Papa Msofe ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam linamshilikia mfanyabishara maarufu, Marijan Abubakari maarufu kama Papaa Msofe kwa tuhuma za mauaji.

Habari zinasema kuwa Papaa Msofe alikamatwa na Polisi juzi jijini Dar es Salaam na anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Magomeni jijini humo.

Akizungumza na NIPASHE jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha Papaa Msofe kushikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za mauaji.

“Ni kweli tunamshikilia Papaa Msofe katika Kituo cha Polisi cha Magomeni na tunaendelea kumhoji na kufanya upelelezi zaidi kuhusiana na tukio analotuhumiwa nalo,” alisema Kamanda Kenyela.

Akisimulia tukio hilo, Kamanda Kenyela, alisema Papaa Msofe alikamatwa baada ya kutokea mauaji ya Onesphori Kituli, mkazi wa Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam.

Alisema kabla ya kutokea mauaji hayo, Papaa Msofe na marehemu walikuwa wakigombea nyumba ambayo ilikuwa imewekwa rehani kwa Sh. milioni 30.

Habari zaidi kuhusiana na tukio hilo ambazo hata hivyo hazikuthibitishwa na Kamanda Kenyela, zinasema kuwa bado kuna mtu mwingine ambaye anahusishwa na tuhuma hizo za mauaji, lakini mpaka sasa hajakamatwa.

Kamanda Kenyela alifafanua kwamba Papaa Msofe alimpa marehemu fedha hizo kwa makubaliano kwamba ikiwa atashindwa kuzilipa atachukua nyumba yake.

Kabla ya mauji hayo ilidaiwa kwamba, Papaa Msofe na mwenzake walikuwa wakimtishia maisha marehemu huyo.

Kamanda Kenyela alisema kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo, marehemu alifungua kesi mahakamani na kwamba siku ya hukumu alikutwa amekufa mbele ya mlango wa nyumba yake na kwamba hakuna mali yoyote iliyochukuliwa.

Kwa mujibu wa Kamanda Kenyela, mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote baada ya upepelezi kukamilika.

CHANZO: NIPASHE
 
Hata kama kweli kaua with malice aforethougt kwasababu ya mambo yapesa itaishia kuwa
manslaughter au watasema yupo huru kabisa ila kaue wewe hata kama ume ua in provocation itakuwa murder tu hata hu aduce evidence in standard of proof.
 
Duuu kazi kweli kweli,ila kesi yenyewe ni ngumu kidogo!!mtu uanemdai anakutwa amekufa nje ya nyumba yake....pasipo kuibiwa chochote!!na wakati inapoelekea jamaa anapoteza nyumba yake alioweka rehani!!kesi ngumu sana kwa kweli
 
Papa Msofe nasikia ametoka na hata kesi ya kujibu mambo ya pesa bana!

Polisi hawajapewa mshaara kwhyo ni mbinu ya kupata pesa tu hyo papa musofe aliua tangia mwaka jana mwezi wa kumi juzi juzi tu ndio wammekamata kwa sababu polisi wamecheleshewa mshaara wakaona ngoja wamkamate kwa uchunguzi hili wapate hela ya kusavaivu mpaka tarehe 40 wapate salary!
 
Polisi hawajapewa
mshaara kwhyo ni mbinu ya kupata pesa tu hyo papa musofe aliua tangia
mwaka jana mwezi wa kumi juzi juzi tu ndio wammekamata kwa sababu polisi
wamecheleshewa mshaara wakaona ngoja wamkamate kwa uchunguzi hili
wapate hela ya kusavaivu mpaka tarehe 40 wapate salary!
huyu mtu hatari sana,nadhani hata serikali inamwogopa
 
Hatimaye papaa msofe kafikishwa mahakamani, kawa mdogo. Ngoja kwanza asote segerea mpaka kesi ihishe atakuwa amesota vya kutosha!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom