Vikundi maalumu vya Kijeshi visivyo rasmi ni hatari

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
6,405
Reaction score
12,707
Hivi vikundi maalumu vya kijeshi visivyo rasmi vinavyo tumika kulinda mamlaka kwa njia yoyote ni hatari sana tena zaidi ya hatari.

Huko tuendako kama nchi ni hatari hivi vikundi vikiendelea kuchekewa na kutumika kuumiza na kuua watu katika mfumo usio rasmi ni njia mbaya.

Hivi vikundi vikilewa madaraka huwa ni vibaya sana kwanza huwa sio jeshi rasmi hivyo hata mfumo wake wa kupokea order ni tofauti kabisa na jeshi rasmi la wananchi JWTZ au jeshi la Polisi.

Hivi vikundi hujishikiza na walioviunda huwa vipo juu ya majeshi yote kwa sababu hata kikatiba huwa havipo rasmi hivyo vinatenda na kudharau nguvu na mamlaka ya majeshi yote rasmi yanayo tambulika.

Ni rahisi zaidi nchi kuingia katika vita dhidi ya ugaidi au civil war kutokana na uwepo wa vikundi hivi.

Mimi yangu nimemaliza najua nchi hii ina Rais iwe wa kuchaguliwa na wananchi wote ama laah pia nchi hii ina mkuu wa majeshi na hata mkurugenzi wa idara ya usalama wa Taifa haijalishi ni kwa namna gani chama cha mapinduzi kimeharibu hii nchi toka uhuru mpaka sasa tena hasa huu utawala uliopo sasa madarakani lakini nawasihi tumieni hata punje za akili zenu huu ni wakati sahihi kuiokoa nchi huko mahali tuendako ni pabaya.

Haya makundi huchipua kama mchicha baadae hugeuka mbuyu na hapo ndipo ambapo yanakuwa hayawezi kuzuilika na mamlaka za ndani.

Leo yanaweza kuwa upande wenu kesho yakawa yana pambana nanyi huku maafa makubwa yakiwafikia wananchi wasio na hatia kutokana na uzembe na upuuzi wenu.

Nawakumbusha tena kila mwaka mnazalisha vijana wa JKT walio na mafunzo na kuwarudisha mtaani huku mkiendelea kuchekea makundi ya kipuuzi kama haya.

Nanawa mikono kama Pilato.
 
Hata mmilikiwa wa kundi hili la chui keshasema hili kundi halimsikilizi yeyote upo sahihi huko tuendako halitakuwa controled na yeyote maana yake linaeza kuleta maafa makubwa,pia huenda likapata ufazili kutokq nchi za kiislamu ili lianze kupambana na wakristo
 
Ndio maana tunasema katiba mpya ni jambo la lazima na haliepukiki, maana mambo yanavyozidi kwenda nchi itatumbukia katika machafuko sababu ya familia chache tu za mafisadi zenye uchu wa madaraka na kulazimisha kukubaliwa.

Inashangaza sana mtu aliyetudanganya/aliyejidanganya amechaguuliwa kwa mamilioni ya kura sawa na 98% hajamaliza hata mwaka anakumbana na kukataliwa na upinzani mkali sana hadi anatumia mitutu kuhadaa watu.

Sheria ya ulinzi wa taifa inazuia uundaji wa jeshi nje ya mfumo rasmi [militia/junta] ilq leo mtu anajiundia genge la wanamgambo kwa baraka za CCM na majeshi yote yaliyowekwa kwapani na kuwa majeshi ya CCM yanabariki uhuni huu mtu anafanya hadi press zaidi ya mara 3 kutishia watu ndio unakuja ule msemo ukimuona kobe juu ya mti ujue amepandishwa.

Tukirudi katika muktadha huo tunaona pia jeshi kuwa deployed mitaani sawa na polisi ni kinyume na katiba sababu majukumu ya wanajeshi sio kuzagaa mitaani ilhali hali ya hatari haijatangazwa.

Ufuataji katiba kwa sasa haupo nchi iko autopilot kesho tusishangae watu wasio na mafungamano na CCM nao wakiunda vikundi vya wanamgambo kupambana na CCM tutakua hatuko sahihi kuwakemea maana kama akina Mwaipopo wameunda vikundi hivyo kwa baraka za CCM hao watu watakua sahihi kuunda vikundi pia kujibu mapigo kwa CCM.

Kwa majirani hapo tuliona baada ya bunge kuvamiwa na kuchomwa mwezi June 2024 ndio waziri wa ulinzi kwa idhini ya bunge na kwa kunukuu vifungu vya katika aliomba jeshi la Kenya liwe deployed mitaani kuimarisha ulinzi na sio kama tunavyoona kinyume na katika Tanganyika jeshi liko mitaani wakati hakuna notice yoyote na bado linashirikiana na wanamgambo wa Mwaipopo.
thumb_1200_1698.png
 
Hivi vikundi maalumu vya kijeshi visivyo rasmi vinavyo tumika kulinda mamlaka kwa njia yoyote ni hatari sana tena zaidi ya hatari.
Moja ya majukumu ya msingi ya JWTZ ni "kufundisha umma shughuli
za ulinzi wa Taifa".
===
Sasa tusiumize vichwa, waulize JWTZ kama vikundi hivi uviitavyo vikundi maalumu vya kijeshi, vina baraka za JWTZ kwa kufundishwa shughuli za ulinzi wa Taifa,? maana vikundi hivyo vyaonekana ni sehemu ya umma uliotajwa kwenye majukumu ya msingi ya JWTZ.
 
Vinaanza kama mzaha lakini matokeo yake ni makubwa sana.
Hii yote ni kutokana na kuwa na viongozi wenye upeo mdogo sana wa akili .
Rais,IGP,DGIS wote elimu zao ni za kuungaunga tu unatagemea nini kama nchi.
Mwaipopo ana kikundi Cha kuilinda nchi technically anamaanisha jeshi la polisi na wananchi limeshindwa kuilinda nchi.
Kama nchi tunaongozwa na wajinga na wanaotuongoza wanatuona wajinga zaidii.
 
Hivi vikundi maalumu vya kijeshi visivyo rasmi vinavyo tumika kulinda mamlaka kwa njia yoyote ni hatari sana tena zaidi ya hatari.

Huko tuendako kama nchi ni hatari hivi vikundi vikiendelea kuchekewa na kutumika kuumiza na kuua watu katika mfumo usio rasmi ni njia mbaya.

Hivi vikundi vikilewa madaraka huwa ni vibaya sana kwanza huwa sio jeshi rasmi hivyo hata mfumo wake wa kupokea order ni tofauti kabisa na jeshi rasmi la wananchi JWTZ au jeshi la Polisi.

Hivi vikundi hujishikiza na walioviunda huwa vipo juu ya majeshi yote kwa sababu hata kikatiba huwa havipo rasmi hivyo vinatenda na kudharau nguvu na mamlaka ya majeshi yote rasmi yanayo tambulika.

Ni rahisi zaidi nchi kuingia katika vita dhidi ya ugaidi au civil war kutokana na uwepo wa vikundi hivi.

Mimi yangu nimemaliza najua nchi hii ina Rais iwe wa kuchaguliwa na wananchi wote ama laah pia nchi hii ina mkuu wa majeshi na hata mkurugenzi wa idara ya usalama wa Taifa haijalishi ni kwa namna gani chama cha mapinduzi kimeharibu hii nchi toka uhuru mpaka sasa tena hasa huu utawala uliopo sasa madarakani lakini nawasihi tumieni hata punje za akili zenu huu ni wakati sahihi kuiokoa nchi huko mahali tuendako ni pabaya.

Haya makundi huchipua kama mchicha baadae hugeuka mbuyu na hapo ndipo ambapo yanakuwa hayawezi kuzuilika na mamlaka za ndani.

Leo yanaweza kuwa upande wenu kesho yakawa yana pambana nanyi huku maafa makubwa yakiwafikia wananchi wasio na hatia kutokana na uzembe na upuuzi wenu.

Nawakumbusha tena kila mwaka mnazalisha vijana wa JKT walio na mafunzo na kuwarudisha mtaani huku mkiendelea kuchekea makundi ya kipuuzi kama haya.

Nanawa mikono kama Pilato.
Mpaka hapo ilipofikia,ukidokezwa kwamba CCM huwapatia silaha na fedha UVCCM na vikundi vingine vya wahuni kuteka,kutesa na kupoteza/kuua utabisha kweli? Kwenye kampeni za chaguzi hayo makundi huwa wakatili kukiko The Janjaweeds na Interahamwe!
 
Lile kundi letu na captain Tesha liko wapi ? Mbona mnatoa milio ? wajinga mlivyovunja sehmu za watu na kufanya uharibu hamtoruhusiwa hata kutoka , wasiohusika na mambo ya maandamano ni wengi so hatutaki. Hata sungsungu itabidi walinde mchana dhidi ya nyie vibaka wajinga wajinga.
 
Kumbe Mwaipo anajeshi lenye Askari 38,000:
Anawalipaje au kwa ufadhiri wa Iran na Yemen:
 
Hivi vikundi maalumu vya kijeshi visivyo rasmi vinavyo tumika kulinda mamlaka kwa njia yoyote ni hatari sana tena zaidi ya hatari.

Huko tuendako kama nchi ni hatari hivi vikundi vikiendelea kuchekewa na kutumika kuumiza na kuua watu katika mfumo usio rasmi ni njia mbaya.

Hivi vikundi vikilewa madaraka huwa ni vibaya sana kwanza huwa sio jeshi rasmi hivyo hata mfumo wake wa kupokea order ni tofauti kabisa na jeshi rasmi la wananchi JWTZ au jeshi la Polisi.

Hivi vikundi hujishikiza na walioviunda huwa vipo juu ya majeshi yote kwa sababu hata kikatiba huwa havipo rasmi hivyo vinatenda na kudharau nguvu na mamlaka ya majeshi yote rasmi yanayo tambulika.

Ni rahisi zaidi nchi kuingia katika vita dhidi ya ugaidi au civil war kutokana na uwepo wa vikundi hivi.

Mimi yangu nimemaliza najua nchi hii ina Rais iwe wa kuchaguliwa na wananchi wote ama laah pia nchi hii ina mkuu wa majeshi na hata mkurugenzi wa idara ya usalama wa Taifa haijalishi ni kwa namna gani chama cha mapinduzi kimeharibu hii nchi toka uhuru mpaka sasa tena hasa huu utawala uliopo sasa madarakani lakini nawasihi tumieni hata punje za akili zenu huu ni wakati sahihi kuiokoa nchi huko mahali tuendako ni pabaya.

Haya makundi huchipua kama mchicha baadae hugeuka mbuyu na hapo ndipo ambapo yanakuwa hayawezi kuzuilika na mamlaka za ndani.

Leo yanaweza kuwa upande wenu kesho yakawa yana pambana nanyi huku maafa makubwa yakiwafikia wananchi wasio na hatia kutokana na uzembe na upuuzi wenu.

Nawakumbusha tena kila mwaka mnazalisha vijana wa JKT walio na mafunzo na kuwarudisha mtaani huku mkiendelea kuchekea makundi ya kipuuzi kama haya.

Nanawa mikono kama Pilato.
Hawajali hilo hawa wahuni...
 
Inaogopesha lakini ndio wenye bunduki sisi makapuku silaha yetu ni kelele tu. Mungu atusaidie!
 
Back
Top Bottom