Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,195
- 1,661
Moja ya misafara nilojifunza vitu vikubwa ndani ya muda mfupi , ni huu msafara niloamua kwenda kutalii Falme za kiarabu.
Nilianza Sharjah, huko nikakuta ni magodown ya bidhaa used yamejaa. Nikaenda Abuu dhabi kule ni makazi ya matajiri wa kiarabu na ndiko balozi za nchi mbali mbali ziliko. Nikamalizia Dubai hapo ndipo penye bidhaa original. Ziara yote hii ilikuwa ndani ya siku saba .
Ndani ya siku saba hizi, ilipofika jumapili maduka mengi hawafungui ni kama mapumziko. Nami nikaona ni fursa ya kutembelea Dubai mall sambamba na Burji khalifa.
Kutoka Samaya Hoteli nilikofikia hadi Dubai mall unatumia usafiri wa treni inayopita chini ya ardhi. Ndani ya treni wameweka tangazo la wanawake kukaa upande wao ,endapo mwanaume atakaa upande wa akina mama na askari akamkuta fani ni Dirham (AED) 200 kama tzs 127,000 hivi. (Dirham moja ni sawa na tzs 635 hivi)
Niseme Dubai hawatumii sharia za kiislam kwa 100% kama wanavyotumia Saudi Arabia, ila wamejitahidi kuheshimu uislam mfano barabara wameziita majina ya maswahaba (wanafunzi) wa mtume kama bara bara ya Abuubak Swidik (Khalifa au kiongozi wa kwanza wa uislam baada ya kufariki mtume mwaka 633), Bara bara ya Umar bin Khatwab (Khalifa au kiongozi wa pili wa uislam baada ya kufariki Abuubakr Swidik mwaka 635) , na bara bara ya Khaalid bin Waalid (Komandoo hodari wa ulinzi zama za mtume na makhalifa).
Pia kwenye vyumba vya hotel kwa juu kuna mshale unakuelekeza kibla (mahali waislam wanakotakiwa waelekee wakiwa wanaswali ambako ndiko iliko makkah)na wanakuwekea muswala (kijizulia ) wa kuswalia,
Basi, Treni inatufikisha Dubai Mall ,hapo kuna screen unasearch kama google unataka kwenda wapi ,kisha inakuonesha ramani na njia ya kufika uendako, maana humu kila maduka ya brand zote maarufu duniani. Lakini kubwa lilonipeleka ni aina ya samaki na viumbe walokusanywa humu unawaona kwa kulipia. Ukitaka pia kuna eneo la kujifunza ndege za emirate ila hauruki,ziko hapo hapo ardhini.
Kuona vivutio hapa Dubai mall pekee kabla ya Burji khalifa unalipia kama Dirham 400, na kama hautaki kukaa foleni unalipia Dirham 500 unapewa beji ya fast track , Hapo wahudumu wanasubirisha watu wengine ili mtangulie kwa kila hatua ya kivutio. Hadi hapa siyo lengo la makala yangu, bali hatua inayofuata.
Baada ya kumaliza vivutio vya Dubai mali, tukakata tiketi ya kupanda Burji khalifa, hapo unalipa kwa kadri unataka uishie floor ya ngapi. Kuna hatua tatu za floor .
Tuje mpaka juu ya jengo refu kuliko yote duniani. Jengo hili wenyeji wameliita Burji Khalifa.(Khalifa Tower) Nikisema refu namaanisha ni refu, umbali wa mita 828 toka Ardhini . uunganishe viwanja nane vya mpira wa miguu kisha uvisimamishe.
Hapo kuna hisia mbili unazipata ukiwa umbali huo. Moja furaha kuouona mji mzuri wa Dubai tokea juu.
Pili unapata hofu fulani unajiuliza kama tetemeko la ardhi likitokea?
Ziara inaisha Ninarudi hotelini .
HAPA NDIYO FIKRA ZANGU NAPENDA KUSHARE NANYI
Umri huu wa kulekea miaka 40 inahitaji upate walau dakika 60 za kutafakari kila siku.Hapa Napata muda wa kutafakari na ndiyo napenda kushare nanyi tafakari zangu., naangalia picha za mchana kutwa nakutana na vuta picha ya Dubai kabla ya 1970 ilikuwa sawa na nchi nyingi zinazoendelea, Lakini imezipita ghafla . Hapa nauliza wazoefu wa huu mji kwani Dubai wana mafuta kiasi gani? Kwa kifupi anasema wanakaribiana na Nigerian. Hapa nambandika swali lingiine fikirishi kwa nini Dubai imepiga hatua kubwa? Hapo kanipa siri kubwa ya akili ya uongozi alotumia Mfalme wa Dubai ,Mohamed bin Rashid Almaktoum, kwa kuona mafuta ya UAE , 94% yapo Abuu Dhabi , 2% yako Sharjah na Dubai wana 4% tu ya mafuta yote ya UAE ,alichofanya ni kugeuza Dubai kuwa mjii wa kibiashara. Baadhi ya mambo ya mapinduzi alofanya ni :
Sheria ya usajili na uwekezaji ambapo mwekezaji toka nje ya nchi, anatakiwa kuwa partner na mwenyeji raia wa Dubai. Na hapa maduka ya jumla mengi tulopita mabosi wa kwanza ni waarabu (wanaongea kiarabu zaidi) ambao wanakuwa zao majumbani ,kisha watendaji wa kila siku wanakuwa wahindi(wanaongea kiingereza) na wasaidizi kama kukaribisha wageni na kuwatembeza wanakuwa wengi ni waafrica magharibi(Wanaongea kifaransa na kiingereza) .(Alhamdulillah, lugha zote tatu nazielewa hivyo nawatafsiria watanzania watalii wenzangu).
- Bidhaa toka nje zimeshushwa ushuru zaidi ili kuvutia makampuni kuleta bidhaa Dubai kwa kuwa Dubai hawazalishi bidhaa ila zinaingizwa toka nje hasa Japan, Taiwan na nchi zingine.
- Kununua bidhaa Dubai kwa wageni unarudishiwa ushuru kwa kuwa hahuuzii pale ,utauzia nje ya Dubai .Hivyo ukishanunua ,wale wenye maduka ya jumla wanakuandalia fomu ya kudai (claim back) ushuru ulotozwa kwenye bidhaa.
- Kitaalamu kama watu wengi wanaleta bidhaa na wengi wanafuata bidhaa unahitaji usafiri, na hapo shirika lao la ndege emirate likatumia fursa hiyo kuyapiku mashirika yote ya ndege duniani na kuwa uwanja ulio busy kwa ndege duniani ni emirate (DXB)
- Ukiwa na wateja wanakuja na usafiri wako hapo unabuni utalii hata kama hauna vivutio.Utalii wa Dubai ni majengo marefu yalojengwa mpaka majengo mengine hayana wakazi wala si ofisi , yamejengwa kufanya mji uvutie.
- Usalama wa hali ya juu. Ndani ya Dubai ni kazi kuona bastola hadi namaliza siku 7. Pia kwenye maeneo ya watu wengi ,polisi wamepaki gari zao aina ya VX masaa 24 na juu kuna Camera wanafuatilia nani anavunja sheria
Ni usiku mwingi sasa, inabidi kulala asubuh tuwahi Baniya square (Kariakoo ya Dubai) kufunga mzigo.