Papa Sylvester alisoma madrasa. Alifuzu somo la hesabati

Pole mkuu allah hakuwepo enzi za adam na eva. Alikuwepo Mwenyezi Mungu
Ikiwa mpaka hapo umeelewa basi ni kheri kubwa
Endelea kufaidi matunda.
Nikusahihishe tu kuwa Adamu na Hawa sio kwamba ni wetu bali ni wa Allah na waislamu wa mwanzo.
 
Wala hakuna debate. Nyie ndiyo mnataka iwe debate. Alisoma Spain na baadhi ya elimu aliyopata ni ile iliyokuwa imepokelewa toka Waislam wa Andalusi. Yeye binafsi hakuwahi kwenda Moroco kusoma. Historia iko wazi na ushahidi upo.
Kwa Hio proffesor wa Historia hajui ila wewe una uhakika kabisa unajua?
 
Acheni kujilisha matumaini hewa. Alisoma Spain to be specific ni Barcelona wwkati huo Barcelona utawala wa Waislam ulisha furushwa. Hilo wala siyo la mjadala
Lete ushahidi wako kukanusha hilo
Unajichanganya sana kwa hili.
 
Guinness world record inatambua Bologna italy kama chuo cha kwanza Cha magharibi na sio duniani, ukumbuke Bologna imekua Chuo miaka ya 1000 wakati huo miaka 200 na kitu kabla hicho cha Morocco kilishakua chuo

Roma ili fall, na Elimu ya Kigiriki ikapotea Ulaya, ila Middle East ili Endelea kuwepo, so wazungu Wakaja kuipata tena Elimu ya Kigiriki na ya Middle East kupitia waisilamu.

Kuna muda unajulikana kama "Age of translation" ambao Academics wengi wa Ulaya walikuja maeneo ya waisilamu kujifunza kiarabu na kutafsiri elimu toka Kiarabu kwenda lugha zao za asili

1.well mkuu sijapinga kuhusu hiyo hoja ya hiko choa, nimeingia several pages na kuona kuna vinavyosema ni Bologna na vyengine uwepo wa hiko chuo...

2.Ukikubali uwepo wa Dola ya Roma basi napo utakubali kuwa Roma ndiyo walioeneza Advance maths ulaya na mashariki ya kati,
-Kwa maana Roma ilitawala mpaka mashariki ya kati.
-Hapo ndiyo utaona hiyo hoja ya wazungu kutojua hesabu karne ya 9 ni uongo.

-Roma ndiyo wakioeneza teknolojia ya Ujenzi (Soma kuhusu msikiti wa Hague Sophia,ujue ulijengwa na nani)

Lakini pia hesabu ni zao la jamii tofauti tofauti na wala siyo dini.....
 
Quran 4:11
Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho kiacha maiti. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi fungu lake ni nusu. Na wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi ya alicho kiacha, ikiwa anaye mtoto. Akiwa hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja. Na akiwa anao ndugu, basi mama yake atapata sudusi. Haya ni baada ya kutolewa alicho usia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, nyinyi hamjui ni nani baina yao aliye karibia zaidi kwenu kwa manufaa. Hiyo ni Sharia iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.


Hayo mahesabu yaliyopo hapo ambayo Mtume Muhammad aliwafundisha waislam karine 6

Wewe jinsi ulivyo kilaza ukipewa Mbuzi 70 uwagawanye Kwa hayo maelezo hapo hauwezi

Hesabu za Alijebra ulizosoma shule msingi wake ndio upo hapo katika hiyo aya

Aliyeandika na kufundisha hizo hesabu alikuwa anaitwa ALLY JABIRi wazungu wakaziita hesabu za Aljebra Ili kuondoa chembechembe za uislam katika somo la hesabu Ili waendelee kuwadanganya vilaza kama wewe
Mkuu,

Mimi ninataka kujifunza jambo haswa kulingana na chimbuko halisi la dini ya Islam. Hii itatupa picha halisi bila kuwa bias ni nani walikuwa waanzilishi wa mwanzo kabisa wa hesabu katika karne nyingi sana zilizopita.

Sina shaka na Misri ya zamani maana mambo makubwa ya kihistoria yamefanyika huko, hesabu pamoja na maandishi ya kale pia.

1. Je, ni kweli Islam ilikuja baada ya Mtume Muhammad (saw) kuzaliwa?, au ni dini iliyokuwepo tangu awali hata kabla ya kuzaliwa kwa mtume?

2. Quran kama kitabu cha muongozo kwa Muslims, kiliteremshwa kipindi cha Muhammad (saw), au ni kitabu kilicho kuwepo karne nyingi kabla ya kuzaliwa kwa mtume?.

3. Mwisho kabisa, Islam kama dini ilianza karne ya ngapi, na hizi hesabu zinazo zungumziwa zilikuwepo Misri ya zamani na Mashariki ya mbali zilianza karne ya ngapi?.

Natanguliz shukran.
 
Mimi tena nilete ushahidi? Wewe uliye leta madai kuwa pope kasoma Moroco ndiyo uweke hapa ushahidi usio na shaka. Acha kujitoa ufahamu
Mimi nimeshaleta ushahidi wangu kupitia historia inayosimuliwa na watu ambao wameshafika huko na kupitia watafiti wengine wa historia.
Sasa ni zamu yako kuthibitisha mimi ni muongo kupitia ushahidi usio na shaka ulio nao wewe kukanusha kuwa hakusoma huko.
Mara nyingi kwenye mijadala huwa uanaonekana una mikwara sana lakini kwenye mada kama hizi unapata mshtuko mpaka mtu mzima unaadhirika.
 
Ni kweli kabisa.
Muhimu hata hizo habari za Pyramid na maajabu yake zilianza kuelezwa na waislamu ndipo akina nyie mkaelewa.
Na kumbuka kuwa uislamu haukuanza na Muhammad saw.Twataraji hata hao wamisri wa kale walikuwa waislamu.
Mtu wa mwanzo kuzichambua kumbukumbu hizo za kale ni Ibn Yussuf.
Ukiacha hilo.Hesabu za wamisri wa Kale zimefanyiwa ukarabati na waislamu na tukapata hizi zinazotumika leo dunia nzima na ndizo alizosoma papa Sylvester na kuwapelekea wakristo wa Ulaya.
Mkuu,mbona unalisha watu matango poring hapa....
-Hivi unajua Dola ya Misri ilianza mwaka gani na kuisha mwaka gani...?
-Hivi unajua Uislam uliingia Afrika kupitia Misri mwaka gani...?
-Hivi unajua hata Dola ya Kiislam ilikuwa mwaka gani?
-Je,unajua hata Kazi ya hizo Pyramid huko Misri ilikuwa ni nini?
-Leta ushahidi kama kuna ya Afrika ilikuwa na Uislam au Waarabu kabla ya Karne ya 1.

Weka sources hapo.
Hebu google hivyo, vitu kabla ya kunena...
 
Profesa gani? Wek hapa ushahidi usio na shaka kuwa pope kasona Madrasa. 😂😂
Bro nimekuandikia hapo juu jina comment iliopita na hapa unauliza tena anaitwa nani? Kwa jina anaitwa Attilio Gaudio toka Paris proffesor anayedeal na historia ya sahara including Morroco.

Sio yeye tu kuna ushahidi wa kutosha kama vile Abacus ya huyo Pope aliipata Chuoni Morocco, ushahidi huu upo
Truitt, E. R. (2015). Medieval robots : mechanism, magic, nature, and art. Philadelphia: University of Pennsylvania Press. p. 77.
 
Mkuu,

Mimi ninataka kujifunza jambo haswa kulingana na chimbuko halisi la dini ya Islam. Hii itatupa picha halisi bila kuwa bias ni nani walikuwa waanzilishi wa mwanzo kabisa wa hesabu katika karne nyingi sana zilizopita.

Sina shaka na Misri ya zamani maana mambo makubwa ya kihistoria yamefanyika huko, hesabu pamoja na maandishi ya kale pia.

1. Je, ni kweli Islam ilikuja baada ya Mtume Muhammad (saw) kuzaliwa?, au ni dini iliyokuwepo tangu awali hata kabla ya kuzaliwa kwa mtume?

2. Quran kama kitabu cha muongozo kwa Muslims, kiliteremshwa kipindi cha Muhammad (saw), au ni kitabu kilicho kuwepo karne nyingi kabla ya kuzaliwa kwa mtume?.

3. Mwisho kabisa, Islam kama dini ilianza karne ya ngapi, na hizi hesabu zinazo zungumziwa zilikuwepo Misri ya zamani na Mashariki ya mbali zilianza karne ya ngapi?.

Natanguliz shukran.
Uislamu ni dini ya awali kabla hata dunia haijaumbwa.
Mitume waliotangulia kabla kuja Yesu na Muhammad wote walikuwa waislamu
Mitume ni wengi sana lakini waliotajwa kwenye Qur'an ni 25 tu.Mitume waliopita duniani tunaamini walikuwepo Afrika kusini ya jangwa la sahara na kwengineko
Kwa vile elimu yote ni ufalme wa Allah hivyo humfunulia amtakae na kwa kiwango akipendacho.Hesabu walizijua wamisri wa kale na kwengineko
Kilichowazi zaidi ni kuwa baada ya kuteremsha Qur'an kwa Muhammad rehema na amani zimshukie kiwango cha elimu ikiwemo elimu ya hesabu kilikuja kwa kasi ya ajabu na waislamu walipewa kipaji na njia za kueneza elimu zote ikiwemo Kemia.
Wazungu wote walijifunza elimu muhimu kupitia waislamu na watafiti wengi wamekubali hilo na halifichiki.
Papa Syvester alijifunza kitu muhimu kutoka kwa waislamu lakini ni kidogo sana kuliko elimu iliyorithishwa Ulaya
Wakati Marekani inafikiwa na Columbus tena kwa kufuata ramani zilizochorwa na waislamu wakati huo sayari tano kati ya idadi tuliyonayo sasa zilikwishavumbuiiwa na waislamu;
 
Chuo kikuu kikongwe zaidi duniani ambacho kinaendelea kutoa elimu ni kile kilichopo barani Afrika, nchini Morocco na ambacho kilianza msikitini(masjid) na kuendeshwa kwa mfumo wa madrasa.

Chuo kikuu hicho kilijengwa na bi Fatma kikiambatana na msikiti wakati wa ukhalifa wa Abbasiya ambao ulitawala mashariki ya kati, Ulaya na Afrika. Ukhalifa huo na watangulizi wao walitilia umuhimu mkubwa masuala ya elimu na hivyo kurithisha fikra hizo kwa kila watu wa eneo fulani.

Miongoni mwa wanafunzi wa chuo hicho ni papa Sylevester (2).Somo lililomvutia zaidi ni hesabu wakati huo Ulaya ikiwa haijui hata kuhesabu machungwa.

Mfumo wa kuhesabu hasa kwa kutumia kifaa cha Abacus alichojifunzo kutoka walimu wa chuo cha Alqarawiyen ulimfanya aonekane kama ni mchawi na hiyo ikawa ndiyo sababu ya Ulaya nzima kujifunzo na kuanza kuhesabu kutoka kanisani kwake.

Mahesabu mengine magumu na elimu ya astronomy alichukua kutoka dola ya kiislamu ya Andalasia.

Sawa, hata teleban na alqaida wamesoma hapo
 
Mkuu,mbona unalisha watu matango poring hapa....
-Hivi unajua Dola ya Misri ilianza mwaka gani na kuisha mwaka gani...?
-Hivi unajua Uislam uliingia Afrika kupitia Misri mwaka gani...?
-Hivi unajua hata Dola ya Kiislam ilikuwa mwaka gani?
-Je,unajua hata Kazi ya hizo Pyramid huko Misri ilikuwa ni nini?
-Leta ushahidi kama kuna ya Afrika ilikuwa na Uislam au Waarabu kabla ya Karne ya 1.

Weka sources hapo.
Hebu google hivyo, vitu kabla ya kunena...
Dola ya Misri unayouliza sijui ni ipi kwani kama ni watawala wa Misri wapo wengi na wote tunawaita dola
Kwa mfano dola ya Fatima ilianza 909 mpaka 921 na zilikuwepo nyingi kabla yake tangu enzi za mafarao.
Ukisema Uislamu uliingia Afrika kupitia Misri si kweli.Kuna tafiti zinaonesha Uislamu uliotangazwa na Mtume saw uliingia kusini ya Afrika kupitia maeneo tofauti na yawezekana kabla ya Misri.Mfano mmoja wapo ni waislamu walihamia Ethiopia hata Mtume saw hajahama Makka kwenda Madina.
Unauliza dola ya kiislamu ilikuwa mwaka gani?.Ni dola gani unayoulizia.
Dola za kiislamu zilizunguka maeneo karibu yote ya mashariki ya kati Ulaya mpaka India ,China na Urusi.
Ushahidi kuwa Afrika ilikuwa na uislamu kabla ya karne ya 1 ni uchambuzi wa aya za Qur'an kuwa kulikuwa na mja mwema aitwaye Luqman na huyu inaaminika alikuwa maeneo ya milima ya Nuba.
 
Mimi nimeshaleta ushahidi wangu kupitia historia inayosimuliwa na watu ambao wameshafika huko na kupitia watafiti wengine wa historia.
Sasa ni zamu yako kuthibitisha mimi ni muongo kupitia ushahidi usio na shaka ulio nao wewe kukanusha kuwa hakusoma huko.
Mara nyingi kwenye mijadala huwa uanaonekana una mikwara sana lakini kwenye mada kama hizi unapata mshtuko mpaka mtu mzima unaadhirika.
Hakuna ushahidi umeleta zaidi ya porojo
 
Hakuna ushahidi umeleta zaidi ya porojo
za kwako ndio porojo mbaya zaidi kwa sababu unapinga bila kuleta ushahidi.
Leta ushahidi kupinga watafiti wa historia kuwa Papa Sylvester hakusoma chuo kikuu cha Fez ambacho kimeendelea kufundishwa kwa mfumo ule ule wa madrasa.
 
za kwako ndio porojo mbaya zaidi kwa sababu unapinga bila kuleta ushahidi.
Natudua tena kanisa linakanusha unachosena na hakuna Pope yoyote aliyepata kwenda Masomoni Moroco.
Mnang'ang'ania pope kasoma Moroco ndiyo itasaidia nini kwa mfano?
 
Hesabu mzee wangu mpaka za chuo kikuu ni uvumbuzi wa waislamu.
Zimeendelezwa na kubadilika kulingana na wakati lakini muhimu nyingi zimebaki kama zilivyokuwa.
Sio kila Muarabu ni Muislam.
 
Back
Top Bottom