Pamoja na kutumia nguvu nyingi kuwasaidia Wabunge wa CCM kutinga Bungeni dalili zinaonesha watamuangusha Rais Magufuli

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Hili halina ubishi 85% ya wabunge wapo mjengoni kupitia mgongo wa Rais Magufuli, maana wengi wamechaguliwa kwa huruma za wananchi baada ya Rais kuwapigia debe majukwaani. Wao kama wao wasingetoboa hata kwa tindo na kotapini.

Napiga picha jinsi mbunge wa Geita mjini ambavyo alikuwa hakubaliki kwa wananchi mpaka akalazimishwa na Rais kuomba msamaha kwa wananchi mbele ya hadhara. Kama sio JPM huyu mbunge asingerudi mjengoni.

Sitaki kuongea mengi juu ya huyu mbunge bali wakazi wa Geita ni mashuhuda. Lakini amestaajabisha watu pale alipoamua kujitoa ufahamu na kutetea uovu ambao haustahili kutetewa hata kwa namna yoyote.

Hata kama hakuna ufisadi, unaweza kutetea manunuzi ya gari ya mil 460? Wakati wananchi wako wanaishi kwenye lindi la umaskini! Hivi huyu mbunge anapajua Shilabela? Nyankumbu na maeneo ya watu hohehae? Anajua maisha ya Geita kwa undani? Hivi Rais Magufuli alikuwa anapigia chapuo wabunge kama huyu?

Huyu ni mfano tu, nenda jimbo la Ilemela huko Mwanza. Ni kwamba wananchi hawamkubali huyu mama tena ni waziri mdogo. Lakini ukikaa maeneo ya Ilemela wananchi wana kilio kikubwa sana. Maji, barabara na miundombinu ni shida tu. Ni kama hawana mbunge kwa zaidi ya miaka mitano. Maana ni kero na shida.

Kwa ufupi Magufuli kama mwenyekiti wa CCM awe makini na wabunge ambao aliwapigia debe lakini pindi akiondoka madarakani atatuachia kilio kikubwa sana watanzania. Maana bungeni ni kama hatuna wawakilishi.

Rais anapinga matumizi ya pesa za umma yasiyofaa mbunge anatetea. Hivi hii Tanzania yetu imemkosea Mungu. Any way nimetoa mifano miwili ila tutaoumia ni sisi wanyonge ambao hatuna mbele wala nyuma.
 
Acha urongo wabunge hawakuchaguliwa na wananchi na rais mwenyewe hakuchaguliwa na wananchi.Wewe unajua hili,wananchi wanajua na dunia inajua.
Kweli kabisa, mimi nilikuwa msimamizi wa uchaguzi huu, katika kituo changu Lissu alipata kura 79 na Magufuli kura 31 lakini matokeo yaliyo bandikwa ni lissu 06 na Magufuli 370 hapakuwa na uchaguzi ilikuwa ni ujinga tu.
 
Huwezi kumuondoa Rais kama sehemu ya tatizo. Kama yeye hataki matumizi ya kufuru, kwanini kusiwe na mswada na sheria inayoweka ukomo wa matumizi ya kununua gari.

Sheria isema wazi "kutakuwa na kima cha labda 200Mn kwa ajili ya kununua gari"

Hivo yani!
 
Kweli kabisa, mimi nilikuwa msimamizi wa uchaguzi huu, katika kituo changu Lissu alipata kura 79 na Magufuli kura 31 lakini matokeo yaliyo bandikwa ni lissu 06 na Magufuli 370 hapakuwa na uchaguzi ilikuwa ni ujinga tu.
Nje ya mada, na madai hayana uthibitisho.
 
Huwezi kumuondoa Rais kama sehemu ya tatizo. Kama yeye hataki matumizi ya kufuru, kwanini kusiwe na mswada na sheria inayoweka ukomo wa matumizi ya kununua gari..
Lipo wazi, halmashauri wanatakiwa kutumia Prado, lakini halmashauri ina kata 13, kwa nini usinunue Suzuki maruti?
 
Acha urongo wabunge hawakuchaguliwa na wananchi na rais mwenyewe hakuchaguliwa na wananchi.Wewe unajua hili,wananchi wanajua na dunia inajua.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Acha ujinga wewe sisi wananchi ndo tulichagua nyie nyumbu mlikuwa mnavuka mto mnapambana na mamba,

lini mgejua uchaguzi ulikuwa huru wakati mlikuwa mnapambania maisha yenu kwa kutotumia akiri kuvuka mto.

Kama mnadhani watu milioni moja na ushee wanaweza kuzidi watu milioni kumi na mbili na ushee basi hamkutumia akiri bali ni makalio
Ni kitu gani kinakupa ufahamu kwamba Tundu angeshinda uchaguzi huo?
 
Acha ujinga wewe sisi wananchi ndo tulichagua nyie nyumbu mlikuwa mnavuka mto mnapambana na mamba,

lini mgejua uchaguzi ulikuwa huru wakati mlikuwa mnapambania maisha yenu kwa kutotumia akiri kuvuka mto. Kama mnadhani watu milioni moja na ushee wanaweza kuzidi watu milioni kumi na mbili na ushee basi hamkutumia akiri bali ni makalio
Ni kitu gani kinakupa ufahamu kwamba Tundu angeshinda uchaguzi huo?
Hivi wewe na Mimi Nani nyumbu ,una nini zaidi ya kujikombe na wakati mwingine mna rukishwa ukuta ili muweze kula? Mimi nafanya maisha yangu bila kutegemea siasa ila napenda haki.Na sitakujibu Tena.
 
Mlilazimisha kuwapa ushindi wasiostahili, wenye uwezo mdogo wa kuchambua mambo na kujenga hoja, mkayapiga teke maamuzi ya wananchi, leo mnaanza kulalamika mtam-let mwizi mwenzenu wa kura down!

CCM sijui mmelaaniwa na nani, kila mnalofanya kwa wananchi linageuka baya.
 
Mlilazimisha kuwapa ushindi wasiostahili, wenye uwezo mdogo wa kuchambua mambo na kujenga hoja, mkayapiga teke maamuzi ya wananchi, leo mnaanza kulalamika mtam-let mwizi mwenzao wa kura down!

CCM sijui mmelaaniwa na nani.
Pointless.
 
Back
Top Bottom