Operesheni "Gothic Serpent"!!!!!

Mchana wa tarehe 3 October 1993, kikosi kile maalum (The TASKFORCE ranger) walipata taarifa za kiintelejensia kwamba viongozi wawili wakubwa wanaotokea katika ukoo wa Aidid walikua katika makazi ya eneo la bahari nyeusi (black sea) lililopo pembezoni mwa mji wa Mogadishu. Kikosi kile maalum kilituma ndege 19, magari 12 na askari 160 kwenda kuwakamata viongozi wale.
Wakati wa misheni hiyo, askari mwenye cheo cha private, Private Todd Blackburn alikosea kushuka kwa kwamba (fast roping) wakati wa kushuka kwenye helikopta aina ya MH-60 Black hawk. Alianguka umbali wa futi 70 kwenda chini na kujeruhiwa vibaya.
Viongozi wale wawili walikamatwa kwa uharaka na wote pamoja na private Blackburn wakaingizwa katika moja ya magari (convoy) yaliyokua chini. Ijapokua, wanamgambo waliokua na silaha pamoja na raia (wanawake na watoto) walizingira eneo lile na kuanza kushambulia. Sergeant Dominick Pilla na mpiganaji wa kisomali walikutana ana kwa ana ghafla na wote wakafyatuliana risasi kwa wakati mmoja. Wote wawili walifariki.
Makamanda wa operesheni walishtuka kupata taarifa ya kifo cha askari wao kwakua hawakutegemea majeruhi katika operesheni ile. Wakati wa masaa ya mwanzo ya mapambano, helikopta aina ya MH-60 Black hawk super six one iliyokua ikiongozwa na rubani aliyeitwa Cliff Walcott ililipuliwa na mpiganaji wa kisomali kwa kutumia silaha aina ya RPG. Marubani wote walikufa lakini askari waliokuepo ndani ya ile helikopta (crew members) walinusurika na kutua salama (crash landing).
Baadae, helikopta nyingine aina ya black hawk super six four ililipuliwa na RPG kutoka ardhini na wanamgambo wa kisomali. Hakukua na kikundi cha uokoaji cha haraka hivyo askari wachache waliosalimika akiwemo mmojawapo wa marubani aliyeitwa Michael Durant hawakuweza ku-move kutoka eneo walilokuepo.
Ma sniper wawili kutoka delta unit, master sergeant Gary Gordon na sergeant first class Randy shughart walitoa ulinzi (cover) wakiwa kwenye helikopta katika eneo lile helikopta ilipoanguka (crash site). Katika jaribio la tatu la kwenda kufanya uokoaji, walipewa kibali na wote walifahamu kwamba inaweza ikawagharimu maisha yao. Walipofika eneo la tukio, walijaribu kupambana ili kumiliki eneo lile na kwa bahayi mbaya Gordon aliuwawa na wakasalia Durant na shughart pekee.
Baadae, baada ya kupambana sana na kufanikiwa kuua zaidi ya wapiganaji 25 wakisomali, shughart aliuawa na Durant akachukuliwa mateka. Itaendelea
Mkuu mbona kama unahadithia filamu ya BLACK HAWARK DOWN?.... naona unaenda hatua kwa hatua kwenye hii filamu?
 
hizi habari za nusunusu hizi zinanikera sana ukianza maliza kunawachambuzi wa makala ndefu mwanzo mwisho wanakuja
 
Hapo ndipo Hollywood wakaja na bonge la movie Black Hawk Down.
Kama vile haitoshi jamaa wakaongeza na game Delta Force; Black Hawk Down.
Kama sijakosea operation hii ina a.k.a The Battle of Mogadishu
Hii iliwapa funzo kubwa kuwa in future mashambulizi ya helcopter yanabidi yasaidiwe na wanajeshi wa ardhini.
Kipigo walichopata kamwe hawawezi kukisahau na kiliwapa funzo kubwa
 
Back
Top Bottom