Papaa Msofe kupandishwa kizimbani leo

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Wakuu,

Kama mlifuatilia hii thread - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...m/301102-papaa-musofe-mbaroni-kwa-mauaji.html basi hii leo jamaa anapandishwa kizimbani Kisutu kuhusiana na sakata hili.

Papaa Musofe alikamatwa kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mfanyabiashara mwenzake, Onesphor Kituri, mkazi wa Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa kuwa kabla ya mauaji hayo, Papaa Msofe alikuwa na mgogoro na marehemu wa kugombea nyumba ambayo ilikuwa imewekwa rehani kwa Shilingi milioni 30 ambazo Msofe alimpa marehemu kwa makubaliano kwamba akishindwa kuzilipa atachukue nyumba yake.

Papaa Msofe inadaiwa walikuwa wakimtishia maisha marehemu huyo.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, kutokana na vitisho hivyo, marehemu alifungua kesi mahakamani, lakini siku ya hukumu alikutwa akiwa amekufa mbele ya mlango wa nyumba yake huku kukiwa hakuna mali yeyote iliyochukuliwa.
 
Duuu wakimpa kesi mauaji amekwisha!!!hadi ije isikilizwe miaka 3-4 anasota rumande!pole zake sana!ndio maisha hayo lakini
 
Marijani Abubakar a.k.a Papaa Msofe! Hahaha, mutu ya pesa mingiiii
 
Aliyemtisha marehemu alikuwa Alex Massawe ila Msofe alinunua hiyo nyumba kwa Alex.
 
Duh! Japo kama hela anazo anazo atasota afu arudi kuanza upya. Mbona kama wamem-hold muda mrefu bila kumpeleka mahakamani?
 
hahahhah mkuu kuna mzee mmoja aliwahi kuniambia kuwa kuna umri wa kufanya mambo fulani na mambo fulani....leo ndio nimeamini
 
Kesi itaedeshwa kwa speed isito ya kaaida na atashida kwa ushahidi hafifu utakaotolewa na policcm' wait and see
 
Nasikia Alex Massawe huo ndio mchezo wake anakukopesha hela iwapo utweka rehani nyumba yako ,mnaandikiana mkataba kuwa ikifika tarehe flani utarudisha pesa na riba yake na usiporudisha nyumba yako itakuwa halali yake sasa anachofanya ni kuwa ikifika siku ile ya kurudisha pesa hapatikaniki si kwa simu wala ofisini kwake muda ukipita ndio anaibuka na kudai umevunja mkataba ,kosa ni kwa mkopaji kwani anakuwa hajasoma vizuri mkataba ,kwani hakuna sehemu ambayo inaandikwa je kama siku hiyo haupo kitatokea nini,kwa ulaghai wake huo A.M kajipatia nyumba chungu nzima huko Sinza na maeneo mengine Dar na Arusha,huo ndio ujanja pori wa AM
 
mfianchi,

Hawa jamaa ni matabeli wa kutupwa,hilo jengo lililowapeleka lupango ni la maana kweli kama ghorofa 3 hivi.....Alex Masawe kashakimbia hayupo nchini.
 
Hawa jamaa ni matabeli wa kutupwa,hilo jengo lililowapeleka lupango ni la maana kweli kama ghorofa 3 hivi.....Alex Masawe kashakimbia hayupo nchini.

Wacha wafungwe kutokana na uchafu wao wakapasuliwe masaburi yao, washenzi sana hawa jamaa.
 
mmh hiyo sio kesi ya Papaa Msofe, ni kesi ya Mr. A.M... ila wote ni matapeli wakubwa sana hapa mjini
 
mwache akapakatwe na masela,yeye c kazoea kutapeli watu,na bado mafia alex massawe atafuatia
 
Aliyemtisha marehemu alikuwa Alex Massawe ila Msofe alinunua hiyo nyumba kwa Alex.

Siyo kweli!!!marehemu aliweka bond kwa massawe,baada ya kuchelewa kugomboa mkali massawe akaipiga bubaa baada ya kubadilisha madocs akamuuzia msofe!marehemu kuibuka akakuta mjengo umesukumwa kwa msofe ikabidi afuatilie,msofe akamtolea bomba kuona jamaa anamletea chafya!massawe kwakuwa ni mjanja inasemekana akaamua kuimaliza kesi kibingwa kwa kumuua mshkaji na maiti ikatupwa maeneo ya kwa msofe ili ijulikane msofe ndo muuaji!!!!masawe kamdondoshea jumba bovu msofe hii kesi ila watu watapotea hawa wakifanya masihara kwani mkulu alishawaonya na sasa wamejitela wenyewe!
 
Aliyemtisha marehemu alikuwa Alex Massawe ila Msofe alinunua hiyo nyumba kwa Alex.

Siyo kweli!!!marehemu aliweka bond kwa massawe,baada ya kuchelewa kugomboa mkali massawe akaipiga bubaa baada ya kubadilisha madocs akamuuzia msofe!marehemu kuibuka akakuta mjengo umesukumwa kwa msofe ikabidi afuatilie,msofe akamtolea bomba kuona jamaa anamletea chafya!massawe kwakuwa ni mjanja inasemekana akaamua kuimaliza kesi kibingwa kwa kumuua mshkaji na maiti ikatupwa maeneo ya kwa msofe ili ijulikane msofe ndo muuaji!!!!masawe kamdondoshea jumba bovu msofe hii kesi ila watu hawa watapotea hawa wakifanya masihara kwani mkulu alishawaonya na sasa wamejitela wenyewe!
 
Mnamtetea msofe kwani ni mara yake ya kwanza? Kwani ile kesi ya kina zombe msofe hakuhusika kuua wale jamaa? Ancheni unafiki Msofe ni muuaji na kawaminya wengi kimya kimya hii ya juzi kusanuka ni kwamba arobaini yake imefika.. Msofe hafai hata magereza angenyongwa kabisa.
 
Acha afungwe kwani huyo aliyepoteza maisha alikuwa na familia na watu wanaomtegemea ili waione kesho katika mwanga bora,sasa wanataabika kwa hila za hao matapeli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom