Ukijua pendo ukaishi na pendo, ni vigumu sana kuja ishi bila pendo. Ukiweza...usivue pendo, maana kuishi bila pendo ni kazi kama mtu mzima kuishi bila kipato. Maisha bila ya pendo baada ya kujua pendo, ni utumwa mkubwa moyoni na nafsini, haijalishi una nini vingine. Ukilijua pendo na kuishi na pendo maisha yako hupata maana mpya na bora zaidi. Tunza pendo ulipatapo, maisha bila ya pendo baada ya pendo ni jela ya nafsi na moyo.