Papa Francis hapaswi kukosolewa dhidi ya uamuzi wake juu ya LGBTQ

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
1,118
1,915
Ufafanuzi kuhusiana na uamuzi wa Papa Fransis kuwakaribisha wapenzi wa jinsia moja katika kanisa Katoliki.

Watu wengi duniani hasa dini ya Kiislamu, Wahindu na wengineo wamekuwa wakituhumu Imani ya Kikristo pamoja na kiongozi wetu Papa Fransis kana kwamba dini zao zinawaumini Watakatifu pekee jambo ambalo linaweza kuleta picha ya aibu na fedheha katika imani yetu kwa baadhi ya waumini wengine.

Wapo walioenda mbali na kusema Papa Fransis na Imani ya Kikristo inajihusisha na Ushetani.

Kwanza kabisa Papa ameweka mbele swala la maslahi katika kanisa hili, lengo la yeye kuchukua uamuzi huu anataka kanisa liwe na idadi kubwa ya waumini pasipokujali tabia na mienendo ya waumini wake akilenga kuwa sadaka itaongezeka mara dufu na hasa ukizingatia Italy ina mashoga wengi sana na ni matajiri wakubwa ili kupata pesa yao ni kuwaruhusu huku akiamini atakayewahukumu ni Mungu pekee yeye hataki kujihusisha na swala la hukumu hilo ndilo lengo lake.

Kawaida binadamu anapokuwa akihitaji wafuasi wengi hatabagua wezi, wavivu, washirikina na wengineo, dhamira yake italenga kuwa na idadi kubwa ya wafuasi.

Kwahiyo Papa Fransis haenezi ushetani kama watu wanavyomtuhumu na wala Wakristo tusionee aibu imani yetu.

Papa hataki kujihusisha kwenye hukumu ya wakosefu anataka Mungu awahukumu yeye mwenyewe, dhamira yake ni kuhakikisha kanisa linapata wafuasi wengi pasipokujali mienendo na tabia za waumini wake.

Swala la hukumu ni jambo gumu sana duniani ndio maana watu wanamwachia Mungu.

Nadhani amefikiri mara kadhaa kuhukumu waumini wa Kanisa Katoliki akashindwa pengine ameona kuwa akianza kutoa hukumu itabidi achanganye wote wakiwemo wezi, walevi, wavivu, washirikina, mafisadi, makahaba, wanyang'anyi, walawiti na wengineo.

Katika hotuba ya Mwalimu Nyerere kuhusiana na ubaguzi alitoa mfano akasema kuwa nchi ya Tanzania imejengwa na makabila tofauti haikujengwa na kabila moja, madhara ya ubaguzi katika nchi ya Tanzania ni kuwa tukianza kuwaondoa Wazanzibari tukamaliza wote, tutajikuta Wazaramo wamebaki tutawaondoa tena wote, tukimaliza Wazaramo tutakuta kuna Wachaga tutaondoa wote tukimaliza tutagundua kuna Wahaya halikadhalika.

Kwahiyo Papa ameona kuwa Kanisa Katoliki limejengwa na waumini wema na wabaya halikujengwa na Watakatifu pekee akianza kuondoa walawiti akamaliza atajikuta wezi wapo ataondoa atamaliza, atajikuta washirikina wapo halikadhalika kwahiyo hatabakiwa na waumini Watakatifu pekee.

Ndugu zangu tuzungumze kwa uwazi kuhusiana na uamuzi wa Papa Francis kuwapa mashoga uhuru.

Wakosoaji wakubwa wa uamuzi huu ni madhehebu mengine yasiyo ya Katholiki huku wakidai kuwa dini ya Katholiki inaruhusu ushoga.

Kabla ya kumtuhumu Papa ni kuwa idadi ya mashoga duniani imeongezeka sana kiasi kwamba inatishia idadi ya wale wasio mashoga.

Takwimu alizopokea Papa zimemfikirisha mara kadhaa na kuona kuwa endapo akiwatenga mashoga basi atabaki na idadi ndogo sana ya waumini wa Katholiki, ili kuzuia anguko hilo akaona awaruhusu mashoga kuwa waumini wa kanisa la Katholiki.

Wenzangu wa madhehebu mengine wakiwemo Waislamu, Wahindu na wengineo, mnapomnyooshea kidole Papa mnamaanisha kuwa hakuna muumini wetu hata mmoja duniani ambaye ni shoga.

Swali la kujiuliza, je katika dhehebu lako hakuna muumini wenu hata mmoja duniani ambaye ni shoga?

Turejelee msemo wa kuwa kabla hujatoa boliti katika jicho la mwenzako basi hakikisha katika jicho lako umekwishatoa!

Ikiwa kuna faida inapatikana kutoka kwa mashoga nadhani mtu mwenye akili atachuma lakini tabia na mienendo yao atawachia wao
 
Kuna siku papa atawapulizia filimbi wakatoliki
Kwamba sasa ni ruksa maana mambo uanza kidogo kidogo.
Idadi ya mashoga imeongezeka sana kiasi kwamba anaumiza sana akili afanyaje, manake akitenga atabakiwa na waumini wachache sana
 
Wewe Huwa u afikilia kweli?
Yaani kipi kinafuatwa Sheria za mungu au idadi ya waumini?
Au wewe mwenzetu umeshahama group na hapa unawatetea wanzako indirectly???
Jibu hoja sio uniingize mm kwenye mada Huo ni ubakaji wa mada
 
Kuna siku papa atawapulizia filimbi wakatoliki
Kwamba sasa ni ruksa maana mambo uanza kidogo kidogo.
Ukatoliki siyo Mali ya PAPA FRANSIS, UKATOLIKI ulikuwepo tangu mwaka 33 AD.
Hivyo, kama akikosea katika maamuzi marekebisho yatafanywa na watakaofuatia baada yake.
Kwakuwa UKATOLIKI siyo Mali ya PAPA FRANSIS, ni Upumbavu kuikimbia Mali yako Kwasababu ya majungu ya WATU.
 
Yeye inabidi afate misingi ya dini sio nyomi then wenye imani watabaki na kanisa. Kanisa linatumika kama tawi la kueneza ajenda za kishetani na mpaka sasa shetani ameshalikamata barabara

Taasisi gani ya kidini ulimwenguni sio agent wa shetani?
 
Back
Top Bottom