Panya Road wavamia Chamazi

Panya Road wavamia Chamazi

Kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia nilizopenyezewa na raia wema ni kwamba genge hatarishi la Panya Road limefanya uhalifu usiku huu katika maeneo ya Chamazi (Jimbo la Mbagala) na sasa wamekusanyika karibu na eneo la chuo cha afya cha Muhimbili lililopo Chamazi, wakilenga kuendelea na uhalifu wao kama kawaida. Hivi sasa wananchi wako roho juu wakihimizana kufunga milango ya nyumba zao na kuepuka kutoka nje ili kujilinda na uhalifu wa genge hili la kimafia linalozidi kutikisa jiji la Dar es Salaam siku hadi siku.

Nimeuweka uzi huu hapa kwa makusudi. Panya Road wametufikisha hapa baada ya kushindwa kudhibitiwa kikamilifu na vyombo vya ulinzi.

Tutapeana taarifa baadaye kadri ninavyozipata kutoka eneo la tukio. Wananchi wanaishi kwa hofu kubwa kufuatia kundi hili linalojibadilisha kila kukicha kutoka genge la wahalifu na kuwa kundi la kigaidi. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwalinda raia na mali zao na ikibidi wananchi wamilikishwe silaha nzito kwa ajili ya kujilinda wao wenyewe na mali zao. Kuna haja ya kuanzisha mafunzo ya lazima ya kijeshi kwa wananchi ili kuwajengea uwezo wa kujilinda.
majeruhi%20issa%20joseph.jpg
Hii nchi tumeringwa na Nani?
 
Nanyi si mujiorganize na mujiite paka road af munawasaka mpk kieleweke... Kila raia ni mlinzi kwa nafasi yake
 
KABLA YA POLICE KUWA AGRESSIVE NA HAWA
PANYA ROAD ....INABIDI WAZAZI NA JAMII INAYOWAZUNGUKA HAO WATOTO WAKAE NAO CHINI NA WAZUNGUMZE NAO....WAACHANE NA UJINGAA HUO WANAOUFANYAAA.....IKISHINDIKANA POLISI WAWASHUGULIKIE KAMA WANAVYO WAFANYAGA MAJAMBAZI......

OVA
 
Dawa ni Kuwaua tu,serikali ya mtaa iagize kila nyumba/kaya kuwa na Filimbi kama ya Refalii wa football wakitokea upande wenu mnapuliza kila mmoja wenu, na kutoka nje na silaha mbalimbali,mapanga,jambia,mishale ya sumu,mawe,acid,mikuki,marungu,tofali,mafuta ya taa then mnawaweka kati Wananchi mnamaliza shughuli,haiwezekani watu alfu 5000 mkashindwa kudhibiti kundi dogo LA vijana 30 na hiyo ni komesha popote watakapotokea,chonde msijifungie ndani
 
mkuu, lakini nadhani pia tangu polisi walipoacha kukaa vituoni usiku kundi hili limepata kasi ya kuendelea kuwatesa raia na kuwanyima raha kabisa. serikali inapaswa kufikiria upya uamuzi wake wa kufunga vituo ili polisi wachache waliopo washirikiane na wananchi kutokomeza kundi hili la kigaidi.
Ulinzi shirikishi ulipigwa marufuku kuu
 
Mzunguko mdogo wa hela mitaani ni moja ya kichocheo cha matukio haya.

Kwa mtazamo wangu,hawa ni vijana waliokata tamaa ya maisha na wako tayari kwa lolote kwani wanaona hawana cha kupoteza.
Sasa mwanaukawa mwenzangu mzunguko wa hela na watoto wa miaka 13-17 wapi na wapi

Au na wao wana majukumu ya kulea wazazi wangali wanalelewa
 
Kamanda Sirro vipi? Watu wanaishi kwa hofu kama wako vitani? Itafika kipindi wananchi watachukua Sheria mkononi halafu muanze kulaumu wakati waliopewa dhamana ya kulinda na kuhakikisha usalama wa wananchi wameshindwa kutimiza majukumu yao. Panya road hawajaanza jana wala juzi, hadi tabata walisumbua sana kipindi cha nyuma. Kama mnaona Jeshi la Polisi limeshindwa ruhusuni raia wajilinde wenyewe.
 
Kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia nilizopenyezewa na raia wema ni kwamba genge hatarishi la Panya Road limefanya uhalifu usiku huu katika maeneo ya Chamazi (Jimbo la Mbagala) na sasa wamekusanyika karibu na eneo la chuo cha afya cha Muhimbili lililopo Chamazi, wakilenga kuendelea na uhalifu wao kama kawaida. Hivi sasa wananchi wako roho juu wakihimizana kufunga milango ya nyumba zao na kuepuka kutoka nje ili kujilinda na uhalifu wa genge hili la kimafia linalozidi kutikisa jiji la Dar es Salaam siku hadi siku.

Nimeuweka uzi huu hapa kwa makusudi. Panya Road wametufikisha hapa baada ya kushindwa kudhibitiwa kikamilifu na vyombo vya ulinzi.

Tutapeana taarifa baadaye kadri ninavyozipata kutoka eneo la tukio. Wananchi wanaishi kwa hofu kubwa kufuatia kundi hili linalojibadilisha kila kukicha kutoka genge la wahalifu na kuwa kundi la kigaidi. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwalinda raia na mali zao na ikibidi wananchi wamilikishwe silaha nzito kwa ajili ya kujilinda wao wenyewe na mali zao. Kuna haja ya kuanzisha mafunzo ya lazima ya kijeshi kwa wananchi ili kuwajengea uwezo wa kujilinda.
majeruhi%20issa%20joseph.jpg
Wanamme wa dsm mna matatizo. Ninyi ndo mnaishi nao lkn unataka vyombo vya ulinzi viwabaini. Kwa nini usihamasishe jamii kushikamana na kushirikiana na vyombo vya dola?

Wanamme wa dsm nyie ni hovyooo kabisa
 
Mkuu delete hii post plz!! inakudhalilisha ndugu yangu... usifute thread Bali futa hii post uloandika Tusi
Mkuu unajua watu wengine bila kuambiwa kwa ukali ni wagumu wa kuelewa.
 
Ni kweli. Hili kundi hata sijui limeibukaje wakati Dar ilikuwa imenza kuwa tulivu. Serikali inapaswa kuwapa wananchi mafunzo ya kijeshi na kuwamilikisha silaha kwa ajili ya kujilinda na makundi ya kipuuzi kama hili la Panya Road.
Wewe utakuwa jambazi unayetafta kuhalalisha ujambazi wako. Yaani umilikishwe silaha? Zipi kwanza? Maana kama ni shortgun, pistol, sime, panga, kisu, ni vitu ambavyo ni ruksa kuvimiliki.

Bunduki zinahitaji utaratibu lkn silaha za jadi ni freee
 
Kamanda Sirro vipi? Watu wanaishi kwa hofu kama wako vitani? Itafika kipindi wananchi watachukua Sheria mkononi halafu muanze kulaumu wakati waliopewa dhamana ya kulinda na kuhakikisha usalama wa wananchi wameshindwa kutimiza majukumu yao. Panya road hawajaanza jana wala juzi, hadi tabata walisumbua sana kipindi cha nyuma. Kama mnaona Jeshi la Polisi limeshindwa ruhusuni raia wajilinde wenyewe.
na hili ndilo ninalopendekeza....kwamba serikali iwekeze kuwapa mafunzo ya kijeshi raia wake kwa lazima na kisha kuwamilikisha silaha ili wajilinde wenyewe...hakuna jinsi....maana polisi wameelekezwa na wakubwa wao ikifika saa 12 jioni wafunge vituo warejee makwao. sasa raia tutajilindaje ilhali hatuna mafunzo ya kivita na wala hatuna silaha? mimi naona ianzishwe JKT mpya ambayo raia wote wenye umri zaidi ya miaka 18 waende wakajifunze mbinu za kujilinda kwa kutumia silaha. kila raia akimilikiswa silaha hawa mbwa wanaojiita panya road hawakatizi mitaa bila kupasuliwa vichwa.
 
Wewe utakuwa jambazi unayetafta kuhalalisha ujambazi wako. Yaani umilikishwe silaha? Zipi kwanza? Maana kama ni shortgun, pistol, sime, panga, kisu, ni vitu ambavyo ni ruksa kuvimiliki.

Bunduki zinahitaji utaratibu lkn silaha za jadi ni freee
mkuu sijakuelewa bado. wewe unataka tumilikishwe silaha za jadi badala ya kumilikishwa silaha nzito? hujui kuwa panya road wanatumia silaha za jadi kuwadhuru raia?
 
Dar es salaam si salama hasa nyakati za Usk (saa 1-5) hata yake maeneo ya kishua. Ukijipendekeza kupiga boda jamaa wanakupa za mbao.
 
badala ya serikali ya CCM kulazimisha kuwapima watu UKIMWI nyumba kwa nyumba, ni wakati mwafaka wa kugawa silaha nyumba kwa nyumba kwa ajili ya wananchi kujilindia dhidi ya genge hili la panya road.
 
Kwakiswahili huitwa Genge la wahuni.. Kwa wenzetu huitwa Gang... Lengo lao la makundi haya ni kupata mali kwa njia zilizo na zisizo halali kwa kutumia umoja na kusaidiana..
Wananawatu wao ambao huwasupot kwa kutumia umaarufu wao na watu hao huitwa Gangstar..
Mfano Bongo vikundi hiv hutumia musiki wa singeli kujinadi...
Ukiwaskiliza mastar wa Singeli Tanzania kama Shoro mwamba na Man Fongo katika nyimbo zao malimbali au kwenye matamasha utasikia Wakisema "NAWAKUBALI WANANGU WA ROAD" Maana yake anawakubali Panya road, si hao tu yapo makundi mengi ambayo huyataja na hata wakienda mikoani huulizia kwanza makundi sumbufu ya mikoa husika na kisha kuyataja katika matamasha yao...
Fikiria msanii anafanya show alafu katikati ya show anauliza, "Kuna vibaka wangapi humu ndani? Vibaka wote nyoosha mikono ju".. Hata hivyo rekodi ni nying sana za uporaji na mambo ya uzalilishaji katika mziki wa singeli tenazikifanya katika show za mastaa wa mziku huu Tanzania,.
Siku hizi katika vigodoro vya singeli uswahilini wadau wa mzikii huu wanaenda wamevaa bukta(jezi za timu mbali mbali) ili mradi tu aonekane hana kitu ili asiporwe.
Singeli imeasisiawa kutoka kwenye mnanda na kigodoro, aina za miziki zilizopigwa marufuku kwa sababu za kujaa uhaifu na upungufu mkubwa wa maadili..
Lakini mziki wa Singeli sasa unapata umaarufu na kupewa support na midia kubwa nchini pia zikiigwa na midia ndogo kwa lengo la kupata waskilizaji zaidi, pia wapo wasanii wakubwa na wengineo walioonekana wanaharakati wamejitumbukiza kwenye mziki huu kurudisha umaarufu wao kwenye mziki na kujipatia fedha zaid kama Professa J bila kutazama upande wa pili wa Mziki huu...
Sina tatizo na Singeli kwakua unatoa ajira kwa vijana wengi ila mziki huu utazamwe upya kwani ni moja kichocheo cha uhalifu..
Huu ni utafiti wangu mdogo ila ni vyema utaft zaid ufanyike ili kujua vyanzo halisi vya matatizo kuliko kukata matawi nakuacha mizizi maana tunaona Panya road wengi ni watoto wadogo miaka kumi na nne na kuendelea wengine wao bado wapo shule, sasa ni ugumu wa maisha tuu au na kufuata mkumbo kwenye mikesha ya Singeli?
 
Back
Top Bottom