Parking ya magari jijini Dar es salaam

Iwensanto

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
1,173
1,092
Wakuu kichwa cha habari hapo juu kimezingatiwa
Kumekuwa na shida kubwa katika malipo ya parking katika jiji la Dar es salaam.

Nilifuatwa na watu wa parking juzi tarehe 28 August 2023 katika ofisi yangu iliyopo katikati ya jiji na kulezwa kuwa nadaiwa deni la sh 200,000.

Nikaomba kupata ufafanuzi juu ya deni hilo.

Ndipo niliposhangazwa kuona nimeandikiwa gharama za parking katika sehemu ambazo sijawahi kupaki hata siku moja.

Mbaya zaidi gari liliandikiwa gharama hata siku ambazo halikuwepo mjini.

Hili ni tatizo kubwa nilipowauliza jambo litatuliwa vipi nikaambiwa nikaongee na msimamizi wa wakusanya madeni.

Ingawa walikili kuwa system ya machine inatakiwa imbalance hivyo mwenye kituo husika huweka namba ya gari lolote analolifahamu ili aweze kubalance mahesabu yake.

hili ni tatizo tunaomba wahusika watafute namna bora ya kulipa hizo gharama.

Kibaya zaida hata unapolipa bado system hainoshi kama umelipa wataalamu.

msituingeze katika mifumo amboya bado haijakaa sawa kama mifumo haipo sawa rudishe ule utaratibu wa kukatia risiti badala ya huu ambao mnatuingiza katika matumizi ambayo hayatuhusu.
Mwananchi.
 
Back
Top Bottom