Pale Rais Magufuli anapomsifu Mkapa kwa demokdasia na utawala bora

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,095
Jana wakati Rais Magufuli anasoma hotuba ya Tanzia juu ya kifo cha Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, alizungumza mambo mengi mazito ambayo rais huyo aliyetutoka alilifanyia Taifa.

Kwa kweli Mkapa ameacha alama katika nchi hii, yeye ndiye aliyesuka engine ya Tanzania ya leo tunayoiona. Yeye alisuka mifumo mingi zaidi ambayo ndiyo nguzo mama ya nchi yetu kwa sasa.

1. Kama ni michezo, basi kuna TFF, kuna uwanja wa Mkapa — Kazi ya Mkapa hiyo

2. Kama ni barabara kuna TANROADS — Kazi ya Mkapa hiyo

3. Kama ni Elimu, kuna MMEM, MMES — Kazi ya Mkapa hiyo

4. Kama ni kupamvana na rushwa kuna TAKURU/TAKUKURU — Kazi ya Mkapa hiyo

5. Kama ni kupambana na Umasikini kuna TASAF, MKUKUTA, MKURABITA — Kazi ya Mkapa hiyo

6. Kama ni Afya kuna NHIF — Kazi ya Mkapa hiyo

7.Kama ni Elimu ya Juu kuna LOANS BOARD, TCU — Kazi ya Mkapa hiyo

8.Kama ni Maji kuna mradi wa Maji Ziwa Victoria hadi Shinyanga — Kazi ya Mkapa hiyo

9. Kama ni ushawishi duniani, kuna kupunguziwa Madeni — Kazi ya Mkapa hiyo

10. Kama ni kupambana na UKIMWI kuna TACAIDS — Kazi ya Mkapa hiyo

11. Kama ni kubuni vyanzo vya Mapato kuna VAT — Kazi ya Mkapa hiyo

Kilichonisukuma niandike huu uzi, ni kuhusu Fanikio moja la Mzee Mkapa ambalo rais Magufuli alilitaja mwanzoni kabisa katika listi ya mafanikio ya BWM katika utawala huu, nalo ni Demokrasia na Utawala bora.

Ni dhahiri, kama alivyosema Tundu Lissu. Kwenye suala la Demokrasia na Utawala bora, Utawala huu wa awamu ya Tano ukiulinganisha na Utawala wa awamu ya Tatu, basi Utawala wa awamu ya Tatu upo juu sana kulinganisha na sasa.

Sasa najiuliza, kama Magufuli anatambua kuwa Mkapa alivilea vyama vya siasa, kwa kutozuia shughuli halali za kisiasa, kwa kutoharibu chaguzi za serikali za mitaa, kwa kutonunua wapinzani, kwa kutowafungulia kesi za ajabu ajabu, kwa kusimamia bila nongwa kuvipa vyama ruzuku zao, Kwanini asifuate nyayo zake?

Kama amesema kuenzi mazuri yote ya Rais Mkapa, kwanini Magufuli asifuate nyayo za rais Mkapa kwenye demokrasia?

Rais Magufuli inabidi ajue tu kuwa kama anataka naye aje akumbukwe na wananchi kwa miaka mingi, kujenga vitu peke yake hakutoshi bali lazima asimamie na alinde haki za wananchi.

Makosa yote anayoyafanya kwa sasa akiwa madarakani hasa kukanyaga haki za makundi ya kijamii zilizoko kisheria na kikatiba yatakuwa nyayo za kukanyagia legacy yake pindi akitoka madarakani.

Wananchi huwa hatumkumbuki mwalimu Nyerere kwa sababu alijenga TAZARA au viwanja vya ndege au vyuo vya ufundi na chuo kikuu, au viwanda vya zana za kilimo UFI, au URAFIKI, Tanganyika Parkers na vinginevyo vingi tu, bali huwa tunamkumbuka kwa kuwa alikuwa anatetea Haki za Watu, kuheshimu katiba na kutuletea Uhuru licha ya kuwa tunajua kuwa naye kuna makosa aliyafanya pia katika utawala wake, lakini dhati yake kwenye Haki tunaifeel mioyoni, na hicho ndo kinatufanya tumkumbuke.
 
Mkapa katetea democrasia wapi wakati mauaji ya wazanzibar yaliyokea, cuf ngunguri kuvunjwa miguu, democrasia IPO wapi hapo?
 
Back
Top Bottom