Padri amkimbia muumini

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,020
577
Source: Yahoo. friends

Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.

"padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"

"endelea"

"bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?"

"utasamehewa"

"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe na hiyo?"

"utasamehewa"

"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Yesu atanisamehe?"

"utasamehewa"

"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto. Yesu atanisamehe na hilo?"

- kimya........

"padri, Yesu atanisamehe kwa hilo?"

- kimya.........

Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka.

"sasa baba mbona umenikimbia?"

padri kwa taabu akajibu

"nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"​

 
Huyo kwa kweli anaogopesha, maana stahili yake akiona wako wawili ni kuua tu, ndio maana padre aliogopa akaona sasa ni zamu yake akaingia mitini!!!!!!! very interesting comedy!
 
hahahahahaaaaa.........tihitihihitihiitihhiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.............mbavu zangu weeeee.........mamaa wee....................uwiiiiiiiiiiiiii..................lo!!
 
nakumbuka hii kitu ilikuwemo humu majuma kadhaa nyuma
anyway, unadhania padri yeye haogopi? mmh aliona hapa jamaa kinachofuata ni mimi kwa nini asianzishe kivyake
 
Maisha ni mzunguko mkuu. Hata mitindo ya nguo ya sasa ilishakuwapo sana, sasa inajirudia ntu kwa wale ambao hawakuiona enzi hizo. Watu ndio hubadilika lakini matukio yanajirudia sana kwa faida na wala sio kwa hasara. Hata mie sikuiona uliyoiona wewe. Thanks.
 
Maisha ni mzunguko mkuu. Hata mitindo ya nguo ya sasa ilishakuwapo sana, sasa inajirudia ntu kwa wale ambao hawakuiona enzi hizo. Watu ndio hubadilika lakini matukio yanajirudia sana kwa faida na wala sio kwa hasara. Hata mie sikuiona uliyoiona wewe. Thanks.

Ni kweli, mimi pia nimeiona leo. Hata ningekuwa mimi ndio padri ningetafuta pa kwenda maana kifo si mchezo.
 
Mmeshupalia ilishakuwepo ili iweje wakati wengine hatukuiona kabisa...

asante sana umenifurahisha sana...
Barikiwa tafadhali.
 
asante sana, inafurahisha,yani tena ni story ambayo hujui mwisho wake nini ...so at the end...lol
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom