Uchaguzi 2019 Pamoja na kuvurugika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kwanini Waziri Jafo hajiuzulu?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
12,791
Points
2,000

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
12,791 2,000
Kila kona unayotembelea ndani ya nchi hii, hakuna habari nyingine unayokutana nayo, bali ni malalamiko ya vyama vya upinzani, kufanyiwa hila katika zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa kuenguliwa wagombea wake kugombea katika uchaguzi ujao unaotarajiwa kufanyika hapa nchini, tarehe 24 mwezi huu.

Wakati ni kilio na kusaga meno kwa wapinzani nchi nzima, wenzao CCM ni kicheko na kushangilia kwa kuwa wagombea wake, wanatangazwa nchi nzima kupita bila kupingwa na hivyo kujipatia ushindi wa kishindo.

Hivi imefika hawa wasimamizi wa uchaguzi, kufikia hatua ya kum-disqualify, hata mgombea mwenye "diploma holder" kuwa hajui kuoma na kuandika, kwa kuwa tu ni mgombea wa upinzani??

Hivi kama nchi tutaendelea kuulea upuuzi huu hadi lini??

Ndipo hapo ninapojiuliza, hivi hii "fedheha" kubwa iliyolikumba taifa letu hivi sasa, ni kwa nini Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo, aendelee kukalia kiti chake na hajiuzulu?

Kama anagoma kujiuzulu, ni kwa nini Rais aliyemteua, ambaye najua fika kuwa ana "zero tolerance" kwa upuuzi wa aina aina yoyote unaoendelea nchini, asimfute kazi mara moja??

Na kama hatamfuta kazi, wananchi tutakuwa tumepata ushahidi wa "beyond reasonable doubt" kuwa yeye ndiye "mastermind" wa haya yote yanayotokea nchini kwetu hivi sasa
 

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Messages
12,791
Points
2,000

Mystery

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2012
12,791 2,000
Jafo hawezi kujiuzulu, ajiuzulu kwasababu gani wakati ametimiza wajibu aliotumwa na boss wake?
Hivi Jafo anajua kuwa ni yeye ndiye anataka kuivuruga amani na anataka kuleta umwagaji damu nchini??

Hivi kukitokea machafuko hapa nchini kutokana na huu "uchafuzi" wanaoufanya, ni nani atalaumiwa??
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
47,289
Points
2,000

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
47,289 2,000
Hivi Jafo anajua kuwa amani ya nchi hii kwa hivi sasa ni yeye anataka kuivunja na anataka kuleta umwagaji damu nchini??

Hivi kukitokea machafuko hapa nchini kutokana na huu "uchafuzi" wanaoufanya, ni nani atalaumiwa??
Ukiwa CCM akili na ufahamu wako wote unausalimisha mfukoni mwa jiwe. Ukiwa na akili za Mussa Assad lazima utimuliwe na uchafuliwe.
Kiufupi, Jah Hana la kufanya zaidi ya kuitikia ndio mzee JIWE.
Bado wanadhani habari za machafuko Ni za Africa Kaskazini na Mashariki ya Kati
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
47,289
Points
2,000

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
47,289 2,000
Najua kuwa Jiwe ndiye aliyetoa maagizo yote hayo, lakini kwa muumini wa dini kama Jafo, ni kwanini akubali hili jumba bovu limwangukie??
Jah ni mganga njaa, jiwe akimwagiza ale sahani nzima ya kitimoto huku tukio Hilo likirushwa mubashara, atatii. Ila upumbavu Kama huo jiwe akimwagiza mtu mcha Mungu, muadilifu, mnyenyekevu na mweledi Kama Mussa Assad, kamwe hawezi jaribu. HUENDA akavua hata kiatu amtandike nacho jiwe usoni
 

sweettablet

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2014
Messages
3,867
Points
2,000

sweettablet

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2014
3,867 2,000
Hivi Jafo anajua kuwa ni yeye ndiye anataka kuivuruga amani na anataka kuleta umwagaji damu nchini??

Hivi kukitokea machafuko hapa nchini kutokana na huu "uchafuzi" wanaoufanya, ni nani atalaumiwa??
Jaffo anavuruga amani kwa lipi? Kama vipi lianzishe uone kwanini UKUTA haukufanikiwa.
 

Forum statistics

Threads 1,390,621
Members 528,220
Posts 34,056,665
Top