JembePoli
JF-Expert Member
- Jul 14, 2015
- 1,324
- 995
Natumai hamjambo na mnaendelea na kukulu kakala za utafutaji,
Ni miaka 6 sasa nilipokutana na binti mipakani nikifanya biashara Enzi hizo ilikuwa ni biashara za magendo Kasumuru/Tunduma pia yeye nae alikuwa na biashara yake haikuwa halali tulisaidiana kila baya lilipomkuta mmoja wetu tumeenda hivyo mpaka mnamo mwaka 2012 mwishoni nilipomwambia mimi nataka niache biashara hizi za mipakani akaniambia na yeye anampango huo tena anahama na kutaka kuhamia Dar na akasema kama niko tayari tuungane na kuiunganisha mitaji yetu ili tuwe vizuri.
Tukakubaliana na tukafanya hivyo safari yetu ilitufikisha Dar na kutafuta nyumba ya kuishi tukapata nyumba mtaa mmoja lakini ni nyumba mbili tofauti, baada ya hapo tukaingia kusaka Fremu ya duka K/koo MUNGU mkubwa tukapata na kuilipia japo ilikuwa gharama lakini nilimshauri mwenzangu hela yake ianze kulipa pango la biashara.
Tumefanya biashara kwa mafanikio makubwa kwani sasa tayari tuna maduka mawili tatizo lilianza wiki iliyopita mwenzangu alipoamua kuniambia nanukuu " (jina) nimekaa na wewe kwa mda mrefu sana nimekujua unanijua lakini hata siku moja hukuwahi nidharau naomba nitakayokwambia usinidharau au kunifikilia vibaya.
Nikamjibu wewe sema tu akaniambia ananipenda sana na anaomba niwe mume wake kwani siku nyingi amekuwa akiumia na siri hiyo"niseme tu hapa kazini wengi wanajua ni mdogo wangu jinsi tunavyoishi na nadhani hata mimi ndio nilivyokuwa nikimchukulia kwani hata urembo wake sikuwa nikiutazama kwa kumtamani nikimchukulia kama dada of course ni Cute na kule kutomuona akijishughurisha na wanaume nikajua ni ule u busy wa kazi maana kila siku saa 11 asubuhi kazini na kutoka 12 mpaka folen hizi 4 usiku home hiyo J'pili ya mapumziko akitoka church ni kazi mpaka jioni, mimi nina msichana wangu siwezi muita demu anajieshimu japo sijamjua vema nilianzisha uhusiano nae ni kama miezi 8 iliyopita japo saivi kaamishwa kikazi lakini tuko vizuri ki mawasiliano nikili tu Nampenda".
Nilimjibu partner kuwa nitampa jibu aniache nitafakari wakuu mimi ni mtoto wa kiume nimefikilia wiki nzima nimeona acha tu nikae kwa huyu partner.
Huyu mpenzi wangu tayari tulishaanza kupanga mwezi wa 7 nikatoe posa kwao kosa kubwa sikuwahi mshirikisha partner kuhusu mahusiano yangu na hiyo mwanamke wangu nikijua mapema sana lkn kwa hili alilokuja nalo sasa naona Nimkubalie kwa masrahi ya ustawi wa biashara zetu japo tunaweza kugawana lakini hofu yangu kwa hari ilivyo sasa kiasi tutayumba ama mimi au yeye na hatuwezi kutupana tumetoka mbali.
Msaada wa ki mawazo member nigeuze partner awe mke au niendelee na mausiano yangu na msichana wangu.