Mwamuzi wa Somalia wa Kombe la Dunia akataliwa kuingia nchini Marekani

Mwamuzi wa Somalia wa Kombe la Dunia akataliwa kuingia nchini Marekani

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
185
Reaction score
307
20260609101630483.jpg
Gazeti la New York Times hivi karibuni limetoa ripoti ikisema, mwamuzi wa Kombe la Dunia la mwaka 2026 ambaye ni raia wa Somalia Omar Artan, amekataliwa kuingia nchini Marekani.

Artan alikuwa mmoja wa waamuzi 7 wa Afrika waliochaguliwa kwa Kombe la Dunia la mwaka 2026 litakalofanyika nchini Marekani na Mexico, pia alichaguliwa kuwa Mwamuzi Bora wa Mwaka na Shirikisho la Soka la Afrika mwaka jana.

Hii siyo mara ya kwanza kwa watu muhimu wa Afrika kukataliwa kuingia nchini Marekani katika muda mrupi uliopita. Mwezi Aprili, Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Enoch Godongwana na Gavana wa Benki Kuu ya nchi hiyo Lesetja Kganyago walishindwa kuhudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Wakuu wa Benki Kuu wa Kundi la G20 uliofanyika nchini Marekani baada ya kukosa idhini ya kuingia Marekani.

Uzoefu wa Artan unaonesha sera za kibaguzi za serikali ya Marekani kwa Somalia na bara zima la Afrika. Desemba mwaka uliopita, rais Donald Trump wa Marekani aliwaita wahamiaji wa Somalia kama “watu wasiofaa” na kudai kwamba Somalia “haistahili kuwa nchi”. Zaidi ya hayo, Marekani imeweka vikwazo vikali vya usafiri na visa dhidi ya Somalia, ambavyo vinamaanisha kwamba hata mtu muhimu kama Artan hawezi kuingia nchini Marekani.

Wakati Marekani inapomkataa Artan, serikali ya nchi hiyo ilikuwa ikishirikiana na Somalia kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya kile kinachoitwa “maeneo yanayolengwa yenye silaha” nchini Somalia, ili kulinda usalama wa Marekani. Kwa upande mmoja, Marekani inahitaji ushirikiano wa Somalia katika kupambana na ugaidi, kwa upande mwingine, inawaaibisha Wasomalia bila ya sababu.

Michezo inapaswa kuvuka mipaka ya kitaifa, rangi, na siasa, na Kombe la Dunia linaashiria hamu ya binadamu ya umoja na amani. Hata hivyo, mwamuzi wa Kombe la Dunia anapozuiwa kuingia nchini Marekani kwa sababu tu ya uraia wake, ndoto hii inavunjwa.

Artan kukataliwa kuingia nchini Marekani sio tu ni msiba kibinafsi, bali pia ni mfano mdogo wa dhuluma ya kimfumo ya Magharibi dhidi ya nchi za Afrika. Wakati michezo haiwezi kuepuka kivuli cha siasa, na wakati talanta na bidii haviwezi kushinda ubaguzi, jamii ya kimataifa bado ina safari ndefu ya kufikia usawa na haki ya kweli
 
Fifa nao ndo wahuni. Hili jambo lilihitaji diplomasia kuliweka sawa. Walishindwaje kufanya clearance kwa watu wake mhm wanaingia US?
 
Mmeifanya kuwa dili
Marekani keshasema watu wa Somalia hawataingia nchini kwake
Nawaomba wa Marekani was hiki lie hapo hapo maana watu hao wakiingia huko Marekani hufanya madudu mengi sana wanautumia uhuru wanaopewa huko vibaya!!
 
Sio Yeye tu timu nzima ya Iran imepigwa chini kucheza kombe la dunia.
Kwasasa wanasomeka kama Magaidi,wanaweza kwenda na mabomu wakalipua popote kule huku wamesema wachezaji.
 
Back
Top Bottom