Viongozi wa dini kuingiwa na uwoga hata kusema uongo, hakuna utengano wa dini na siasa

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Andiko la Padri Titus Amigu, soma hadi mwisho acha uvivu.

=======

VIONGOZI WA DINI KUINGIA WOGA HATA KUSEMA UONGO

Dini hazijaanza jana, wala siasa hazijaanza jana. Kwa Wakristo Wakatoliki, kwa woga, watu wanafuja vipaimara vyao na sakramenti ya Daraja inayowafanya wawe makuhani, manabii na wafalme hapa ulimwenguni. Hao wanapatwa na woga kiasi hiki wanasema uongo wa kwamba dini haipaswi kuhusiana na siasa.

Ni uongo kabisa kwani hata Pasaka yenyewe, tunayoisherehekea kila mwaka, ni matunda ya mwingiliano wa dini na siasa. Wayahudi wanaokolewa kutoka katika mikono ya Farao (mwanasiasa). Musa alikuwa mtu wa dini lakini alipambana na Farao, mwanasiasa. Kumbe, kudai dini isihusiane na dini siyo tu woga unaowashika viongozi wa dini isipokuwa ni pia ishara ya kutoyajua Maandiko. Tangu mwanzo wa Biblia hata mwisho wake, watu wa dini walihusiana na wanasiasa. Abrahamu alihusiana na Melkizedeki, mfalme. Tena alihusiana na Farao kule Misri hata akalazimika kusema uongo wa kwamba Sara si mkewe akiogopa kuuawa. Yusufu alihusiana kisiasa na Farao sawia na Putifa na mkewe.

Musa ndiyo tusiseme alihusiana na Farao. Mapigo kumi dhidi ya Wamisri shauri lenyewe lilikuwa siasa, utumwa. Na tunajua pigo la kumi na mbili, kuuawa kwa wazaliwa wa kwanza wa wanyama na wanadamu wa Wamisri ndilo lililo asili ya sikukuu ya Pasaka. Tupo pamoja?
Naomba niendelee na mifano. Samweli alihusiana na wanasiasa Sauli na Daudi. Elisha alihusiana na akina Ahabu na Jezebeli. Isaya alihusiana na akina Sairusi. Yeremia alihusiana na siasa za wafalme wengi hata akatupwa katika shimo la simba. Danieli na wenzake walihusiana na akina Nebukadreza na Belshaza.

Manabii wote walihusiana na wafalme ama wakiwaunga mkono na kuwashauri au kuwaonya na kuwasahihisha. Yohane Mbatizaji alimkanya mwanasiasa Herodi Antipasi akalipia kwa shingo lake. Yesu mwenyewe alihusiana na wanasiasa kama akina Herode na Pilato. Mbona tunakumbuka kwamba Yesu alihukumiwa na Pilato.

Hatimaye, mitume nao walihusiana na wanasiasa, wengine wakali sana wakawatoa roho zao. Hata kitabu cha mwisho cha Biblia (ndiyo Ufunuo) ni mahusiano kati ya Dola ya Rumi na Wakristo. Makaisari walikuwa wanasiasa. Kaisari Konstantino aliyelisaidia Kanisa kupata nafuu ya madhulumu alikuwa mwanasiasa. Je, hatumsifu kwa kuwa mtu mwema?

Baada ya mitume, watakatifu mbalimbali walihusiana pia na wanasiasa kwa kuwaunga mkono au kuwakanya. Akina Thomas More na John Fisher walipotezaje maisha yao? Maximilian Kolbe alikufa katika muktadha gani? Kwa nini Baba watakatifu walioishi wakati wa biashara ya utumwa na hata wakati wa mauaji ya kimbari yaliyoendeshwa na Adolf Hilter dhidi ya Wayahudi wanalaumiwa kwa kutokuwa na misimamo ya kuwatetea wanyonge?

Si hivyo tu, historia ya Kanisa imejaa hati zinazohusika na mambo ya siasa. Rerum Novarum ina muktadha upi? Gadium et Spes ina muktadha gani, kwa nini tuseme Kanisa Ulimwenguni? Ulimwengu wa wapi wanaoishi wanadini peke yao pasipo dola, nchi na mataifa? Sasa inakuwaje ajabu au haramu kwetu sisi tunaoishi katika karne hii kujihusisha kwa namna yake na siasa?

Tusijipinge wenyewe. Kwa nini kila tunaposali sala za waumini tunaiombea serikali na viongozi wao? Tunawaombeaje ikiwa mambo yao hayatuhusu? Lakini ukweli ni huu. Tunaishi katika ulimwengu mmoja na wanasiasa. Ni katika ulimwengu huo huo tunamoaswa kufanya utume. Yesu Kristo hajawapa Wakristo ulimwengu wao peke yao (Yn 16:33).

Kama ndivyo, tutawezaje kuzungumzia mambo ya haki, amani na upatanisho pasipo kuwagusa wanasiasa na watawala ambao ndio wenye vyombo vinavyohusika na hayo? Anawezaje mwanadini kuzungumzia haki bila kuigusa nchi na watawala wake? Anawezaje mwanadini kuzungumzia haki na amani pasipo kuwagusa polisi na mahakimu?

Nadhani kama Wakristo wasingelikuwa raia wa nchi za ulimwengu huu na wanasiasa wasingelikuwa waamini wa dini za ulimwengu huu, dini na siasa vingeliweza kutenganishwa vizuri kabisa. Lakini kama waamini tusingelikuwa raia tusingelilipa kodi na wala tusingelishiriki chaguzi zozote na wanasiasa nao wasingelikuwa waamini tusingeliwatazamia waje kusali wala kushika amri yoyote ya Mungu. Kumbe basi, woga wetu usitufanye tuseme uongo wa kutaka dini na siasa visigusane, tunamuumiza sana Yesu aliyekuwa jasiri namba moja.

Ukweli ni kwamba wanadini siasa inatuhusu na wanasiasa dini inawahusu. Nani aliyesema mwanadini hawezi kuwa mwanasiasa na mwanasiasa hawezi kuwa mwanadini? Tusipotoshe mambo kwa woga wetu. Kumbe, kinachohitajika ni busara na kujali uwiano wa kusifiana, kuhimizana, kujadiliana na kuonyana ili wote tusiukose uzima wa milele. La sivyo, waamini na viongozi wao wasiseme wanashiriki ofisi za unabii na ufalme za Yesu Kristo!

Aidha, kukutana dini na siasa si ajabu. Kama tumetumwa ulimwenguni tukawafanye watu wote wanafunzi wa Yesu tusistaajabu kukutana na wafanyabiashara, wanasiasa, wema na wabaya. Acha nikumbuke wimbo wa zamani. Ni hivi kila mwamini, kwa sababu ya utume wake wa kimisionari ambao kwao anatakiwa kukutana na watu wote, anapaswa kujiimbisha wimbo wa zamani wa “Wote ni abiria wangu”, maana yake wanasiasa na siasa zao wamo kati ya abiria wake.

Ndimi mzee wenu Pd. Titus Amigu.
 
Sijasoma andiko lako maana ni refu na lilivyopangwa halihamasishi kulimaliza. Nimeagalia conclusion na nikaungana na wewe kwamba hakuna ukuta kati ya dini na siasa.

Mtu yeyote anayetaka kuvitenganisha ama anaogopa nguvu ya upande wa pili, ama hajui maana halisi ya dini, ama hajui uhalisia wa siasa na mahusiano ya hivi vitu katika maisha ya kila siku ya binadamu.

Siasa zinatengeneza mifumo ya mwongozo wa maisha ya kila siku ya binadamu katika kila jambo linalowahusu vikiwemo uchumi, usalama, mazingira, mahusiano, afya, technolojia, mawasiliano, desturi, mila, sheria n.k. Imani inakusudiwa kumfanya mtu ayaishi maisha yake yote Utakatifu na Ucha Mungu.

Unaposema Viongozi wa Imani wasihusike na siasa ni ujinga na upofu kwa kuwa imani inagusa maisha yote ya mtu kuanzia kabla hajaziwa, kuzlliwa, kuishi, kufa na baada ya kufa. Hivyo siasa ni sehemu moja tu katika maisha ya dini ambayo inahusisha wakati mtu yuko hai.
Lazima binadamu ashirikia katika kutengeneza mazingira sahihi ya uhai.

Wanasiasa msitake kujijengea ukuta wa kukataa maoni ya watu wengine kwa kisingizio cha dini ambazo nanyi mnazo ila pengine tu hamzielewi ipasayvo.

Hakuna miaka baina ya dini na siasa. Mipaka iliyopo ni uelewa, utashi na uwezo wa mtu kushiriki kwa kuwa binadamu tunavipaji, na viwango mbalimbali. Kama mtu wa dini anaweza kutoa michango kwenye uongozi bora, sioni kwa nini azuiliwe eti kwa kuwa ni kiongozi wa dini.

Iwapo mtu wa dini anaelimu ya technolojia, sioni nia njema ya kumzuia asifanye kwa kuwa ni kiongozi wa dini.

Iwapo mtu anaufahamu wa masuala ya kijeshi, budget, etc, sioni kwa nini azuiliwe ama asipewe nafasi afanye hivyo kwa maslahi ya taifa eti tu kwa kuwa ni kiongozi wa Imani.

Sioni Imani ya Kikristo inamzuia Kiongozi wa idara yoyote kufanya imani eti kwa kuwa anshiriki kutunga sheria za nchi katika bunge!

Imani hasa ya Kikristo ni mfumo wa maisha ya kila siku, siyo kitu cha msimu ama mahala fulani fulani. Waacheni Wakristo wenye sifa, nia na uwezo wafanye siasa ili tupate mipango, sheria na mtangamano safiii wa maendeleo ya taifa. Acheni woga.
 
Dini na Siasa vinaungana kwenye kudai haki.

Siasa za uongo, ghiliba, uonevu na hata mauaji dini inapinga.

Siku zote viongozi wa dini wanatakiwa kusimama upande wa wanaoonewa ili wapate haki.

Mifano yote iliyotolewa kwenye maandiko matakatifu inahusu kudai haki kwa wanaoteswa na watawala.
 
Dini na Siasa vinaungana kwenye kudai haki.

Siasa za uongo, ghiliba, uonevu na hata mauaji dini inapinga.

Siku zote viongozi wa dini wanatakiwa kusimama upande wa wanaoonewa ili wapate haki.

Mifano yote iliyotolewa kwenye maandiko matakatifu inahusu kudai haki kwa wanaoteswa na watawala.

Sheria gani inakubaliana na siasa za uwongo, Ghilba na mauaji? Hakuna!. Mtu anyefanya hayo hafanyi siasa bali anafanya uharifu!. Inahitaji kuwa na watu wa dini wenye nguvu katika ngazi za uongozi ili wasimamie utunzi na utelekezaji wa sheria zikiwemo za kudhibiti waharifu wa kisiasa wanaoonge auwongo na kufanya ghilba.

Hujaona watu wakihojiwa (ingwa hatuoni hatua zikichukuliwa) na PCCB kuhusu watoa rushwa kwa mfano?

Hujasikia watu wkailalamikia uharifu wa kunyamazia mauji ya kisiasa wakati sheria iko bayana juu ya murder?

Hakuna kitu kama upande wa dhambi wa siasa. Uvnjaji wa sheria ni uvunjaji hata ufanyike katika chaguzi, uongozi, afya, mawasiliano, ulinzi, uraiani n.k.

Msihalaishe uharamia wa wanasiasa majambazi na kuona hiyo ni siasa. Hakuna kitu kama hicho!.
 
Hao wanasiasa karibia wote wana dini zao, ndio maana wakati wa kuapishwa wote hushika vitabu vyao vitakatifu kuonesha watatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Kama hawataki kuihusisha dini na siasa, waache kushika vitabu vitakatifu wakati wakiapishwa.

Lakini zaidi, viongozi wa dini wakiwasifia CCM hakuna kelele zozote, ila viongozi wa dini wakiwakosoa CCM, hapo ndipo kelele zinapoanza.
 
Desparation ndiyo inayoleta haya! Mpeni huyo kijana agombee ubunge ama cheo ili ajiheshimu! Watanzania wa siku hizi ni watu wa ajabu sana. Mtu anatunga kitu kwa kuwa ameona waliofaidi vyeo awamu hii walipata hivo vyeo kwa njia hii! Dhambi ya mauti kutunga uwongo!
 
Sheria gani inakubaliana na siasa za uwongo, Ghilba na mauaji? Hakuna!. Mtu anyefanya hayo hafanyi siasa bali anafanya uharifu!. Inahitaji kuwa na watu wa dini wenye nguvu katika ngazi za uongozi ili wasimamie utunzi na utelekezaji wa sheria zikiwemo za kudhibiti waharifu wa kisiasa wanaoonge auwongo na kufanya ghilba.

Hujaona watu wakihojiwa (ingwa hatuoni hatua zikichukuliwa) na PCCB kuhusu watoa rushwa kwa mfano?

Hujasikia watu wkailalamikia uharifu wa kunyamazia mauji ya kisiasa wakati sheria iko bayana juu ya murder?

Hakuna kitu kama upande wa dhambi wa siasa. Uvnjaji wa sheria ni uvunjaji hata ufanyike katika chaguzi, uongozi, afya, mawasiliano, ulinzi, uraiani n.k.

Msihalaishe uharamia wa wanasiasa majambazi na kuona hiyo ni siasa. Hakuna kitu kama hicho!.

Uwepo wa sheria ni jambo moja na utekelezaji ni jingine.
Mashitaka yote ya jinai hutegemea viongozi wa serikali zaidi katika utekelezaji wake.
Kama serikali (viongozi) na zaidi sana Rais wa jamhuri hana nia ya kushitaki, kesi hiyo haitapelekwa mahakamani na hasa hasa pale ambapo jinai au uhalifu huo unamnufaisha kwa namna moja au nyingine.
Dini pia hutumiwa kama kichaka cha wahalifu kujificha. Chunguza matendo, maneno na mienendo ya viongozi wa dini kama kuna haki hapo.
Haki husimama yenyewe, haihitaji dini, serikali au siasa ili ionekane.
 
Ukiona Padre anaandika mambo kama haya wakati ndani ya miaka mitano kanisa katoriki walikaa kimya,kwa tunaoona nyuma ya pazia kunajabo litatokea
 
Back
Top Bottom