Padre Baptist Mapunda atoa somo gumu Songea leo

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Kwa wana jf wote jina la Padre Baptist Mapunda si geni. Leo alikuwa anahubiri hapa kanisa la Mjimwema Songea mjini. Bahati nzuri leo hii ni sherehe za CCM kutimiza miaka 38.

Alisema leo wana sherehekea miaka ya 38 ya kuwatesa na kuwanyanyasa nyie wananchi. Hawa ni wauaji na nyie mnawa shangilia. Kuendelea kuichagua ni kujichoma sindano ya sumu. Unakufa taratibu. Anasema najua mpo wana CCM hapa nendeni mkamwambie Kikwete nipo hapa leo.

Katiba inayopendekezwa. Akauliza mnataka kuipigia kura ya ndiyo mmeisoma? Anauliza wangapi wanayo? Akanyosha mtu mmoja tu kanisa nzima. Mnaona umati wote huu anayo mmoja tu? Halafu unashabikia CCM. Kwanini hawasambazi mkaipata? Kimya kanisa lote.

Escrow na Askofu. Alimponda askofu aliyechukua milioni 80. Anasema yule askofu hana maadili. Unachukuaje hela usiyoijua wala usiyofanyia kazi,?

Hitimisho; CCM kuendelea kuiweka madarakani ni kujilisha sumu mwilini mwisho itakuua mwenyewe.

Hakika Padre huyu mahubiri yake unaweza kuyaogopa kama una moyo mwepesi
 
Huyu Mapunda ni kiongozi mkweli kwa kizazi cha sasa, Aibu kwa Kilain hadi viongozi wenzie wanasema hadharani anapaswa kuiomba radhi jamii.
 
Huyu padri namfahamu vizuri toka miaka ya mwanzo ya 2000 huwa anaongea ukweli bila kupepesa macho,yaani nyeusi anasema nyeusi na nyeupe anasema nyeupe,anasemaga kweli na siku zote kweli humweka mtu huru.
 
Kwa wana jf wote jina la Padre Baptist Mapunda si geni. Leo alikuwa anahubiri hapa kanisa la Mjimwema Songea mjini. Bahati nzuri leo hii ni sherehe za CCM kutimiza miaka 38.
Alisema leo wana sherehekea miaka ya 38 ya kuwatesa na kuwanyanyasa nyie wananchi. Hawa ni wauaji na nyie mnawa shangilia. Kuendelea kuichagua ni kujichoma sindano ya sumu. Unakufa taratibu. Anasema najua mpo wana CCM hapa nendeni mkamwambie Kikwete nipo hapa leo.
Katiba inayopendekezwa. Akauliza mnataka kuipigia kura ya ndiyo mmeisoma? Anauliza wangapi wanayo? Akanyosha mtu mmoja tu kanisa nzima. Mnaona umati wote huu anayo mmoja tu? Halafu unashabikia CCM. Kwanini hawasambazi mkaipata? Kimya kanisa lote.
Escrow na Askofu. Alimponda askofu aliyechukua milioni 80. Anasema yule askofu hana maadili. Unachukuaje hela usiyoijua wala usiyofanyia kazi,?
Hitimisho; CCM kuendelea kuiweka madarakani ni kujilisha sumu mwilini mwisho itakuua mwenyewe.
Hakika Padre huyu mahubiri yake unaweza kuyaogopa kama una moyo mwepesi

Tunahitaji viongozi wakweli wawazi na majasili, tunahitaji mashekh, wachungaji, na wazee wote waheshima kuungana kukemea uzalilishaji, ukandamizaji na unyanyasaji mkubwa unaofanywa na sisiem, Haki ni tunda lamani ambayo ccm wanaikanyaga.

kazi kubwa ya viongozi wa dini nikuhakikisha watawala na wataliwaliwa wanatenda kwa mujibu wa haki, kweli na heshima.
 
Fr. Mapunda, namfahamu vizuri, ni-mtu anayeamini katika kweli na huwa haogopi kusimamia haki na ukweli. Alikuwa hapa Mwanza miaka ya 1996-2002. Nilikuwa sikosi kanisani kusikiliza mahubiri yake.
 
Hongera Padri Mapunda kwa kutetea uokovu mkamilifu wa binadamu (mwili na roho).CCM inaangamiza miili ya watanzania, na huyu padri anatetea miili hiyo ili roho iokoke.
 
Nashangaa mijitu hala inashadadia ooh namfahamu huyo padre toka so n so... Kazi ya padre ni kuhubiri mambo ya mungu au habari za siasa. Ya kaisari amwachie kaisari
 
Rejesha kwanza ubongo uliouazimisha kwa jirani.
 
Maandiko Matakatifu yanatukumbusha kwamba, nyie msipomsemea, Yeye atatumia hata MAWE, kusema!
Keep it up, Bambo Mapunda.
 
Nashangaa mijitu hala inashadadia ooh namfahamu huyo padre toka so n so... Kazi ya padre ni kuhubiri mambo ya mungu au habari za siasa. Ya kaisari amwachie kaisari
-Kilaini alivyokuwa anampigia debeJK 2005 alikuwa anahubiri mambo ya Mungu au siasa?
 
Back
Top Bottom