Panya Road, tunahitaji kufumua Jeshi la polisi?

Panya Road, tunahitaji kufumua Jeshi la polisi?

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
710
Reaction score
1,365
Jana majira ya saa saba usiku jirani yangu alivamiwa na wezi maarufu kama panya Road.

Walikuwa vijana zaidi ya kumi na tano huku wakiwa na mapanga na kuzua kadhia kubwa mtaani kwetu Bunju B..

Walivamia nyumba kadhaa na kujeruhi kwa mapanga.

Baada ya tukio kuisha ndio majirani tukaweza kutoka na kutoa msaada kwa ndugu zetu

Baada na nusu saa ndo police walifika na kuanza kufuatilia ikiwemo kupata maelezo ya majirani.

Jeshi la polisi mnawajibu mkubwa kuondoa hii "Taharuki" kwa wananchi ili waweze kufanya shughuli zao pasi na hofu.

Mh Rais ndo kwanza ameanza kufungua Nchi kwahiyo hivi vitu "Panya Road" vinaleta taswira mbaya sana ndani na nje hasa wawekezaji.

Rai yangu, Police kufanya Doria za mara kwa mara mitaani pia serikali iwekeze katika kuwapatia vifaa vya kisasa pamoja magari ya kutosha.
 
Polisi wakiwalamba shaba kuna wanaharakati wanalia haki za binadamu! Hawana ubinadamu hawa labda hujawahi kukutana nao.

Polisi fanyeni kazi yenu. Swala la panya road hupima mtafanya nini, ambush ndogo wanapiga kwingine.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Baada ya tukio ndo mkatoka kutoa msaada.. ni msaada Gani huo mlioutoa basda ya panya road kutoka
Wanaume wa DAR hao[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Police hawatoshi kukulindeni, jukumu la usalama ni lenu. Hao 15 tena wanakuja usiku mmeshindwa vipi kuwadhibiti kutoa Mfano wasije tena. Panya utafuna mitaa dhaifu ya waoga
 
Wabongo mtu unajenga nyumba unashindwa kujiongeza kuwa na chumba cha siri a.k.a panic room au hata bunker?tahadhari ni muhimu maana serekali imeshindwa kulinda raia na mali zake.
Hizo siyo level za wanaovamiwa na Panya road,mnaangalia sana movie,panic room ni akina Mo Dewji na marehemu Mengi.Wewe ulipokulia kulikuwa na panic room na bunker?
 
Screenshot_20230210-192656.png
 
Wabongo mtu unajenga nyumba unashindwa kujiongeza kuwa na chumba cha siri a.k.a panic room au hata bunker?tahadhari ni muhimu maana serekali imeshindwa kulinda raia na mali zake.
👀
 
Back
Top Bottom