Dawa hii inayumika kama sumu ya panya. Je, ni salama kwa matumizi ya binadamu?

Jan 31, 2021
12
6
Ndungu zangu mm nimefika katika jukwaa hili ili niweze kutoa hili jambo ambalo binafsi limenitisha naomba kupata majibu kwa wataalamu, kuna dawa ya kutuliza maumivu kwa jina INDOSINE (si mtaalamu katika kuandika majina ya madawa).

Dawa hii imekuwa ikitumika kama sumu ya panya, na mimi binafsi nimeitumia kwani nilikuwa nasubumbuliwa sana na panya katika stoo yangu, ndugu zangu hii dawa imefanya vizuri sana kuliko dawa zote za panya nilizotumia zinazozalishwa nje na ndani ya Tanzania.

Sasa wasiwasi na swali langu, "hivi hii dawa itakuwa salama kweli kwa afya zetu sisi binadamu kama panya wanakufa kiasi kile na ukizingatia majaribio mengi ya tiba panya hutumika kama vijaribio?

Msaada kwa wataalamu wa madawa na afya. Asante.
 
Hiyo dawa inateketeza panya mpaka basi. Yaani ukiiweka kwenye chakula, panya watakula hicho chakula na kufa wote.

Ila cha kushangaza, eti imetengenezwa mahsusi kwa matumizi ya binadamu! Na wataalam wa afya wanasema ni dawa inayotumika kutuliza maumivu ya mifupa kwa binadamu.
 
Nimesikia kuna dawa za kuua magugu shambani ambapo kwa magugu ni sumu na mmea ni mbolea.Naona ni sawa na hiyo.

🤔🤔 Ngoja waje.
 
Back
Top Bottom