BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
mpaka sasa hivi habari zinachanganya changanya jinsi zinavyotoka japo inaonekana wana huakika wamemuua.
Haikuwa na haja Obama kutoa habari kama bado wajamaliza dna tests na hawako tayari kuonesha picha zake .
Ni habari nyeti hizi Mkuu AW, bila shaka walishaziangalia prons & cons za kutangaza mauaji ya Osama kabla ya kuwa na ushahidi wa kutosha na ushahidi huo kutolewa baadaye na pia kukaa na habari hizi (sijui kwa muda gani) mpaka hapo wapate uthibitisho 100% kwamba kweli waliyemuua ni Osama. Kama habari hizo zingevujishwa kabla ya kutangazwa na Obama basi ingekula kwa Obama tena kwa kiwango cha juu sana.
Wamarekani wasingemuelewa kabisa Obama kukaa na habari hizo kwa siku kadhaa bila kuwatangazia Walimwengu.