Kwanini Papa Francis anawaandalia watoto na wajukuu SODOMA? Kwa nini hakuonyesha huu msimamo wake ujanani? Bado anabaki kuwa mtakatifu?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Papa kwa sasa ni mzee sana, anapaswa kuepuka kuweka misingi ya kesho ya Dunia hasa pale anapotakiwa kutoa msimamo wake kuhusu mambo yenye utata.

Naamini wapo watu wanatumia vibaya uzee wake. Wapo watu ndani ya Vatcan wana ndoa wanatafuta msamaha wa Mungu kwa kuweka misingi ya kubarikiwa kwa kuwekewa mikono.

Papa alipaswa kutoa msimamo wake kwa kuzingatia vitabu vitakatifu na kuzingatia ukweli kwamba hakuna binadamu anayefuta dhambi. Mtu akiua akaenda kwa Padre kumweleza haimaanishi kwamba dhambi yake imefutika. Dhambi ipo pale pale na itaambatana na kizazi chake. Sawasawa na mtu anaposema afanye mapenzi ya jinsia moja au kinyume cha maumbile kisha akatakaswe na padri au papa. That will never serve sins........

Kanisa liweke makatazo ya wazi kwa hawa viongozi wazee na wanaoongoza taasisi. Ifike wakati tusifungwe na katiba za kanisa tufungwe na maandiko matakatifu.

Hongereni KKKT na SDA kwa kusimama katika haki kipindi hiki cha mabeberu kutaka kuvamia dini kwa kigezo cha uchumi.
 
Watu wanabadilika, swali lako halina mashiko
 
Kuna vitu vingi vya kujifunza aisee...

Ndugu zangu tuenzi Mila na desturi za mababu zetu...

Hawa mabeberu wana jambo lao
 
Huu ni utamaduni mpya kama matumizi ya smartphone
Tuombe Mungu atulindie watoto wetu
Wakuu wa dunia wameamua iwe hivyo huezi kuzuia
 
Juzi kulikuwa na wiki ya kupinga ukatili wa kijinsia ikiwalenga wanaume peke yao kama ndio katili dhidi ya wanawake na watoto, kampeni hizi watu wengi hawataki kuziangalia kwa udadisi ni jinsi gani zinachochea mapenzi ya jinsia moja!

Kiashiria angalia nchi ambazo mapenzi ya jinsia moja yameshamiri nakuhalalishwa kisha angalia mkazo wa hizi sheria zinazompa mwanamke nguvu dhidi ya mwanaume tutapata majibu ya kijacho.

Ushauri wangu kwa serikali iangalie kwa umakini hizi harakati dhidi ya jinsia na kuidhinisha vilivyo sahihi na visivyo sahihi tuwaachie wenyewe huko magharibi vinginevyo tusikatae kula nyama isipokuwa mchuzi wake!
 
Back
Top Bottom