Papa Msoffe na wenzake wafutiwa mashtaka na DPP

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
1624015226923.png
Marijani Abdubakari Msoffe aka Papa Msoffe ameachiliwa huru baada ya MKurugenzi wa Mashitaka (DPP) kusema hana mpango wa kuendelea na kesi dhidi yake. Walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kujipatia fedha kiasi cha Sh943 milioni kwa njia ya udanganyifu

Mbali na Msofe, washtakiwa wengine walikuwa wakili wa kujitegemea, Mwesigwa Mhingo, Wenceslau Mtui, Josephine Haule na Fadhil Mganga

Miongoni mwa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili ni kuratibu genge la uhalifu, utakatishaji fedha na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu

Zaidi, soma:
1). Papaa Msofe naye yamkuta. Afikishwa Mahakamani akituhumiwa na makosa matano likiwemo ya Utakatishaji fedha

2). Papaa Msoffe apata dhamana baada ya kubadilishiwa mashtaka

3). Papaa Msofe akabiliwa na kesi ya mauaji

4). Papa Msofe ni mfanyabiashara au tapeli Maarufu?
 
Kinachofanyika ni vema kuachia watu waliosingiziwa na haki haikufuatwa (lakini tuangalie tusije kuwaachia hata wale wenye makosa)

Cha maana tufuate sheria watu washikwe washitakiwe kwa mujibu wa sheria na serikali ihakikishe kesi za kushinda inashinda na sio kufanya chanzo cha kupata mlungula.
 
Kinachofanyika ni vema kuachia watu waliosingiziwa na haki haikufuatwa (lakini tuangalie tusije kuwaachia hata wale wenye makosa)

Cha maana tufuate sheria watu washikwe washitakiwe kwa mujibu wa sheria na serikali ihakikishe keshi za kushinda inashinda na sio kufanya chanzo cha kupata mlungula....
Dikteta aligeuza magereza kuwa source of income
 
Kwa kweli tulikuwa na utawala wa hovyo sn dikteta aliamini kila aliyefanikiwa ni wizi.
Mh... Huyu ''Papaa'' siyo mtu mzuri. Labda iwe walimkamata kwa kukurupuka lakini rekodi yake uraiani siyo nzuri hata kidogo. Kuachia watu waliokamatwa kwa kukomolewa au bila ushahidi ni jambo zuri sana lakini wawe makini wasiachie na wahalifu wazoefu au wenye mamlaka wasitumie hii nafasi kuachia wahalifu kwa kupewa mshiko!
 
Acha tuanze upya mkuu maana watu walionewa sn na utawala wa shetani
 
Back
Top Bottom