Partner kwenye biashara, anataka twende mbali zaidi

Partner kwenye biashara, anataka twende mbali zaidi

Mwanamke sahihi anayekufaa hapo ni huyo partiner kumbuka umedumu nae kwenye biashara kwa muda mrefu.
Mnafahamiana kiundani kutokana na kushare biashara zenu.
Suala la kwamba kwa nin hakukwambia tangu kipindi cha nyuma ni kwakuwa alihitaji kukusoma zaidi kukujua uko vipi...Kitu pekee ni wewe kumwambia ukweli huyo partiner kwamba ulikuwa na msichana hata hivyo haujafika mbali nae huyo msichana.
Muelezee ni kwa jinsi unaona yeye anafaa kuwa mkeo,mwisho kabisa mkubalie ili mkahalalishe ndoa.

Naamini huyo partiner ana faida kubwa kwako kifamilia na hata kibiashara.
 
ila biashara ukiichanganya na mapenzi sometimes inakua complicated sana, yaani mapenzi yakiyumba biashara na yenyewe inayumba sana
Ewaaa mkuu na hiyo ndio hofu yangu ndio sababu sijampa jibu mpaka leo japo namuamini sana kwenye mipango ya biashara yuko vizuri mno
 
Siku nikiambiwa KikulachoChako nakupenda sana.....nahisi nitazimia hapo hapo kwa masaa yasiyo pungua matatu....na nikizinduka nitazimia tena kwa mshangao.....na nikizinduka nazimia tena kwa wasi wasi.....

Kuna watu wanabahati huko duniani.....yaani kabisa katoto ka kike kanakuambia live NAKUPENDA
 
mkuu unaonekana ni kama umeshafanya maamuzi kwa partner just reading between the lines
 
Natumai hamjambo na mnaendelea na kukulu kakala za utafutaji,
Ni miaka 6 sasa nilipokutana na binti mipakani nikifanya biashara Enzi hizo ilikuwa ni biashara za magendo Kasumuru/Tunduma pia yeye nae alikuwa na biashara yake haikuwa halali tulisaidiana kila baya lilipomkuta mmoja wetu tumeenda hivyo mpaka mnamo mwaka 2012 mwishoni nilipomwambia mimi nataka niache biashara hizi za mipakani akaniambia na yeye anampango huo tena anahama na kutaka kuhamia Dar na akasema kama niko tayari tuungane na kuiunganisha mitaji yetu ili tuwe vizuri.

Tukakubaliana na tukafanya hivyo safari yetu ilitufikisha Dar na kutafuta nyumba ya kuishi tukapata nyumba mtaa mmoja lakini ni nyumba mbili tofauti, baada ya hapo tukaingia kusaka Fremu ya duka K/koo MUNGU mkubwa tukapata na kuilipia japo ilikuwa gharama lakini nilimshauri mwenzangu hela yake ianze kulipa pango la biashara.

Tumefanya biashara kwa mafanikio makubwa kwani sasa tayari tuna maduka mawili tatizo lilianza wiki iliyopita mwenzangu alipoamua kuniambia nanukuu " (jina) nimekaa na wewe kwa mda mrefu sana nimekujua unanijua lakini hata siku moja hukuwahi nidharau naomba nitakayokwambia usinidharau au kunifikilia vibaya.

Nikamjibu wewe sema tu akaniambia ananipenda sana na anaomba niwe mume wake kwani siku nyingi amekuwa akiumia na siri hiyo"niseme tu hapa kazini wengi wanajua ni mdogo wangu jinsi tunavyoishi na nadhani hata mimi ndio nilivyokuwa nikimchukulia kwani hata urembo wake sikuwa nikiutazama kwa kumtamani nikimchukulia kama dada of course ni Cute na kule kutomuona akijishughurisha na wanaume nikajua ni ule u busy wa kazi maana kila siku saa 11 asubuhi kazini na kutoka 12 mpaka folen hizi 4 usiku home hiyo J'pili ya mapumziko akitoka church ni kazi mpaka jioni, mimi nina msichana wangu siwezi muita demu anajieshimu japo sijamjua vema nilianzisha uhusiano nae ni kama miezi 8 iliyopita japo saivi kaamishwa kikazi lakini tuko vizuri ki mawasiliano nikili tu Nampenda".

Nilimjibu partner kuwa nitampa jibu aniache nitafakari wakuu mimi ni mtoto wa kiume nimefikilia wiki nzima nimeona acha tu nikae kwa huyu partner.
Huyu mpenzi wangu tayari tulishaanza kupanga mwezi wa 7 nikatoe posa kwao kosa kubwa sikuwahi mshirikisha partner kuhusu mahusiano yangu na hiyo mwanamke wangu nikijua mapema sana lkn kwa hili alilokuja nalo sasa naona Nimkubalie kwa masrahi ya ustawi wa biashara zetu japo tunaweza kugawana lakini hofu yangu kwa hari ilivyo sasa kiasi tutayumba ama mimi au yeye na hatuwezi kutupana tumetoka mbali.

Msaada wa ki mawazo member nigeuze partner awe mke au niendelee na mausiano yangu na msichana wangu.
Kwnyw suala la mapenzi,ushauri mzuri ni kufuata moyo wako tu,unweza ukamkubalia kwa kisingizio cha kuokoa biashara yenu,lkn mwisho wa siku ukagundua kuwa hukumpenda na ukakosa amani mwisho wa siku mkaachana na ukajikuta unapoteza vingi.
 
jipe mda wakufikiria na jiulize jee anazo sifa za kua mkeo wako na mama wa Watoto wako? moyo ukikubali mshirikishe mwenyezi mungu na muombe kama huyo mke ana kheir na wewe basi akufanyie wepesi na kama ana shari na wewe akuepushie na wala usijute...
Amina mkuu ndio maana sijutii kulisema hili hapa
 
Mwanamke sahihi anayekufaa hapo ni huyo partiner kumbuka umedumu nae kwenye biashara kwa muda mrefu.
Mnafahamiana kiundani kutokana na kushare biashara zenu.
Suala la kwamba kwa nin hakukwambia tangu kipindi cha nyuma ni kwakuwa alihitaji kukusoma zaidi kukujua uko vipi...Kitu pekee ni wewe kumwambia ukweli huyo partiner kwamba ulikuwa na msichana hata hivyo haujafika mbali nae huyo msichana.
Muelezee ni kwa jinsi unaona yeye anafaa kuwa mkeo,mwisho kabisa mkubalie ili mkahalalishe ndoa.

Naamini huyo partiner ana faida kubwa kwako kifamilia na hata kibiashara.
Inawezekana mkuu maana anamisimamo ya hatari sana kuna kipindi alikuja na story ya mapenzi lakini akataka nimshauri lakini baadae akaniambia ni kama ikatokea,Sasa nimemuelewa nini alikuwa anataka nijue.
Ahsante kwa ushauri wako unaizidi kunipa mwanga wa hili maana liko kwenye hatma ya maisha ya kibiashara na kimapenzi
 
Fimbo ya mbali haiui nyoka mkuu. Huyo aliyekaribu na wewe ndio akufaaye tena mmedumu katika utafutaji miaka nenda miaka rudi. Huyo mwingine mpotezee ataelewa tu mchezo japo jiandae maana anaweza kuja kufuatilia kisa ya cha yeye kutoswa.
 
Kama humpendi mwache na biashara ya pamija mvunje, maana hamtaweza kukaa pamoja kama utaoa mke mwingine. Mchukue huyo partner ndiyo mke atakae kufaa. Ukudharau basi fanya upendavyo
 
Siku nikiambiwa KikulachoChako nakupenda sana.....nahisi nitazimia hapo hapo kwa masaa yasiyo pungua matatu....na nikizinduka nitazimia tena kwa mshangao.....na nikizinduka nazimia tena kwa wasi wasi.....

Kuna watu wanabahati huko duniani.....yaani kabisa katoto ka kike kanakuambia live NAKUPENDA
Haahaha mkuu "eti huko duniani..
Mkuu huyu binti hatujajuana ki mjini mjini ni miaka 6 ujue afu wote mnajuana kwenye mazingila ya hatari,
Magendo na wale Askari wa mpakani unaweza kujikuta unanyang'anywa kila ulichonacho na hata nauli unakosa lakini binti anakusaidia ndio maana hata yeye mwenyewe nadhani ananishangaa kwa nini sikuwahi mwambia nampenda maskini mimi nilikuwa nikimchukulia kama dada tu.
Alishawahi kamatwa na sukari na power(pombe ya Malawi) kama si mimi dada wa watu angekuwa jela bahati nzuri tayari mimi nilishasafisha njia kwa hiyo nikawambia wale Askari mkuu nilishamuona na mzigo ni wangu akaachiwa mpaka leo huwa hasahau hilo
 
Kwnyw suala la mapenzi,ushauri mzuri ni kufuata moyo wako tu,unweza ukamkubalia kwa kisingizio cha kuokoa biashara yenu,lkn mwisho wa siku ukagundua kuwa hukumpenda na ukakosa amani mwisho wa siku mkaachana na ukajikuta unapoteza vingi.
Kweli mkuu lakini kwa sasa acha nimpe nafasi Partner nadhani kwa huyu ni rahisi zaidi kuongea lugha moja kwenye maisha mda mwingine ni vizuri kufuata akili na sio moyo.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Jamani na mimi ni team PARTNER, muoe huyo dada haraka sana.
 
Fimbo ya mbali haiui nyoka mkuu. Huyo aliyekaribu na wewe ndio akufaaye tena mmedumu katika utafutaji miaka nenda miaka rudi. Huyo mwingine mpotezee ataelewa tu mchezo japo jiandae maana anaweza kuja kufuatilia kisa ya cha yeye kutoswa.
Na akijua ndio shida itakapokuja maana mpenzi anamjua partner kama dada ila partner hajawahi kumjua kuna kipindi nilitaka kumjulisha partner lakini nikajishauri nijipe muda
 
Back
Top Bottom