Operesheni maalum za kijeshi

Operesheni maalum za kijeshi

Hiki ni Kikosi Alpha, chenye waendeshaji 22 wa SAS, wakiwa sehemu ya Operesheni Blood huko Afghanistan, mwezi Novemba 2001.
Operesheni Blood ilikuwa ni kurejeshwa kwa siri kwa vikosi vya A Squadron na G Squadron katika Uwanja wa Ndege wa Bagram. Operesheni hiyo iliweka msingi wa kile kilichokuja kujulikana kama Operesheni TRENt moja ya operesheni kubwa zaidi inayojulikana kiwahi kufanywa na SAS tangu Vita vya Pili vya Dunia.
 

Attachments

  • FB_IMG_1787243776060.jpg
    FB_IMG_1787243776060.jpg
    25.6 KB · Views: 7
Hiki ni Kikosi Alpha, chenye waendeshaji 22 wa SAS, wakiwa sehemu ya Operesheni Blood huko Afghanistan, mwezi Novemba 2001.
Operesheni Blood ilikuwa ni kurejeshwa kwa siri kwa vikosi vya A Squadron na G Squadron katika Uwanja wa Ndege wa Bagram. Operesheni hiyo iliweka msingi wa kile kilichokuja kujulikana kama Operesheni TRENt moja ya operesheni kubwa zaidi inayojulikana kiwahi kufanywa na SAS tangu Vita vya Pili vya Dunia.
FB_IMG_1787243776060.jpg
 
Pichani ni Greg Symonds, mwenye umri wa miaka 31, kutoka huko Newport, Wales, ambaye alikuwa mwanachama wa kikosi cha A Squadron, 22 SAS.
Huyu Symonds alikuwa amepitia njia ya Parachute Regiment kabla ya kujiunga na SAS. Alipitia safari ile ile ngumu ambayo wanajeshi wengi mahiri wa vikosi maalum vya Uingereza hupitia—kujithibitisha kwanza kama askari wa miamvuli, kisha kufaulu mafunzo magumu ya uteuzi wa UK Special Forces Selection yaliyomuwezesha kujiunga na SAS. Kwa mujibu wa waliomfahamu, alikuwa aina ya mwanajeshi ambaye kikosi hicho kilijengwa juu yake: mwenye uwezo, anayeheshimika na mtaalamu aliyefanya kazi zake kwa utulivu bila kujionyesha.
Kifo chake mnamo Machi 21, 2017, kilikuwa cha kusikitisha sana kutokana na mazingira kilivyotokea. Symonds alikuwa California, Marekani, akishiriki katika zoezi la mafunzo—kazi ya kawaida lakini muhimu sana inayowafanya wanajeshi wa vikosi maalum waendelee kuwa tayari na wenye ujuzi kati ya operesheni zao. Akiwa kwenye barabara yenye giza, aligongwa na gari ambalo dereva wake alitoroka na kumuacha akiwa amejeruhiwa vibaya. Symonds alifariki kutokana na kuvunjika kwa fuvu la kichwa baada ya kugongwa.
Baadaye, uchunguzi wa kifo chake uliofanyika Hereford ulisikia maelezo kuhusu tukio hilo. Juhudi za kumtafuta dereva aliyemgonga na kumwacha Symonds barabarani hatimaye zilisitishwa nchini Marekani.
Ni ukumbusho mchungu kwamba si kila mwanajeshi wa vikosi hivi hupoteza maisha vitani. Baadhi yao hufa katika nyakati za kati ya operesheni—wakati wa mazoezi, katika ajali au katika mazingira yaliyo mbali kabisa na uwanja wa vita. Hata hivyo, kwa wale waliotumikia pamoja nao, maumivu ya kumpoteza mwenzao hayapungui kwa sababu hakufa vitani.
Greg Symonds alitoa miaka ya maisha yake kulitumikia taifa lake katika kiwango cha juu kabisa cha utumishi wa kijeshi. Anastahili kukumbukwa kwa mwanajeshi aliyekuwa, kwa kujituma kwake, uwezo wake na huduma yake kwa nchi yake.
“Who Dares Wins” — Anayethubutu, hushinda.
FB_IMG_1787592329323.jpg
FB_IMG_1787592340589.jpg
 
Pichani hapa ni Kevin Holland akiwa na Saddam Hussein, muda mfupi baada ya kukamatwa kwake.
FB_IMG_1789419521788.jpg


Holland ndiye anayejulikana kuwa mwanajeshi pekee aliyewahi kuhudumu katika vitengo viwili vya siri vya kiwango cha juu zaidi nchini Marekani—kwanza katika kitengo maalum cha Jeshi la Wanamaji (Navy SMU), na baadaye katika kitengo maalum cha Jeshi la Nchi Kavu (Army SMU).


Alihitimu shule ya West Wilkes High School huko North Carolina mwaka 1988, kisha akajiunga na Jeshi la Wanamaji. Akiwa na umri wa karibu miaka 20 tu, alishiriki Vita vya Ghuba (Desert Storm) akiwa kama SEAL, akifanya upelelezi wa kina deep reconnaissance akisaidiana na mlenga shabaha sniper maalum kaskazini mwa Iraq. Baadaye alishiriki katika Operesheni kadhaa ukiwemo Provide Comfort na Uphold Democracy.


Akiwa miongoni mwa asilimia moja ya SEAL bora zaidi, Holland alichaguliwa kujiunga na Navy SMU. Aliondoka jeshini mwaka 1997 na kuwa afisa wa wanyamapori huko North Carolina. Lakini baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001, alirejea jeshini na baadaye akahamia Jeshi la Nchi Kavu, ambako alichaguliwa pia kujiunga na Army SMU.


Tarehe 13 Desemba 2003, Holland alikuwa Ad-Dawr, Iraq, akiwa sehemu ya Task Force 121 iliyokuwa ikimtafuta Saddam Hussein. Kikosi hicho kiligundua shimo dogo lililofichwa chini ya mabaki ya uchafu.


Holland alikuwa miongoni mwa waliomtoa Saddam Hussein ndani ya tundu hilo, wakimvuta kwa nywele na ndevu. Huku Holland akimuelekezea bunduki kifuani mwa Saddam, ikiwa tayari kwa matumizi, hadi alipothibitisha kuwa hakuwa na silaha.


Saddam Hussein, aliyekuwa akitafutwa kwa jina la “Ace of Spades,” alikuwa amekamatwa rasmi.


Mwaka 2011, huyu bwana Holland alipata jeraha kubwa vitani. Alistaafu mwaka 2013 baada ya miaka 25 ya utumishi.
 
Huyu ni Randy Shughart kwenye Vita ya Mogadishu
Inadaiwa kuwa hii ni mojawapo ya picha za mwisho zinazojulikana za Randy Shughart, sniper wa kitengo maalum cha Jeshi la Marekani (Army SMU). Picha hiyo ilipigwa muda mfupi kabla ya kuuawa pamoja na Gary Gordon katika eneo la ajali ya helikopta Super Six-Four, wakati wa Vita vya Mogadishu, Oktoba 3, 1993.
Shughart alizaliwa Lincoln, Nebraska. Alijiunga na Jeshi la Marekani mwaka 1976, kisha akarudi kwenye huduma ya kijeshi ya muda wote Desemba 1983 ili kuhudhuria mafunzo ya Special Forces. Baadaye alipata nafasi katika kitengo maalum cha Jeshi la Marekani (Army SMU).
Mnamo Oktoba 3, baada ya Super Six-One kuangushwa na Super Six-Four kushambuliwa kwa roketi ya RPG muda mfupi baadaye, Shughart na Gordon—ambao walikuwa wakitoa ulinzi kwa kutumia silaha kutoka angani—waliomba mara kadhaa washushwe chini ili kumlinda rubani Michael Durant na wafanyakazi wake.
Uongozi wa operesheni uliwakataa mara mbili. Lakini walipoomba kwa mara ya tatu, ombi lao lilikubaliwa.
Walifika kwenye eneo la ajali na kumtoa Durant kwenye chumba cha rubani. Kisha wakaanza kuwakabili wapiganaji wengi wa Kisomali waliokuwa wakikaribia, wakiwa na silaha zao binafsi pekee.
Gordon alipouawa, Shughart alichukua bunduki yake na kumpa Durant. Kisha akaendelea kupigana peke yake kwa takribani dakika nyingine kumi kabla ya kuuawa.
Durant alichukuliwa akiwa hai na kushikiliwa kwa siku 11 kabla ya kuachiliwa.
Baada ya vifo vyao, Randy Shughart na Gary Gordon walipewa tuzo ya Medal of Honor tarehe 23 Mei 1994. Walikuwa wanajeshi wa kwanza kupokea tuzo hiyo tangu Vita vya Vietnam.
FB_IMG_1791208451050.jpg
 
Back
Top Bottom