Mojawapo ya kazi za kanisa na watumishi wake ni pamoja na:
1) Kuhubiri upendo
Katika upendo viongozi wakristo wanaaswa na Kristo kufanya kazi kama watumishi badala ya kuwa watawala. Kristo mwenyewe katika kulisisitiza hilo, aliwaosha miguu wafuasi wake (Yohana 13: 1-17, Mathayo 20: 25-27), kazi ambayo katika uyahudi ilikuwa ikifanywa na mtumwa kwa mgeni au mwenye nyumba anapoingia sebuleni. Ndani ya CCM na serikali kuna viongozi wakristo ambao hawafuati mafundisho haya, na hawa ni wafuasi na wanafunzi wa Kanisa ambao Padre mapunda ana haki na anawajibika kuwaambia kuwa wanavyofanya si kadiri ya mafundisho ya biblia bali ni ufuasi wa shetani. Na hapo Padre mapunda ana wajibu pia wa kuwaeleza wakristo wasimfuate wala kumtumikia shetani.
2) Kuijua na kuihubiri kweli
Viongozi wa kanisa wana wajibu wa kuwafundisha wakristo kweli ya kristo ambayo husimama katika haki. Yeyote anayeshirikiana na fedhuli kuwagandamiza watu wanyonge na maskini, ni tunda la shetani. CCM inaposhirikiana na serikali kuwaibia, kuwatesa, kuwadanganya na kuwatelekeza watanzania wanyonge, yeyote anayeshirikiana na CCM naye anakuwa ameshiriki uovu. Padre Mapunda ana haki na wajibu wa kuwaeleza waumini kutengana na wadhulumaji, wevi na waongo