PreGE2025 Padri Muchunguzi: Tunaachaje kuzungumzia siasa wakati waumini wetu ni wanasiasa? Tutawafundishaje?

PreGE2025 Padri Muchunguzi: Tunaachaje kuzungumzia siasa wakati waumini wetu ni wanasiasa? Tutawafundishaje?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Wakuu,

Tusubirie kusikia na huyu ameshambuliwa kwa sababu ya kusema ukweli? Tusubiri kusikia na huyu amepigwa vibaya na kuchukuliwa na watu wasiyojulikana sababu amesema ukweli?

Wataumiza na kuua wangapi mpaka wajue hawawezi kunyamazisha watu kusema kweli isipokuwa tu kwa kubadilisha mienendo na kiwajibika?

=====

Akiwa anaongea katika Maadhimisho Takatifu ya Kuwatengeneza wanafunzi wa Seminari ndogo ya Mtakatifu Maria Rubya na kuiombea Miito, Jimbo Katoliki Bukoba, Padri Muchunguzi amesema amesikia kauli ya Rais kuhusu viongozi wa dini kutojihusisha na siasa, Padri anasema wataachaje kuzungumzia siasa wakati waumini wao ni wanasiasa? Watawawekaje vizuri pale wanapopinda kwa kupindisha pindisha maneno?

Akawaambiwa wanafunzi waliokuwa wanahudhuria maadhimisho hayo kuwa kama kuna wazazi wao ni wanasiasa wasiogope kuwaambia ukweli pale wanapoona mambo hayaendi sawa.

Akasema kuna watu wanaweza kutumia maarifa waliyokuwa nayo vibaya kama watakuwa wanaamua wenyewe ikiwa hakutakuwa na usimamizi kwenye maarifa hayo kwenye siasa, mtu anaweza kuonekana mzuri lakini akawa na nia ovu tofauti na ujenzi wa taifa, na wa kuzungumza nao ni pamoja na viongozi wa dini, kwa kuubiri ukweli.

Ameongoza kuwa kama kiongozi wa dini ana wasiwasi wa kutetea ukweli ndio ataishia kusema hali ni shwari tanzania sio kama kongo, lakini inawezekana hali ikawa zaidi ya kongo ikiwa kama hutakiwi kusema ukweli wa hali halisi.

Akisema inashangaza mwanasiasa akiwa mgeni rasmi na kuongea atakachosema ndio kitaonekana kwenye taarifa ya habari na atakachosema muhubiri kitafichwa, halafu watu wanasema hapa ni shwari kuliko kongo!

Tusidandie ajenda za wanasiasa wakati waumuni wetu ni wanasiasa, tutawafundishaje?


 
Kifuatacho tuta uliza location ya makazi ya askari hao
Wanaposhinda na mienendo yao ili tukae mguu pande na kwenda nao sambasamba!

Tatizo ni kwamba wanaona watanzania ni waoga hawawezi kufanya jambo, lkn ipo siku kitawaka ikiwa haya hayatakoma, ule mstari wa uvumilivu utashindwa kustahimili tena, kutakuwa hakuna cha kupoteza.
 
Duh kapiga mule mule,hapindishi, mzanzibar hapumui mwaka huu,Kila Kona nshale
 
Anzisheni shule za siasa, jisajilini kama chama cha siasa.

Wapo waumini sio Wanasiasa pia hawapendi siasa
Na vipi raia wasio na vyama nao wakisema hawamtambui Samia maana hawakumchagua.
 
Back
Top Bottom