Paco Decor amefariki

Status
Not open for further replies.

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,551
2,149
Amefia Aga Khan Dar, kule Instagram kumewaka moto kuhusu kifo chake.

Mimi ndio namsikia leo? Ni nani katika jamii maana mpaka Mange naye anamlilia?
Kumekua na hali ya sintonfahamu kwenye mitandao ya kijamii, kuhusiana na kifo cha aliyekua mwanamitindo na mpambaji maarufu bongo, Herry Pacor Nasser maarufu kama Paco decor.

Mpaka sasa hakuna taarifa ya wazi kuhusiana na kifo chake kama alikua mgonjwa, au alikufa kwa ajali, ila inasemekana march 8 ambayo ilikua siku ya jana marehemu alikua phuket, Thailand, na inasemekana masaa machache tu baada ya kutua nchini humo ikatangazwa kuwa mjasiliamali huyo ameaga dunia.

Ukweli ni kwamba kijana huyo mwenye jinsia tata amefia Thailand ila kifo chake mpaka sasa bado hakijajulikana, tutaendelea kuwa update kuhusiana na kifo chake mpaka ukweli ujulikane

Mmbea wenu mtiifu warumi Heineser
 

Attachments

  • IMG-20160308-WA0201.jpg
    IMG-20160308-WA0201.jpg
    124.8 KB · Views: 399
Alikuwa anavaa hereni kwanini?
Mungu hakumleta duniani na sikio limetoboka ila yeye kalitoboa sijui siku hizi twapotelea wapi
 
Alikuwa anavaa hereni kwanini?
Mungu hakumleta duniani na sikio limetoboka ila yeye kalitoboa sijui siku hizi twapotelea wapi
Ukiliangalia suala la kuvaa hereni katika upana wake, sijui kwanini kuvaa hereni kunahusishwa na ushoga! Katika tamaduni za baadhi ya makabila Tanzania (wasukuma, wamaasi, wagogo?, n.k.), wanaume uvaa mahereni tena makubwa na usuka pia. Kwa kweli uwa sielewi uvaaji huo kuhusishwa na ushoga.

Ukisema Mungu hakumleta duniani na sikio lilitoboka, je Mungu aliwaleta wanawake na masikio yaliyotoboka duniani? Je, Mungu alituleta duniani na kutuvisha suruali kwa wanaume na sketi/gauni kwa wanawake?

Ushoga ni tabia na hulka za mtu husika. Kwa mtazamo wangu mitindo (ambayo imekuwa defined na mwanadamu na siyo Mungu) haihusiani na ushoga, haswa ukizingatia baadhi ya mitindo hiyo imekuwa sehemu ya utamaduni wa kitanzania na hata kiafrika kwa baadhi ya makabila.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom