Best home tutor
Senior Member
- May 8, 2026
- 194
- 264
Leo nimewawaza sana wale watumishi wanaopitia madhira na manyanyaso, mateso na wakati mwingine kutengwa kazini kwao. Katika semina zangu za Uongozi wa Kimkakati, Itifaki, Maadili ya Uongozi na Ustaarabu, nimekuwa nikugusia eneo moja nyeti sana. Nalo ni kuepukana na majungu kazini.
Ofisi nyingi ziko kama ukanda wa vita wa Kandahar. Watumishi wanapigwa vita kulia kushoto. Wakati mwingine, vita hii inatokana na utendaji wao mzuri, kiasi kwamba unakuwa ni tishio kwa walio juu yao. Kiongozi bora ni yule anayelea na kuzalisha viongozi wa kesho. Viongozi wengi kote utumishi wa umma na sekta binafsi wamekwama sana katika pointi hii.
Afisa akionekana ana ujuzi na maarifa sana na kuonekana kumzidi mkubwa wake, majungu na vita vinaanzia hapa. Yupo Afisa mmoja alikuwa anafanya TPSF. Sitomtaja. Aliangalia video clip moja ambayo nilikuwa natoa mafunzo kwa viongozi wa shirika fulani, akaniandikia ujumbe mrefu sana DM. Nilipomaliza kuusoma, macho yangu yalijawa machozi kunilengalenga.
Aliyekuwa boss wake, ambaye ni Mwanamke, alimtesa na kumnyanyasa sana. Wakati mwingine kumtukana matusi ya nguoni, na nyakati zingine alikuwa akimtegea akosee apate sehemu ya kumsema na kumfokea. Kuna wakati alimuuliza, "hivi umeoa?" Kijana akajibu ndio. Yule boss akamwambia, mkeo ana kazi sana kuwa na mume kama wewe. Je, huu ni uongozi au ni ugaidi? Tena boss wa kike kwa afisa wa kiume.
Mara nyingi, wengi wameamini kuwa manyanyaso hutokea kwa watumishi wanawake ambapo labda boss wa kiume kamtaka na afisa kagoma. Lakini kwa experience ya huyu kijana, tunajifunza kuwa hata staff wa kiume wananyanyaswa sana na maboss wa kike.
Manyanyaso ni sehemu zote. Yaani boss wa kike na boss wa kiume anaweza kuwa ni mnyanyasaji mkubwa kwa staff wake. Yupo, dada mmoja kutoka Halmashauri moja, amenyanyasika sana hadi amefikiria kuacha kazi. Afisa Rasilimali watu katika ile Halmashauri ambaye nimetajiwa jina lake, anayoyafanya kwa watumishi sio sawa kabisa.
Viongozi, nafasi uliokalia ipo siku huyu unayempiga vita, kumnyanyasa na kumtesa, kumpiga majungu, ataikalia yeye. Vyeo ni kama daladala, abiria anapanda anashuka kituo kinachofata. Nafasi alioiacha anakalia abiria mwingine.