Messenger RNA
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 1,105
- 3,026
ReutersCopyright: Reuters
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron amesema kuwa nchi yake haitavumilia shughuli za Iran, ambazo alizitaja kuwa za "uovu" katika nchi yake na Mashariki ya Kati.
Cameron alithibitisha katika mahojiano na gazeti la Uingereza la "The Sunday Telegraph" lililochapishwa Jumapili kwamba Uingereza itaimarisha ushirikiano wake na washirika ili kuendeleza hatua za dhidi ya Iran.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza aliishutumu Iran kwa kusaidia "mawakala" wake wa Hamas, Houthi, na Hezbollah kuyumbisha utulivu wa kimataifa, na akasema kuwa inatoa ndege zisizo na rubani, makombora na ujasusi wa kimbinu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza ameongeza kuwa, ujumbe wa onyo wazi lazima upelekwe kwa Iran kutovumilia mashambulizi ya Houthi dhidi ya meli za kibiashara katika Bahari Nyekundu.
Tangu katikati ya Novemba, kundi la Houthi nchini Yemen limeanzisha mfululizo wa mashambulizi dhidi ya meli za kibiashara zinazovuka Bab al-Mandab.
Kundi hilo lilisema kuwa lilikuwa likilenga meli za Israel, kujibu kile walichokitaja kuwa mauaji ya Israel katika Ukanda wa Gaza na kuzingirwa kwake.
Uingereza inashiriki katika muungano mpya wa kimataifa, "Guardian of Prosperity," unaoongozwa na Marekani, kulinda harakati za biashara katika Bahari Nyekundu dhidi ya mashambulizi ya Houthi nchini Yemen.
Pia ilitangaza vikwazo vipya vinavyolenga "wafanya maamuzi wa Iran na wale wanaotekeleza amri zake," akiwemo Ismail Qaani, kamanda wa Kikosi cha Quds cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran.
Cameron alipoulizwa kama London ilikuwa tayari kuweka hatua zaidi, alijibu kwamba suala hilii "sio kwa ajili ya kujadiliwa kwa umma".
BBC Swahili