywa kila ulichonacho na hata nauli unakosa lakini binti anakusaidia ndio maana hata yeye mwenyewe nadhani ananishangaa kwa nini sikuwahi mwambia nampenda maskini mimi nilikuwa nikimchukulia kama dada tu.
Alishawahi kamatwa na sukari na power(pombe ya Malawi) kama si mimi dada wa watu angekuwa jela bahati nzuri tayari mimi nilishasafisha njia kwa hiyo nikawambia wale Askari mkuu nilishamuona na mzigo ni wangu akaachiwa mpaka leo huwa hasahau hilo
Mkuu hilo neno NAKUPENDA ni neno lenye heshima sana.....kwa hiyo litendee haki kwa kumpenda kwa dhati huyo binti mwenye ujasiri na mapenzi ya dhati kwako.....
 
Mapenzi haya heheheh huhuhuhu hureeeeee, itakuwa mbaya sana ukimuacha huyo patna na biashara itayumbaje wakati wote mlikuwa wamiliki buana?!. Kwa kichwa zha patna wako atazidi kukuona bonge la mtu.Ni kuongeza kionjo cha mapenzi tu maana maisha mengine mlishayapitia. Baraka zote mi nawagawia hureeee
 
Mkuu Ngamia kuna mambo lazima ujiulize kwa nini leo na sio huko nyuma na hata dalili zamani hakuwa akinionyesha za kunitaka namjua ni mtu wa misimamo na anaesimamia anachokiamini kwa hili kaniweka kwenye mawazo.
Tatizo umeshaanza doubts, kukitokea kutokuelewana ndo shida itaanzia hapo. Wewe unampenda patner?
 
Si unaona sasaa!! Hayo madharau kwa dume, yaani unakaa na demu miaka 6 mpaka anakuja kukutongoza? Umenisikitisha sana asee. Atakuwa alishakuonyesha kila ishara ila ulifunga macho na masikio.
 
Back
Top Bottom