Operesheni "Gothic Serpent"!!!!!

General situation:
Wakiwa katika mji wa Mogadishu, wanajeshi wa kikundi hiki maalum waliishi katika mahanga(aina ya majengo ya kijeshi) ya kizamani pamoja na kwenye ma trela ya magari. Wakiwa hapo walikumbwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosekana kwa maji safi na salama katika eneo hilo pamoja na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo wa bw. Aidid (mortar attacks).
Mwezi September, kikundi hiki kilifanya misheni mbali mbali ambazo zilikua na mafanikio za kuwakamata waliokua wanamsapoti Aidid pamoja na kukamata silaha nyingi zilizokua zikitumika katika mashambulizi dhidi ya askari hao wa kimarekani. Vile vile ndege zilikua zikipaa na kupita katika maeneo ya miji ili kuweza kuisoma vyema mitaa na pia kuwafanya raia wa Somalia watambue uwepo wao (psychological warfare). Hii ilisaidia kwa kiasj fulani kuleta hofu dhidi ya wale wote waliokua wakishirikiana na Aidid.
Tarehe 21 mwezi huo huo wa September, kikosi hiko kilifanikiwa kumkata mfadhili mkuu wa Mohamed Farrah Aidid aliyeitwa Osman Ali Atto wakati delta team ilipovamia msafara wa magari uliokua unamsafirisha Atto kwenda nje ya mji.
Kwenye majira ya saa nane mchana tarehe 25 September, wafuasi wa Aidid walilipua kwa bomu la RPG(Rocket Propelled Grenade) helikopta ya kijeshi ya marekani aina ya black hawk na kuua askari watatu waliokuemo ndani ya helikopta hiyo katika eneo la bandari mpya karibu na mji wa Mogadishu. Japokua helikopta hiyo haikua ni mojawapo ya helikopta za kikundi kile maalum (the TASKFORCE ranger), huu ulikua ni ushindi mkubwa sana kwa Mohamed Farrah Aidid na SNA (somali national alliance).
The Battle of Mogadishu:
 
Wakuu mnisamehe kwa kupost kidogo², natumia notepad ya kwenye simu ndio maana. Tangu laptop yangu izingue up to right now sina access ya mashine that's why inabidi tu nitumie simu ila msijali, tuendelee kua pamoja.

Pole mkuu,wewe ku download evernote kwenye simu ni nzuri sana kuandikia
 
Mchana wa tarehe 3 October 1993, kikosi kile maalum (The TASKFORCE ranger) walipata taarifa za kiintelejensia kwamba viongozi wawili wakubwa wanaotokea katika ukoo wa Aidid walikua katika makazi ya eneo la bahari nyeusi (black sea) lililopo pembezoni mwa mji wa Mogadishu. Kikosi kile maalum kilituma ndege 19, magari 12 na askari 160 kwenda kuwakamata viongozi wale.
Wakati wa misheni hiyo, askari mwenye cheo cha private, Private Todd Blackburn alikosea kushuka kwa kwamba (fast roping) wakati wa kushuka kwenye helikopta aina ya MH-60 Black hawk. Alianguka umbali wa futi 70 kwenda chini na kujeruhiwa vibaya.
Viongozi wale wawili walikamatwa kwa uharaka na wote pamoja na private Blackburn wakaingizwa katika moja ya magari (convoy) yaliyokua chini. Ijapokua, wanamgambo waliokua na silaha pamoja na raia (wanawake na watoto) walizingira eneo lile na kuanza kushambulia. Sergeant Dominick Pilla na mpiganaji wa kisomali walikutana ana kwa ana ghafla na wote wakafyatuliana risasi kwa wakati mmoja. Wote wawili walifariki.
Makamanda wa operesheni walishtuka kupata taarifa ya kifo cha askari wao kwakua hawakutegemea majeruhi katika operesheni ile. Wakati wa masaa ya mwanzo ya mapambano, helikopta aina ya MH-60 Black hawk super six one iliyokua ikiongozwa na rubani aliyeitwa Cliff Walcott ililipuliwa na mpiganaji wa kisomali kwa kutumia silaha aina ya RPG. Marubani wote walikufa lakini askari waliokuepo ndani ya ile helikopta (crew members) walinusurika na kutua salama (crash landing).
Baadae, helikopta nyingine aina ya black hawk super six four ililipuliwa na RPG kutoka ardhini na wanamgambo wa kisomali. Hakukua na kikundi cha uokoaji cha haraka hivyo askari wachache waliosalimika akiwemo mmojawapo wa marubani aliyeitwa Michael Durant hawakuweza ku-move kutoka eneo walilokuepo.
Ma sniper wawili kutoka delta unit, master sergeant Gary Gordon na sergeant first class Randy shughart walitoa ulinzi (cover) wakiwa kwenye helikopta katika eneo lile helikopta ilipoanguka (crash site). Katika jaribio la tatu la kwenda kufanya uokoaji, walipewa kibali na wote walifahamu kwamba inaweza ikawagharimu maisha yao. Walipofika eneo la tukio, walijaribu kupambana ili kumiliki eneo lile na kwa bahayi mbaya Gordon aliuwawa na wakasalia Durant na shughart pekee.
Baadae, baada ya kupambana sana na kufanikiwa kuua zaidi ya wapiganaji 25 wakisomali, shughart aliuawa na Durant akachukuliwa mateka. Itaendelea
 
Wakuu mnisamehe kwa kupost kidogo², natumia notepad ya kwenye simu ndio maana. Tangu laptop yangu izingue up to right now sina access ya mashine that's why inabidi tu nitumie simu ila msijali, tuendelee kua pamoja.
Asante kwa uzi mtamu, nashauri kitu kimoja unapotoa mwendelezo uweke ktk post ya kwanza yaani unaedit ile post chini yake unaweka mwendelezo inakuwa vizuri kuzipata post zako kuliko bivi zinachngamana na comments
 
We wish to support you for the betterment of stories...napenda sana story za kijeshi
 
Asante kwa uzi mtamu, nashauri kitu kimoja unapotoa mwendelezo uweke ktk post ya kwanza yaani unaedit ile post chini yake unaweka mwendelezo inakuwa vizuri kuzipata post zako kuliko bivi zinachngamana na comments
Asante sana mkuu, nimekusom
 
Back
Top Bottom