Papa Francis, Lissu, machampioni halisi wa haki, usawa na uhuru duniani

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,901
Tufike mahali tuvunje ukimya:

1. Kuzitambua jitihada za kupigiwa mfano za watu wengine ni jambo la kistaarabu.

2. Vita vya kupigania haki, usawa, uhuru, demokrasia na maendeleo ni vita vya kudumu.

3. Nani asiyeyapenda au kuyahitaji matano hayo?

4. Manne ya mwanzo ni ya msingi zaidi duniani, wakati maendeleo ni ya mtu na taifa moja moja.

5. Matano hayo ndiyo agenda kuu katika chaguzi zote za waliostaarabika duniani.

6. Nchi isiyo amini katika matano hayo haina mchango wowote katika dunia hii.

7. Kiongozi yeyote asiyeamini katika matano hayo hatufai!

8. Chama kisichokuwa na imani yoyote kwenye matano hayo ni cha hovyo.

9. Tumekuwa na vyama vya hovyo visivyokuwa na imani yoyote inayojulikana kuyahusu.

IMG_20231222_071641.jpg

IMG_20231222_042155.jpg

10. Kiongozi, chama au taifa lisilokuwa na imani zozote zinazojulikana litakuwa na msimamo gani kwenye nini?

Screenshot_20231222-034830.jpg

11. Imani huzaa misimamo isiyoteteleka:

(a) "Heko Papa Francis, Tundu Antipas Lissu na wengine kwa kuiweka misimamo yenu wazi kuhusu Palestina, Gaza, Israel na hata haki za LGBTQ."

(b) Haipo shaka hata msimamo wa wawili hawa kuhusu Ukraine hauwezi kuwa rojo rojo au kuwa kama wa wasiojitambua

12. Hapo #11; kwa hakika ninyi ni viongozi na hazina kwa dunia kama wale wenye kufuzu zawadi za Nobeli.

Nyetere ni mfano mwingine wa kuigwa:

Palestine, Julius Nyerere and international solidarity – Middle East Monitor
 
View attachment 2849401

10. Kiongozi, chama au taifa lisilokuwa na imani zozote zinazojulikana litakuwa na msimamo gani kwenye nini?

View attachment 2849400

11. Imani huzaa misimamo isiyoteteleka:

(a) "Heko Papa Francis, Tundu Antipas Lissu na wengine kwa kuiweka misimamo yenu wazi kuhusu Palestina, Gaza, Israel na hata haki za LGBTQ."

(b) Haipo shaka hata msimamo wa wawili hawa kuhusu Ukraine hauwezi kuwa rojo rojo au kuwa kama wa wasiojitambua

12. Hapo #11; kwa hakika ninyi ni viongozi na hazina kwa dunia kama wale wenye kufuzu zawadi za Nobeli.
Ushoga ni laana, Ushoga ni Dhambi Mbayaa saaana kuliko pengine hata ya kuuwa, Ushoga ni fedhuli nafedheha kubwa kwa Taifa na Kanisa la Mungu, ##%%KataaaushogakwaAfyayaDunianaHeshimakwaMungu##%%
 
Ushoga ni laana, Ushoga ni Dhambi Mbayaa saaana kuliko pengine hata ya kuuwa, Ushoga ni fedhuli nafedheha kubwa kwa Taifa na Kanisa la Mungu, ##%%KataaaushogakwaAfyayaDunianaHeshimakwaMungu##%%
Hayo ni mawazo yako ewe mwana wa Buguruni Malapa.

Usitujaze uchafu vichwani asubuhi asubuhi kabla hatujapata STAFTAHI. Haswa uchafu unaotoka Buguruni Malapa.

Kuna uchafu na uchafu wa Buguruni Malapa. Ulichokiandika wewe ni Uchafu wa Buguruni Malapa.

Umejamba kama BATA PORI. Bado kidogo utadakwa upelekwe Dodoma kwenye ile hospitali pendwa ya VICHWA KUMCHUZI.

cc cocastic and fantastic
 
Naanza na Lissu ni mwanasiasa, siasa za kitaifa na kimataifa ni zake. Ana ndoto za kuwa rais wa nchi kubwa duniani, ni lazima ajifarague misimamo yake ijulikane kwa mataifa mengine duniani wamtambue ni mwenzao anarandana na misimamo yao kuhusu mambo mbalimbali ya kuungana mikono. Lissu anataka kuungwa mkono na nchi nyingi duniani hususani madola yenye nguvu na pia anahitaji kura za nyingi za kila mtu awaye yote, anatengeneza mtaji wa kura/siasa. Nije kwa papa, papa ni kiongozi wa dini na pia ni kiongozi wa nchi/dola ya vatican. Papa ni mwanasiasa anachofanya ni kuchanganya dini na siasa. Watu wamechanganyikiwa wanashindwa wachukue msimamo upi hasa ni wa papa kuhusu wapenzi wa jinsia moja. Ni siasa anafanya akiwa ndani ya dini. Ni kiongozi wa kanisa katoliki duniani, msimamo wake ndiyo msimamo wa katoliki yote duniani na ujumbe wake hufika kwa wakuu wa nchi zote duniani zenye ubalozi wa vatican mpaka huko umoja wa mataifa.
 
1. Nitofautiane na sababu ulizotoa.

2. Ninadhani ni suala la kuwa principled. Unaamini nini?

3. Angalia hii Nyerere 1977:

IMG_20231222_071641.jpg

IMG_20231222_042155.jpg

4. Ni kuwa unaamini nini, itatengrneza msimamo wako.

5. Hawataipenda kina Allen Kilewella, imhotep na wale wengine hii:

"Huamini kwenye uhuru, haki, demokrasia au usawa," - hutufai!
 
Tanzania iliyokuwa kinara kimataifa miaka ya 1977:

View attachment 2849442

Ikijulikana inasimamia nini:

View attachment 2849443

Leo imesheheni kina Mpaji Mungu

Vijana wa hovyo wasioweza kuwa na mchango wowote popote.

Hawana msimamo Wapo wapo tu na ndiyo eti hao ndiyo wenye akili kubwa.
Ww Hamas inakusaidia nini kwenye maisha yako? Acha kujipa umuhimu kwenye vitu visivyo na tija kwako! U-much know kaufanyie kwenye mambo ya msingi vinavyokujenga ww binafsi na uchumi wako
 
Ww Hamas inakusaidia nini kwenye maisha yako? Acha kujipa umuhimu kwenye vitu visivyo na tija kwako! U-much know kaufanyie kwenye mambo ya msingi vinavyokujenga ww binafsi na uchumi wako

1. Bila shaka hata huyu unamshangaa:

IMG_1567.jpg

2. Huyu naye unamshangaa:

IMG_20231222_042155.jpg

3. Kwamba hujishangai wewe, uko sahihi hata nyani ni hivyo hivyo:

F6kGqZLXMAATAgq.jpeg

4. Bure kabisa!
 
1. Bila shaka hata huyu unamshangaa:

View attachment 2849480

2. Huyu naye unamshangaa:

View attachment 2849481

3. Kwamba hujishangai wewe, uko sahihi hata nyani ni hivyo hivyo:

View attachment 2849485

4. Bure kabisa!
Ukija kuambiwa huna akili unahis unaonewa!

Umeshindwa kujibu swali unaniletea quotation za watu wengine ambazo na zenyewe hazina impact yeyote ila kwa sababu ni mitazamo yao tunaheshimu!

Nijibu wewe binafsi umenufaika na nini mpaka unahisi ambao hawana muda na migogoro ya magaidi wa Hamas na Israel hawana tija kwa taifa?
 
Nimekuja kugundua kudai haki ni jambo gumu sana miongoni mwetu, kumbe wengi wetu tunajiona machampioni wa kudai haki kwa sababu hatujawahi kuguswa vyumbani mwetu, ndio maana tumedumaa kudai haki hizi tulizozizoea kuwadai CCM miaka yote, maji, umeme, fair election ....

Bado hatujawa na uwezo kamili wa kuzitambua haki na kuzidai, hapa nazungumzia haki zile hata ambazo hazituhusu kwa asilimia 100, mfano kwa wale wanaonyimwa haki kuwa sio raia wa Tanzania yetu, au makundi yasiyotuhusu kibaiolojia.

Bahati mbaya zaidi hata pale ambapo tunakuwa na uwezo wa kuzitambua na kuzidai, bado tena tunakutana na kigingi kingine kwenye mind zetu, kumtazama yule anayewanyima haki wengine, kisha kujiuliza vichwani mwetu, hatuna interest nae?

Ikitokea tukawa na interest nae, kwa vyovyote iwe kiimani au kiitikadi, hapo tena tunageuka mabubu, hatuongei tunaishia kuhamisha magoli, kwa ujumla kumbe sisi bado ni wachanga sana kwenye hili suala la kudai haki.

Haki nyingi tulizozoea kuzidai kumbe tumekaririshwa na wanasiasa hizo ndizo tunaziimba miaka yote, kwasababu tumezoea kuwasikiliza kwanza wao kisha tuwafuate nyuma, hatujawahi kutoka nje ya box, tumegeuzwa watumwa wa wanasiasa tusiojitambua!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Nimekuja kugundua kudai haki ni jambo gumu sana miongoni mwetu, kumbe wengi wetu tunajiona machampioni wa kudai haki kwa sababu hatujawahi kuguswa vyumbani mwetu, ndio maana tumedumaa kudai haki hizi tulizozizoea kuwadai CCM miaka yote, maji, umeme, fair election ....

Bado hatujawa na uwezo kamili wa kuzitambua haki na kuzidai, hapa nazungumzia haki zile hata ambazo hazituhusu kwa asilimia 100, mfano kwa wale wanaonyimwa haki kuwa sio raia wa Tanzania yetu, au makundi yasiyotuhusu kibaiolojia.

Bahati mbaya zaidi hata pale ambapo tunakuwa na uwezo wa kuzitambua na kuzidai, bado tena tunakutana na kigingi kingine kwenye mind zetu, kumtazama yule anayewanyima haki wengine, kisha kujiuliza vichwani mwetu, hatuna interest nae?

Ikitokea tukawa na interest nae, kwa vyovyote iwe kiimani au kiitikadi, hapo tena tunageuka mabubu, hatuongei tunaishia kuhamisha magoli, kwa ujumla kumbe sisi bado ni wachanga sana kwenye hili suala la kudai haki.

Haki nyingi tulizozoea kuzidai kumbe tumekaririshwa na wanasiasa hizo ndizo tunaziimba miaka yote, kwasababu tumezoea kuwasikiliza kwanza wao kisha tuwafuate nyuma, hatujawahi kutoka nje ya box!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

Umeandika kirefu, nami nitafanya hivyo kwa ufafanuzi:

1. Ni muhimu kutulia, kutuliza mawazo kwanza kutambua kama taifa tumepotea njia (akiita Kolimba dira na mwelekeo), vyama vya siasa hadi mtu mmoja mmoja.

2. Taifa la watu jeuri (akiwaongelea Nyerere) wenye kuhoji aina ya kina Shivji, Lwaitama, Baregu, Chachage, Mpina, Lissu hawapo tena au ndiyo watakapokwisha ondoka, kondoo waliotamalaki sasa watashika hatamu kama ilivyo sasa wakijiona wao ndiyo wao.

3. Kabla ya kuhoji na hata mtu kuzipigania haki zake, imani inakuja kwanza.

4. Mtu akiamini hiki ni haki yàngu atahoji akinyimwa; akikomaliwa, atakomaa.

5. Imani kama hii, jiulize tukwame wapi kwenye ukombozi:

IMG_20231222_042155.jpg

6. Leo hii waliokuwa wanabeza makelele dhidi ya kuuliwa au kupotezwa kin Ben, Lijenje, Azory au jaribio la LIssu, leo wanapiga kelele watanzania wawili kuuliwa vitani si kwa si sahihi wowote kuuliwa popote wanapokuwa Hawana hatia, bali kwa kuwa ni wakristo wanaodhani Gaza kuna vita dhidi ya wakristo!

7. Leo hii kina FaizaFoxy wana taabu Gaza si kwa sababu ya maonezi kwa wapalestina (ambayo ni kweli), bali kwa sababu wanadhani wanaonelewa ni waislam.

8. Wakristo uchwara wanadhani kumpinga mwisraeli ni kupinga ukristo na kuwa wanaofanya hivyo ni lazima tu wawe mwislamu; wamezidiwa mahaba mshindo!

9. Hapo #8 wanasahau kuwa Mandela, Nyerere, Lissu na wengi hawakubaliani na waisrael Gaza lakini si waislam!

10. Katokea Papa na suala LGBTQ, watu wanashindwa kuona hili ni pilipili usizozila, lisilokuhusu la wale wewe na engine zao kokote liliko sirini huko taabu na wengine tusiohusuka? Uhuru kumbe maana yake nini?

11. Tatizo kubwa ni uelewa na ufahamu kwamba "falsafa" ya nini au nani wanasimamia nini.

12. Bila kujua "falsafa" za vyama, vyama haviwezi kuwa na imani wala misimamo; na hivyo wafuasi; wala nchi ambayo falsafa ya chama tawala ndiyo msingi.

13. Kwenye urojo tuliomo kutowatambua waliobakia wamesimama, tukawa tayari kujifunza kwao na hata kuwa ujasiri wa kuwapa maua yao wanapostahili; ili kama vipi tugute na waliolala waamke, hakutakuwa na maana yoyote kuwapo duniani!

14. #13 hapo ndiyo ulio msingi mkuu wa hoja.

Ni hayo tu ndugu mjumbe.

Imani bila matendo ni bure!
 
Back
Top Bottom