Pamoja na kuvurugika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kwanini Waziri Jafo hajiuzulu?

Watu wa pwani hawanaga shida, ni watiifu, msimuonee , shughulikeni na chanzo.Sisi wa bara ni wababe tu tukubali ndio maana chini ya watu wa pwani na Zanzibar nchi ilikuwa na upendo, amani na utulivu, kimsingi nimeanza kuuchukia ukristo, malezi yake ni mabaya
Kila kona unayotembelea ndani ya nchi hii, hakuna habari nyingine unayokutana nayo, bali ni malalamiko ya vyama vya upinzani, kufanyiwa hila katika zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa kuenguliwa wagombea wake kugombea katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika hapa nchini, tarehe 24 mwezi huu.

Wakati ni kilio na kusaga meno kwa wapinzani nchi nzima, wenzao CCM ni kicheko na kushangilia kwa kuwa wagombea wake, wanatangazwa nchi nzima kupita bila kupingwa na hivyo kujipatia ushindi wa kishindo.

Hivi imefika hawa wasimamizi wa uchaguzi, kufikia hatua ya kum-disqualify, hata mgombea mwenye "diploma holder" kuwa hajui kuoma na kuandika, kwa kuwa tu ni mgombea wa upinzani??

Hivi kama nchi tutaendelea kuulea upuuzi huu hadi lini??

Ndipo hapo ninapojiuliza, hivi hii "fedheha" kubwa iliyolikumba taifa letu hivi sasa, ni kwa nini Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo, aendelee kukalia kiti chake na hajiuzulu?

Kama anagoma kujiuzulu, ni kwa nini Rais aliyemteua, ambaye najua fika kuwa ana "zero tolerance" kwa upuuzi wa aina aina yoyote unaoendelea nchini, asimfute kazi mara moja??

Na kama hatamfuta kazi, wananchi tutakuwa tumepata ushahidi wa "beyond reasonable doubt" kuwa yeye ndiye "mastermind" wa haya yote yanayotokea nchini kwetu hivi sasa
 
Back
Top Bottom