Rais Samia, Mkataba huu utamomonyoa 'sovereignty' ya Tanzania

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
1686215622420.png

Usuli

Mheshimiwa Rais Samia, Tanzania kama Taifa huru linayo haki ya kutowajibika kwa Taifa jingine lolote duniani, na haki hii ndiyo inaitwa "sovereignty" kwa Kiingereza. Hivyo, katika maneno 700 pekee, najadili Mapatano kati ya Serikali za Tanzania na Dubai kwa kugusia yafuatayo: utangulizi, muundo wake, maudhui yake, mazuri yake, mabaya yake, na mapendekezo.

Nitapendekeza kwamba, kwa kuwa mapatano haya ni hatari kwa usalama wa nchi ya Tanzania, na kwa kuwa yanamomonyoa "sovereignty" ya Taifa letu, basi hayafai. Mapatano haya yanaweza kuleta utumwa mamboleo na kuliweka Taifa tena chini ya himaya ya wageni waliowachuuza mababu zetu kwa miaka 400 kama bidhaa sokoni. Naomba ukataliwe na Bunge hadi hapo utakaporekebisha dosari nitakazozionyeha.

Utangulizi

Oktoba 2022, Profesa Makame Mbarawa, akiwa anaiwakilisha Serikali ya Tanzania, na Ahmed Mahboob Musabih, akiwa anaiwakilisha Serikali ya Falme za Kiarabu (UAE), walisaini Mapatano ya Kiserikali (IGA) kwa ajili ya kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Dubai.

Katika kutekeleza Mapatano haya, Tanzania itawakilishwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Dubai itawakilishwa na “Dubai Ports World (DPW).” DPW ni kampuni ya kimataifa ya usafirishaji yenye makao yake makuu Dubai, inayomilikwa na serikali ya Dubai.

Tayari barani Afrika, DPW inafanya kazi ya kuendesha bandari nchini Algeria, Angola, Djibouti, Misri, Msumbiji, Nigeria, Rwanda, Senegal, Somaliland na Afrika Kusini. Yaani, bandari hizi zote zinaunda “Dubai Ports World.”

Kwa asili yake, Mapatano kati ya nchi mbili ni lazima yaidhinishwe na mabunge ya nchi husika. Nchini Tanzania, mapayano haya yanatarajiwa kuidhinishwa tarehe 10 Juni 2023.

Kama mapatano haya yataidhinishwa, DWP itarithi kampuni binafsi iitwayo TICTS iliyoendesha eneo la makontena ya Bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 30 hadi 2022 ambapo Serikali ya Tanzania iliamua kutoendelea na mkataba huo ili kutafuta mwekezaji mwingine wa kimkakati kutoka nje ya nchi.

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo lango kuu la kibiashara la Tanzania, ambapo takriban asilimia 95 ya biashara ya kimataifa ya Tanzania inahudumiwa na bandari hii.

Pia, bandari hiyo inayo mageti 12 yanayotumika kupokea mizigo kutoka nje ya nchi. Inahudumia nchi jirani zisizo na bandari kama Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda na Zimbabwe.

Muundo wa Mapatano

Mapatano haya yamegawanyika kwenye sehemu tano. Yaani, Fasili, tafsiri na mipaka ya miradi (ibara 1); majukumu ya jumla (ibara 16); masuala yanayohusu sheria za kifedha (ibara moja); Vifungu vya majumuisho (ibara 13); na Viambatanisho viwili.

Kiambatanisho cha kwanza ni maeneo ya ushirikiano, ambayo ni tisa, maeneo saba yakiwa awamu ya kwanza, na mawili awamu ya pili. Na Kiambatanishi cha pili ni vibali vya marais wa nchi mbili kwa wawakilishi wao waliosani mkataba kwa niaba yao. Mkataba inazo ibara 31 kwa ujumla.

Maudhui ya Mapatano

Kwa mujibu wa ibara ya pili ya mapatano, malengo ya mapatano haya ni:

Serikali ya Dubai itatafuta na kuleta mtaji wa kifedha na mtaji wa rasilimali watu mitaji itakayosababisha kufanyika kwa uendelezaji, uboreshaji, menejimenti na uendeshaji wa bandari zilizo katika maziwa na bahari, maeneo maalum ya kiuchumi, vituo vya utunzaji na usafirishaji wa mizigo, korido za kibiashara, na miundombinu anwai ya banadari.

Pia, serikali ya Dubai inayo dhamira ya kufanya ujenzi wa uwezo wa Watanzania; uhamisho wa maarifa, stadi, na tekinolojia kutoka Dubai kuja Tanzania; uimarishaji wa taasisi za mafunzo; na ukuzaji wa taarifa za intelijensia ya kibiashara.

Mazuri ya Mkataba

Taarifa kwamba, serikali ya Dubai itakuja na mtaji wa kifedha na rasilimali watu utalaosababisha kufanyika kwa uendelezaji, uboreshaji, menejimenti na uendeshaji wa bandari zilizo katika maziwa na bahari, maeneo maalum ya kiuchumi, vituo vya usafirishaji, korido za kibiashara, na miundombinu anwai ya banadari, ni habari njema.

Pia, dhamira ya kufanya ujenzi wa uwezo wa Watanzania; uhamisho wa maarifa, stadi, na tekinolojia kutoka Dubai kuja Tanzania; uimarishaji wa taasisi za mafunzo; na ukuzaji wa taarifa za intelijensia ya kibiashara; ni habari inayovutia.

Mabaya ya Mkataba

Kwanza, mapatano hayasemi serikali ya Dubai italeta mtaji wa fedha kiasi gani; hauelezi aina ya ujuzi utakaohamishiwa Tanzania; hakuna vigezo vya kupima kasi ya ufanisi wa miradi inayokushdiwa kutekelezwa.

Pili, mapatano ayanaifunga mikono na miguu serikali ya Tanzania, kiasi kwamba, serikali ya Dubai inaweza kufanya lolote na vyvovyote, bila serikali ya Tanzania kusema hapana. Mfano wa kwanza ni ibara ya 7(3) inayosomeka hivi:

1686631049714.png

Pia, mfano mwingine wa tatizo hili ni ibara ya 23(4) inayosomeka hivi:

1686217386210.png

Tatu, mapatano yamesahau kifungu muhimu kuliko vyote: mgawanyo wa mapato yatakayopatikana kutokana na ushirikiano huu. Ukiachana na misamiati ya jumla, hakuna maelezo yenye kuonyesha nchi ya Tanzania itafaidika nini kwa kutaja takwimu halisi. Kwa kimombo kilichosahaulika hapa ni "revenue sharing model."

Nimeshiriki katika uandishi wa “strategic alliance agreements” nyingi, lakini sijawahi kuona “strategic alliance agreements” mbovu kama hii. Hakuna "strategic alliance agreement" isiyotaja "revenue sharing model."

Yaani, mwisho wa siku kila upande unapaswa kujua haki zake ni zipi, kulingana na kiwango cha rasilimali kilichoingizwa katika mradi wa pamoja. Profesa Makame Mbarawa ametuangusha.

Nne, mapatano haya yanaonekana kuwa ni kama "mkataba wa urafiki wa milele", yaani kama ule mkataba wa Chifu Mangungo wa Musovero na mkoloni aliyeitwa Karl Peters.

Mapatano hayataji ukomo wa uhai wake kabisa! Mwanasheria wetu mkuu naona hakushirikishwa. Siku hizi hakuna mkataba au mapatano yasiokuwa na aya ya urefu wa uhai wake, yaani "contract/agreement term."

Kwa ufupi, bila kutaja "revenue sharing model" na bila kueleza urefu wa uhai wa mapatano, ni mambo ambayo yanaashiria ubabaishaji unaoweza kuzalisha mahusiano ya mfuga mtumwa na mtumwa, kati ya Tanzania na Dubai. Tusipokuwa makini historia ya "Tanzania Koloni Jipya la Dubai" itaandikwa.

Tano, ni kwamba, bandari, viwanja vya ndege, na barabara za zinazounganisha nchi na nchi huwa ni maeneo ya kimkakati katika masuala ya usalama wa nchi.

Kuziweka bandari zetu mikono mwa serikali ya nchi nyingine inayosimamia “Dubai Ports World,” na hivyo kuzifanya bandari hizi sehemu ya “Dubai Ports World,” ni sawa na kuimega nchi yetu na kuiweka chini ya Taifa jingine.

Sita, mapatano yanaongelea utoaji wa vibali vya "haki ya kumiliki ardhi" kwa Dubai. Vibali kama hivi vilipotolewa kwa wawekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi vilileta mgogoro wa kumega utaifa wetu.

Kuna wawekezaji walivitumia kama dhamana kwenye mabenki ya nje na kupata mkopo wa kibiashara. Hivyo sehemu ya nchi yetu ikawa inawekwa rehani. Jambo hili halipaswi kukubalika tena.

Saba, mapatano haya yanaifanya serikali ya Tanzania kuwajibika kwa serikali ya Dubai, na hivyo kunajisi haki ya Tanzania kuwa huru dhidi ya kuwajibika kwa Taifa jingine lolote duniani, yaani "state sovereignty." Mfano mzuri wa tatizo hili ni aya ya 4(2) inayosomeka kama ifuatavyo:

1686632422384.png

Nane, kuna jambo baya zaidi. Katiba ya Taifa la Dubai (1996), kwenye ibara ya saba inasema kwamba Dubai ni Taifa lenye dini rasmi, na linaongozwa na "sharia", na kwamba, ajenda yake kuu ni kukuza na kuhami "Uarabu na Uislamu." Nanukuu ibara muhimu:

Article 1--The United Arab Emirates is a Federal, independent and sovereign state, referred to hereafter in this Constitution as the Federation. The Federation is composed of the following Emirates: Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ajman, Umm Al-Quwain, Fujaira, Ras Al-Khaimah.

"Article 7 — Islam is the official state religion, Islamic Sharia the primary source of legislation"

"Article 12 — Foreign policy will be to support Arab and Islamic causes and consolidation of friendship and co-operation with all nations on the basis of the Charter of the United Nations"

Sina imani na serikali inayoongozwa na Katiba ya aina hii, maana "sharia" ni mfumo wa kanuni usiotambua kanuni ya "usawa wa binadamu."

Wawekezaji wenye mtazamo wa aina hii wanapokuja Tanzania wanajaribu kutengeneza "dola ya Kiislamu" ndani ya "dola ya Jamhuri." Mfano, wanawalazimisha wanawake wote wanaowaajiri kuvaa hijab. Mfano mzuri ni NGO ya WIPAHS kule KIbaha, Pwani.

Hivyo, napendekeza kwamba, kushirikiana na Taifa la aina hii ni sawa na kufanya uamuzi wa kumomonyoa “sovereignty” ya Tanzania. Na hivyo, ni kuhatarisha usalama wa nchi. Haya sio mapatano mazuri kiusalama.

Na tisa, ni tatizo la kuandika "Mapatano ambayo ni Mwavuli wa Mikataba ya MIradi" (Inter-Governmental Agreement--IGA) kwa kutumia lugha ya "Mkataba."

Mfano, ibara ya 5(1) inasema kwamba, serikali ya Tanzania inawajibika ("shall") kuipa Dubai "haki ya kipekee ya kuendesha miradi kadhaa." Lugha sahihi ilipaswa kuwa serikali ya Tanzania inaweza ("may") kuipa Dubai "haki ya kipekee ya kuendesha miradi kadhaa."

Kwa mujibu wa ibara ya 53(2) ya "Interpretation of Laws Act No 01 R. 2019," tunasoma:

"53(2) Where in a written law the word “shall” is used in conferring a function, such word shall be interpreted to mean that the function so conferred must be performed."

Kwa hiyo, mapatano haya ni mkataba wa kisheria, yaani ukivunjwa unashitakiwa.

Mapendelezo

Kwa ufupi napenda kusema kuwa haya ni mapatano yanayoruhusu kumegwa kwa “sovereignty” ya Tanzania. Yana harufu ya kitumwa.

Hivyo, mapendekezo yangu ni mafupi sana. Kama tunashindwa kusema ukomo wa uhai wa mapatano, tunaogopa kubainisha "revenue sharing model", na hatuna mfumo wa kuzuia vibali vya umiliki wa ardhi kuwekwa rehani kwenye mabeki ya kimataifa, basi tuachane na mapatano haya.

Kuhusu mfumo wa kugawana mapato, napenda nieleweke vizuri kwa njia ya mfano kama ifuatavyo:

Uamuzi wa kufunga “ndoa ya kibiashara” kati ya makampuni mawili hufanyika kwa ajili ya kuunganisha mitaji ili kuleta tija kwa wanandoa wote. Ndoa hii inaweza kuwa na sura tofauti, na kila sura inayo fomula yake ya kugawana mapato.

Mosi, Kuna ndoa ya makampuni yanayoungana na kuunda kampuni moja mpya baada ya makampuni yote mawili kupoteza uhai wake wa awali (mergers). Hapa kila mwanandoa atapata faida kulingana na kiasi cha hisa alizoweka katika ushirika.

Pili, Kuna ndoa ya makampuni yanayoungana na kuunda kampuni mpya lakini bila makampuni hayo kupoteza uhai wake wa awali (joint venture). Hapa pia mgao wa mapato hutegemea kiasi cha hisa za kila mbia.

Tatu, Kuna ndoa ya makampuni yanayoungana kwa njia ya kampuni moja kuinunua kampuni nyingie (acquisition). Hapa kampuni mnunuzi ndiye mmiliki wa mapato yote, maana ile kampuni iliyonunuliwa hufa kabisa.

Na nne, kama makampuni yanataka kushirikiana lakini bado yanaona mashaka ya kufunga “ndoa za kibiashara” zilizotajwa hapo juu, yanaweza kufunga “ndoa ya miradi,” na kushirikiana katika miradi maalum.

Hapa makampuni husaini “mapatano ya ushirikiano wa kimkakati,” yaani “strategic alliance agreement,” kwa ajili ya kutekeleza miradi maalum.

Katika “mapatano ya ushirikiano wa kimkakati,” lazima kuwepo na kifungu kinachosema majukumu ya kila upande katika kuchangia rasilimali zinazohitajika katika kutekeleza miradi ya pamoja. Kutokana na majukumu haya, lazima kuwepo na kifungu kinachosema haki za kila upande.

Mfano, utakuta tamko kwamba, “mbia wa kwanza atapata asilimia 80 ya mapato kabla ya kutoa matumizi, na mbia wa pilia atachukua asilimia zinazobaki.”

Au, utakuta tamko kwamba, “mbia wa kwanza atapata asilimia 80 ya mapato baada ya kutoa matumizi, na mbia wa pilia atachukua asilimia zinazobaki.”

Kwa ajili ya kufuatilia mapato, matumizi na mgawanyo huu akaunti ya pamoja huundwa kwa ajili ya kupokea na kutunza kila senti inayohusu mradi wa pamoja. Akaunti hii huitwa “escrow account,” kwa Kiingereza.

Katika bandari zote zilizopo Tanzania tunayo ardhi, na tunayo miundombinu yenye thamani ya matrilioni tuliyowekeza tayari. Huu unapaswa kuwa mchango wetu katika maeneo haya.

Hivyo, katika maeneo yote ambako tayari tumefanya uwekezaji, mapatano kati ya Tanzania na Dubai yalipaswa kufuata mkondo huu wa "revenue sharing model."

Lakini, hili halikufanyika. Basi, pengo hili sasa linapaswa kuzibwa kwa kuandaa “Mkataba wa Utekelezaji” ukiwa na jina “Mkataba wa Mgawanyo wa Mapato,” yaani “Revenue Sharing Contract.”

Pasipo andiko hili, Mapatano Mwavuli yaliyosainiwa ni sawa na leseni ya kuzitoa bandari za Tanzania kama zawadi kwa Dubai. Mfumo wa "landlord-tenant" unaotupa fursa ya kukuksanya kodi ya kibiashara na kodi ya ardhi hauna maslahi kwetu. Na katika hili, Bunge linayo kesi ya kujibu.

Nimeambatanisha nakala ya mkataba husika.

1687552443124.png

Picha ya baadhi ya Watanzania waliokwenda Dubai kufanya "due diligence" wakiwa katika picha ya pamoja na Mfalme wa Emirati ya Dubai.
 
Attachments

  • MKATABA KATI YA TANZANIA NA DUBAI KUHUSU UENDESHAJI WA BANDARI ZA TANZANIA.pdf
    2.3 MB · Views: 9
View attachment 2649957

Usuli

Mheshimiwa Rais Samia, Tanzania kama Taifa huru linayo haki ya kutowajibika kwa Taifa jingine lolote duniani, na haki hii ndiyo inaitwa "sovereignty" kwa Kiingereza. Hivyo, katika maneno 700 pekee, najadili Mapatano kati ya Serikali za Tanzania na Dubai kwa kugusia yafuatayo: utangulizi, muundo wake, maudhui yake, mazuri yake, mabaya yake, na mapendekezo.

Nitapendekeza kwamba, kwa kuwa mapatano haya ni hatari kwa usalama wa nchi ya Tanzania, na kwa kuwa yanamomonyoa "sovereignty" ya Taifa letu, basi hayafai. Mapatano haya yanaweza kuleta utumwa mamboleo na kuliweka Taifa tena chini ya himaya ya wageni waliowachuuza mababu zetu kwa miaka 400 kama bidhaa sokoni. Naomba ukataliwe na Bunge hadi hapo utakaporekebisha dosari nitakazozionyeha.

Utangulizi

Oktoba 2022, Profesa Makame Mbarawa, akiwa anaiwakilisha Serikali ya Tanzania, na Ahmed Mahboob Musabih, akiwa anaiwakilisha Serikali ya Falme za Kiarabu (UAE), walisaini Mapatano ya Kiserikali (IGA) kwa ajili ya kuanzisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Dubai.

Katika kutekeleza Mapatano haya, Tanzania itawakilishwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Dubai itawakilishwa na “Dubai Ports World (DPW).” DPW ni kampuni ya kimataifa ya usafirishaji yenye makao yake makuu Dubai, inayomilikwa na serikali ya Dubai.

Tayari barani Afrika, DPW inafanya kazi ya kuendesha bandari nchini Algeria, Angola, Djibouti, Misri, Msumbiji, Nigeria, Rwanda, Senegal, Somaliland na Afrika Kusini. Yaani, bandari hizi zote zinaunda “Dubai Ports World.”

Kwa asili yake, Mapatano kati ya nchi mbili ni lazima yaidhinishwe na mabunge ya nchi husika. Nchini Tanzania, mapayano haya yanatarajiwa kuidhinishwa tarehe 10 Juni 2023.

Kama mapatano haya yataidhinishwa, DWP itarithi kampuni binafsi iitwayo TICTS iliyoendesha eneo la makontena ya Bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya miaka 30 hadi 2022 ambapo Serikali ya Tanzania iliamua kutoendelea na mkataba huo ili kutafuta mwekezaji mwingine wa kimkakati kutoka nje ya nchi.

Bandari ya Dar es Salaam ndiyo lango kuu la kibiashara la Tanzania, ambapo takriban asilimia 95 ya biashara ya kimataifa ya Tanzania inahudumiwa na bandari hii.

Pia, bandari hiyo inayo mageti 12 yanayotumika kupokea mizigo kutoka nje ya nchi. Inahudumia nchi jirani zisizo na bandari kama Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda na Zimbabwe.

Muundo wa Mapatano

Mapatano haya yamegawanyika kwenye sehemu tano. Yaani, Fasili, tafsiri na mipaka ya miradi (ibara 1); majukumu ya jumla (ibara 16); masuala yanayohusu sheria za kifedha (ibara moja); Vifungu vya majumuisho (ibara 13); na Viambatanisho viwili.

Kiambatanisho cha kwanza ni maeneo ya ushirikiano, ambayo ni tisa, maeneo saba yakiwa awamu ya kwanza, na mawili awamu ya pili. Na Kiambatanishi cha pili ni vibali vya marais wa nchi mbili kwa wawakilishi wao waliosani mkataba kwa niaba yao. Mkataba inazo ibara 31 kwa ujumla.

Maudhui ya Mapatano

Kwa mujibu wa ibara ya pili ya mapatano, malengo ya mapatano haya ni:

Serikali ya Dubai itatafuta na kuleta mtaji wa kifedha na mtaji wa rasilimali watu mitaji itakayosababisha kufanyika kwa uendelezaji, uboreshaji, menejimenti na uendeshaji wa bandari zilizo katika maziwa na bahari, maeneo maalum ya kiuchumi, vituo vya utunzaji na usafirishaji wa mizigo, korido za kibiashara, na miundombinu anwai ya banadari.

Pia, serikali ya Dubai inayo dhamira ya kufanya ujenzi wa uwezo wa Watanzania; uhamisho wa maarifa, stadi, na tekinolojia kutoka Dubai kuja Tanzania; uimarishaji wa taasisi za mafunzo; na ukuzaji wa taarifa za intelijensia ya kibiashara.

Mazuri ya Mkataba

Taarifa kwamba, serikali ya Dubai itakuja na mtaji wa kifedha na rasilimali watu utalaosababisha kufanyika kwa uendelezaji, uboreshaji, menejimenti na uendeshaji wa bandari zilizo katika maziwa na bahari, maeneo maalum ya kiuchumi, vituo vya usafirishaji, korido za kibiashara, na miundombinu anwai ya banadari, ni habari njema.

Pia, dhamira ya kufanya ujenzi wa uwezo wa Watanzania; uhamisho wa maarifa, stadi, na tekinolojia kutoka Dubai kuja Tanzania; uimarishaji wa taasisi za mafunzo; na ukuzaji wa taarifa za intelijensia ya kibiashara; ni habari inayovutia.

Mabaya ya Mkataba

Kwanza, mapatano hayasemi serikali ya Dubai italeta mtaji wa fedha kiasi gani; hauelezi aina ya ujuzi utakaohamishiwa Tanzania; hakuna vigezo vya kupima kasi ya ufanisi wa miradi inayokushdiwa kutekelezwa.

Pili, mapatano ayanaifunga mikono na miguu serikali ya Tanzania, kiasi kwamba, serikali ya Dubai inaweza kufanya lolote na vyvovyote, bila serikali ya Tanzania kusema hapana. Mfano mzuri wa tatizo hili ni ibara ya 23(4) inayosomeka hivi:

View attachment 2649978

Tatu, mapatano yamesahau kifungu muhimu kuliko vyote: mgawanyo wa mapato yatakayopatikana kutokana na ushirikiano huu. Ukiachana na misamiati ya jumla, hakuna maelezo yenye kuonyesha nchi ya Tanzania itafaidika nini kwa kutaja takwimu halisi. Kwa kimombo kilichosahaulika hapa ni "revenue sharing model."

Nimeshiriki katika uandishi wa “strategic alliance agreements” nyingi, lakini sijawahi kuona “strategic alliance agreements” mbovu kama hii. Hakuna "strategic alliance agreement" isiyotaja "revenue sharing model." Maana mwisho wa siku kila upande unapaswa kujua haki zake ni zipi, kulingana na kiwango cha rasilimali kilichoingizwa katika mradi wa pamoja. Profesa Makame Mbarawa ametuangusha.

Nne, mapatano haya yanaonekana kuwa ni kama "mkataba wa urafiki wa milele", yaani kama ule mkataba wa Chifu Mangungo wa Musovero na mkoloni aliyeitwa Karl Peters.

Mapatano hayataji ukomo wa uhai wake kabisa! Mwanasheria wetu mkuu naona hakushirikishwa. Siku hizi hakuna mkataba au mapatano yasiokuwa na aya ya urefu wa uhai wake, yaani "contract/agreement term."

Kwa ufupi, bila kutaja "revenue sharing model" na bila kueleza urefu wa uhai wa mapatano, ni mambo ambayo yanaashiria ubabaishaji unaoweza kuzalisha mahusiano ya mfuga mtumwa na mtumwa, kati ya Tanzania na Dubai. Tusipokuwa makini historia ya "Tanzania Koloni Jipya la Dubai" itaandikwa.

Tano, ni kwamba, bandari, viwanja vya ndege, na barabara za zinazounganisha nchi na nchi huwa ni maeneo ya kimkakati katika masuala ya usalama wan chi.

Kuziweka bandari zetu mikono mwa serikali ya nchi nyingine inayosimamia “Dubai Ports World,” na hivyo kuzifanya bandari hizi sehemu ya “Dubai Ports World,” ni sawa na kuimega nchi yetu na kuiweka chini ya Taifa jingine.

Sita, mapatano yanaongelea utoaji wa vibali vya "haki ya kumiliki ardhi" kwa Dubai. Vibali kama hivi vilipotolewa kwa wawekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi vilileta mgogoro wa kumega utaifa wetu. Hawa wawekezaji walivitumia kama dhamana kwenye mabenki ya nje na kupata mkopo wa kibiashara. Hivyo sehemu ya nchi yetu ikawa inawekwa rehani. Jambo hili halipaswi kukubalika tena.

Saba, kuna jambo baya zaidi. Katiba ya Taifa la Dubai (1996), kwenye ibara ya saba inasema kwamba Dubai ni Taifa lenye dini rasmi, na linaongozwa na "sharia". Nanukuu:

"Article 7 — Islam is the official state religion, Islamic Sharia the primary source of legislation"

Sina imani na serikali inayoongozwa na Katiba ya aina hii, maana "sharia" ni mfumo wa kanuni usiotambua kanuni ya "usawa wa binadamu." Ndio maana inaruhusu ndoa za mitala.

Hivyo, napendekeza kwamba, kushirikiana na Taifa la aina hii ni sawa na kufanya uamuzi wa kumomonyoa “sovereignty” ya Tanzania. Na hivyo, ni kuhatarisha usalama wa nchi. Haya sio mapatano mazuri kiusalama.

Na nane, ni tatizo la kuandika "Mapatano ambayi ni Mwavuli wa Mikataba ya MIradi" (Host Government Agreement--HGA) kwa kutumia lugha ya "Mkataba wa Mradi" (Project Agreement). Mfano, ibara ya 5(1) inasema kwamba, serikali ya Tanzania inawajibika ("shall") kuipa Dubai "haki ya kipekee ya kuendesha miradi kadhaa." Lugha sahihi ilipwaswa kuwa serikali ya Tanzania inaweza ("may") kuipa Dubai "haki ya kipekee ya kuendesha miradi kadhaa." Hili ni janga la kisheria.

Mapendelezo

Hivyo, mapendekezo yangu ni mafupi sana. Kama tunashindwa kusema ukomo wa uhai wa mapatano, tunaogopa kubainisha "revenue sharing model", na hatuna mfumo wa kuzuia vibali vya umiliki wa ardhi kuwekwa rehani kwenye mabeki ya kimataifa, basi tuachane na mapatano haya.

Ni mapatano yanayoruhusu kumegwa kwa “sovereignty” ya Tanzania. Yana harufu ya kitumwa.

NImeambatanisha nakala ya mkataba husika.
Yeye anajali nini wakati akimaliza anakwenda nchini kwao na kuwaacha nyie mkihangaishwa na hao waarabu ambao najua wataanza kuwasilimisha kabla ya kuwapeleka utumwani
 
Tumeshauzwa hapa ni kuangalia ustaarabu mwingine.

Baada ya Mungu kumtumia Nyerere kutuletea Uhuru bila hata mlio wa risasi.

Sasa tumerudi utumwani kwa kalamu.
 
wabunge wa CCM hawawezi kukuelewa kwavile wana akili sana kuliko watanzania wate CCM=CHUKUA CHAKO MAPEMA
 
Back
Top Bottom