NICK2275
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 3,930
- 924
Panetta: Bin Laden death photo to be releasedKwa kujadili hili tukio tutatia akili.Wale wanaosema tuhamie kwengine ni wale wavivu wa kufikiri na kutafuta ufumbuzi wa mambo.
Nimesoma revised story ya US kuhusu kifo cha Osama nahisi ndio kwanza utata unaongezeka.Lile jumba kama vile liko ndani ya kambi ya jeshi.Ilikuwa ni mzimu wa pamoja wa US na Pakistan.
Naendelea kuamini kwamba Osama ni marehemu zamani.Kama kuna mtu aliyatajwa kuuliwa basi ni mhanga mwengine wa operesheni hii.Haitokuwa rahisi kudadisi kwa watu wa kawaida na kujua ukweli kwani imeelezwa jumba limezungukwa na watu wa jeshi.Kwamba ilikuwa imetengwa na nyumba nyengine ni kuikosesaha jirani wa kutoa ushahidi juu ya jirani yao.
Watoto walio hai ambao imetajwa wanahojiwa bila shaka hawana asili ya Yemen au Saudia hivyo hakuna mtu atakayewatambua kama ni watoto wa Osama.Mkubwa wao ameuliwa.
Wanasema kulikuwa na wanawake wakijaribu kumhami Osama kwa kumzingira.Huo ulikuwa ni usiku mkubwa na tukio la kushtukiza,jambo hilo si rahisi kufanywa na mwanamke wa kawaida.Wangesema hao wanawake walizimia au walikuwa wakipiga mayowe sawa!.
Hii helkopta iliyoharibika baadae nani alikuja kuichukua?.Jeshi la Pakistan au wamarekani wenyewe?.
Uwezekano ni kuwa familia fulani ya kiCIA imetolewa kafara ili mchezo unoge.
Obama mwenyewe atakuwa kachezewa mchezo na mafreemasons au na wajomba zake mayahudi.Kwanini asitake kuuona mwili wa mtu aliyemuona ni adui mkubwa wa America angalau kwa sekunde chache ndipo ukatupwa baharini.Hajang'amua kwamba picha aliyokuwa akiangalia ni vidio fulani tu kutoka CIA?.
Makamanda waliomwamsha Obama usiku ashuhudie lile shambulio kwanini wasione umuhimu wa kumkabidhi mwili wa Osama halafu maamuzi mengine yakafanyika.Katika hizi stori haijaelezwa uamuzi wa kumtupa baharini ulifikiwaje na kwanini iliamuliwa iwe papo kwa papo.
Wanasema waliotoa taarifa ni wasaidizi wawili wa Osama mtu na nduguye ambao kwa ulofa wao walihisiwa hawangeweza kumiliki nyumba ile.Zaidi ya Osama katika lile jumba kulikuwa na familia nyengine tano.Walikuwa hawatupi takataka zao nje ya nyumba bali wakichoma moto tu.
Wanasema hiyo nyumba haikuwa na walinzi bali kuta nene tu.Wakati huo tangu waingie hapo ilikuwa ni vita tu.Nani walikuwa akipambana nao.
Hiyo nyumba ilikuwa haina simu wala internet,idadi ya kompyuter zilizokutwa na mafaili vya nini?.Labda waseme walikuta Laptop moja tu ya sheikh.
Osama katika hali ya uadui aliokuwa akiusikia umejengwa juu ya jina lake asingeweza kuwa na ofisi na mafaili nyumbani kwake.Nani hao angekubali waingie na kutoka nyumbani kwake kuchukua makaratasi na maelekezo?.Lazima wawe ni wale waliokuwa wakimlinda na haiwezi kuwa ni uamuzi wake.
Osama kwa nafsi yake alikuwa ni mtu mpole sana na hata kuzungumza kwa haya haya.Alikuwa na uelewa mpana wa athari za dunia kutawaliwa na wababe lakini mwenyewe hata bunduki kupiga kwa tabu.
Iwapo ushahidi wa Marekani kuhusu kifo cha Osama ni huu ni wazi kuwa aibu itawaandama na wamejimaliza.Iwapo wana ushahidi mwengine wanapaswa wautoe haraka kabla hawajachelewa na ikawa haiaminiki tena.Ndio maana muda mwingi niko kwenye net nikisubiri ushahidi mwengine.
nadhani siku watakayo toa hizo picha ndipo mtakapo funga midomo