Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Baba Mtakatifu Fransisko amemteua mheshimiwa sana Padre Godfrey Jackson Mwasekaga wa Jimbo Kuu katoliki la Mbeya kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Mbeya , leo tarehe 09.03.2024
Mhashamu Askofu mteule Godfrey Jackson Mwasekaga alizaliwa Machi 17 mwaka 1976 Kyela, jimbo kuu Katoliki la Mbeya.
Baada ya Masomo yake ya upadre, alipata daraja takatifu la upadre Julai 14 mwaka 2005 jimboni Mbeya , kuhudumu katika nafasi mbalimbali za utume ndani ya jimbo Kuu la Mbeya. Hadi uteuzi wake Askofu Mteule Mwasekaga alikuwa Makamu Askofu wa Jimbo kuu la Mbeya.