Operation Sangara: Chadema yajipanga Upya


Watumie akili kidogo wataipata wapi, watu wako kama ma-robot hawafikiri kabisa, na wakifikiri ni labored thinking. Maradhi yetu ndiyo haya na hatutaendelea hata siku moja. Nadhani chuki iliyopo inasababishwa na dissatisfaction. Kila ****** akae chini ajifikirie, atakuta hayuko satisfied na maisha yake ndiyo sababu ya chuki hizi. Mtakufa kwa kihoro.
 
....watu kama hawa ndio wananipa sababu ya kuendelea kusupport separation of church/synagouge/mosque and state,acha waendelee na makelele yao lakini hayana nafasi katika sheria zetu!
 

My friend, things are not as simple as you see or say them. We know viongozi wa dini wana'influence' kubwa sana kwa wafuasi wao wanaowahubiria almost kila siku. Na kinachosemwa hapa si kingine bali ni nguvu ya hiyo influence hata kama wewe ni tofauti. Lakini ujue you are not everybody.

Mara nyingi when certain things are said, some people try to be very apologetic about them na ndio maana badala ya kuwa na umoja fulani katika kupinga maovu tunatofautiana but actually it's just a denial of what is taking place. Take time to observe what's happening! Na kwa kawaida watu ambao mara nyingi wanakuwa misled siyo wewe na mimi ila waumini wa kawaida.

Mtu akihubiriwa kuwa chama fulani kinapinga dini yake mtu huyo bila hata kufanya utafiti wowote ataamini. Na hofu yetu ndiyo hiyo, kwamba hao viongozi wanaojiingiza katika siasa kwa style wanayoifanya kweli wana nia njema au wanatumiwa na wansiasa wenyewe?

Kuna mtu fulani nilikuwa naongea naye leo na alisema hivi: In Tanzania we're not doing politics; it's just something else. Politics is done in Europe. Ukifikiria kiundani utaona ni kweli. Tunachokifanya ni fujo tu siyo siasa kwani siasa huwa ina mweleko fulani.

Na baadhi ya viongozi wetu wa dini nao hawana mwelekeo. Wanaangalia maslahi fulani tu. Mtu akichukia kufichuliwa kwa maovu kama ufisadi halafu uniambie huyo ni kiongozi wa dini nitacheka sana. Ni mchezo mchafu tu!
Tutaendelea kutetea maovu hata lini? If the sufferings of others do not touch me, then I've no reason to believe or claim to believe.
 

Chinkala,

..ume-quote posting yangu halafu ukatoa majibu hayo hapo juu.

..nimeripoti tu kile kilichosemwa na BBC Swahili Service. sijachukua upande wowote ule.

..nadhani cha msingi hapa ni tusubiri tu kampeni za Bahakita vs Chadema.

NB:

..swali la msingi hapa ni kuwajua hao kina Bahakita.

..pia uwezo wa kufanya kampeni nchi nzima wanatoa/watautoa wapi?

..wafadhili na sympathizer wa Bahakita ni kina nani?

..je, wananchi tunakubaliana na madai ya Bahakita?
 
Mimi binafsi huwa naikwepa sana mijadala yenye milengo ya kidini lakini wakati mwingine inanilazimu niichangie kutokana na michango ya baadhi ya watu kuwa imejaa ujinga, uongo, ugoigoi, upumbavu, chuki, dharau, uzandiki na ubaguzi wa hali ya juu. Nadhani tukitumia majukwaa kama haya kuelemishana kwa dhati, siku zote tutafikia malengo yetu katika majadiliano ya kidini au mambo mbalimbali katika jamii zetu, lakini pale baadhi ya watu wanapojiona ni bora kuliko wengine na kutumia lugha za matusi na kejeli kwa wengine basi siku zote kutakuwa na migongano na mifarakano.
 
Inapokuja kwenye hizi dini tulizoletewa na kuzirithi, utagundua kuwa kuna prejudice...Kwamba dini yangu ni bora zaidi ama iko sahihi zaidi nk. Hilo siyo siri...Kila upande una vijimaneno flani hivi vya kuupiga vijembe upande mwingine ama kuukosoa....Hayakuanza leo na certainly hayatakwisha leo.

Tatizo ni sisi warithi..Nimegunduwa matatizo mengi sana...Hata hivyo hili la waislam naona limeongezeka zaidi kwasababu wale wenye msimamo mkali walishafanikiwa kuwa ndiyo wenye influence zaidi kutokana na misuguano mingi ya jamii za waarabu dhidi ya wazungu na wayahudi hususan Palestina....Ku embed dini kwenye matatizo ya kijamii ambayo dini siyo tatizo kuu bali mojawapo ya matatizo.

Waafrika tulipata matatizo ambayo waarabu leo wanayapata lakini sisi hatukusema dini,ila dini ilikuwa mojawapo kati ya matatizo kedekede yaliyoletwa na watawala wa kikoloni kwasababu waafrika si walikuwa na dini zao? Utamaduni wa kuabudu sisi waafrika tulikuwa nao...Kwamba ibada zetu zilikuwa right ama la,huo ni mjadala mwingine. Sisi tulisema ubaguzi wa rangi nk...Lakini kwenye kubaguliwa kwetu,dini na tamaduni nyinginezo nyingi tu ziliathirika....Na hivyo basi kufanya tatizo hilo kuwa mainly ukoloni ambapo ndani kuna watu hao wenye rangi,dini na tamaduni za tofauti.

Lakini kwasababu mwarabu na mzungu walitumia dini kwenye kila mkakati wao wa ku colonize,sasa wamegeukiana wao kwa wao kwani ndio tumegunduwa kuwa kumbe walikuwa na nia ya kututawala milele...Kwasababu sasa huu si utumwa mamboleo? Ndio maana didni na serikali kwenye jumuiya za kistaarabu zinatofautishwa.

Matatizo yaliyokuwa yakitupiganisha waafrika kabla hata hawajaja hawa waarabu na wazungu mainly ilikuwa ardhi..Certainly bado ni tatizo kubwa lenye migogoro Afrika..Sasa je bado tunaka kuendeleza matatizo yenye migawanyo?
Ni wazi kuwa waarabu wenye msimamo mkali wamepata nafasi ndani ya dini ya waislam na ni kwasababu wamefanikiwa kujumlisha siasa na dini na kufanikiwa.

Tanzania ni taifa lenye mfano wa kuingwa lakini sasa kama kuna wenzetu ambao wanaweka dini kabla ya utaifa...Then tunakoeleka sijui.
Huwezi kuwaiga wapalestina lkwa kigezo cha uislam kwasabau wao kwenye nchi yao ni waislam majority na pia wanaweza wakawa wanataka taifa la kiislam kama Iran....Kwa hiyo mnaweza kuona kuwa cause za wapalestina na zetu sisi ni the same only kwamba wao ni waarabau...Ila hatuwezi kusema kuwa ni matatizo ya waislam,tusitafsiri vibaya sisi waafrika tunatumika sana kama wajinga.

Watanzani especially ndugu zangu waislam muelewe kuwa dini na siasa ni tofauti na serikali yetu kamwe haiwezi kuwa na dini kama waislam wengi wanavyopendelea kuwa na serikali za kiislam....Vugu vugu la Palestina lisiwe kigezo kwani wao ni utamaduni wao kwa kila namna na dini ni mojawapo..Tukipigania uhuru wa Tanzania hatupiganii uhuru wa muislam ama mkristo...NI UHURU WA MTANZANIA.

Kwa upande wa wakristo nao ni the same...Isipokuwa wao wameshindwa ku harbor feelings za chuki kwasababu wao wamekuwa upande unaonufaika kisiasa especially Afrika na kwingineko magharibi hivyo kutokujali sana kuhusu anachofanya mwenzake muislam...Na tatizo hilo ambalo wengi wetu hawalizungumzii ni mara baada ya vita ya pili ya dunia...Muarabu/Muislam kwa ujumla alikuwa upande wa Ujerumani na Hitler na ndio maana mara baada ya vita hiyo kuisha mwarabu alikuwa ni kama subsidiary ya tatizo kuu na hivyo kufanya vugu vugu la mvutano huu kuwa kubwa zaidi...Vugu vugu ambalo certainly liliwarudisha wakristo kwenye animosity majority yao mara baada ya sept 11 hapa USA.

Ni vyema basi tukaiangalia historia ya dunia kama watanzania na si kama waislam ama wakristo nk...Hilo litatusaidia kuanza kujenga uzalendo na mapenzi ya kweli kwa Taifa kwa kuwa na uelewa kuwa dini yako hiyo iwe ni kigezo tu cha kukufanya uwe mtanzania mkamilifu katika vita hii ya kubadili mwelekeo wa dunia hii kwani ni muhimu sana kwa vizazi vyetu vijavyo na hii ni kama tunayajali...Kama tunajali tutajiuliza.
 
Last edited:
Inasikitisha sana kuona watu hapa mlivyorukia habari hii na kuijaza hewa chafu kiasi kwamba nafikiria kuwa Udini upo kati yetu ila hatutaki kuamini hivyo..

Nimesoma hoja nyingi humu zinaonyesha wazi kwamba sisi wenyewe ni WADINI tena wala sii kidogo.. kwa sababu maneno ya mtu kama Mwaipopo ambaye ni Mdini yanapojibiwa kwa Udini basi bila shaka sisi wenyewe Wadini..Kifupi mnamfukuza kichaa aliyechukua nguo zenu, mkiwa uchi..

Mara zote najaribu sana kuwafahamisha ndugu zangu Wakristu wapate kuelewa Uislaam kwani Uislaam sii jina la mtu, au kwa kuzaliwa, ukoo nasaba au kuamini kitabu bila elimu ya kufanhamu yaliyomo ndani..Uislaam ni zaidi ya hayo yote!..

Nimesoma hotuba ya huyu Mwaipopo kwanza hawakilishi waislaam isipokjkuwa ni mtu ndani ya taasisi fulani ya habari iliyosajiriwa kwa kutumia jina la Uislaam.. wapo watu kama hawa madhehebu yote hata ndani ya Ukristu hivyo ni muhimu kwetu kuchambua pumba toka ktk mchele..

Iweje leo watu humu muanze ku address kila kitu kuwa Waislaam hivi ama vile kama nyie wenyewe hamna Udini?.. Aliyesema huyo Mwaipopo nani hasa ktk Usislaam?.. He is nobody sawa na Mwanakijiji na KLH News..Huwezi kuhukumu wana blog wote Tanzania kwa sababu Mwanakijiji kasema kitu kinachgomsumbua yeye hata kama kawaomba wanablog wenzake pamoja na kwamba naamini Ujinga alotumia Mwaipopo hawezi kuutumia Mwanakijiji..

Kumbukeni jamani kulikuwepo na mada humu zinazohusu Chadema na Uchagga!.. hawakuwa waislaam waliozungumza hayo na tuliweza kuweka meza sawa tukajadili bila kufikiria nje ya kabila la mtoa hoja. Tulizungumzia pia CUF na Udini na sidhani kama Waislaam waliona vibaya isipokuwa kujiuliza kama kweli CUF ni chama kinachotumia Udini.. As a Muslim, it never bother me kusikia CUF ni chama cha Waislaam wala kufikiria aliyetoa hoja hiyo ni mdini zaidi ya mimi kutafuta majibu kutokana na ukweli..

Yes Mwaipopo ametoka nje ya dini na kuanza kuhubiri siasa akitumia dini lakini tunapoanza kuwavaa Waislaam wote kwa sababu ya Mwaipopo au hilo jina Sheikh tunaonyesha wazi kwamba sisi wenyewe ni Wadini..Kwa nini tusimjibu kwa kumpa mifano bora inayotokana na Operation Sangara! Kwa nini tusijibu maswali mbuzi aliyoyaweka badala yake tunashikwa hasira as if ni kweli Chadema ni chama cha Kikristu..

Binafsi sioni sababu ya kuumia roho ikiwa madai ya Mwaipopo ni ya Uongo..Na hakika Uongo unapojibiwa kama hivi nina hakika wapo watu wantaanza kuamini kwamba kweli Chadema ni chama cha Kikristu..kwa sababu waliojibu kwa jazba ni Wakristu na wameonyesha wazi kutetea Ukristu ndani ya chama badala ya kutenganisha Chadema na Ukristu au Uchagga.. Unapohoiji CUF au CCM kuwa ni vyama vya dini gani ina maana hu deny Chadema kuwa chama cha Kikristu!.. Jamani tuwe makini ktk hili sio wote wanaosoma JF wana akili kama zenu..

Trust me, uvumi mdogo kama huu pamoja na kwamba mnauchukulia light unaweza kabisa kui cost Chadema vibaya sana. Tuwe makini kwa majibu yetu na kibaya zaidi ni kwamba karibu wote waliozungumza humu hakuna hata mmoja anayewakilisha chama Chadema. Lakini kwa msomaji ataelewa kuwa mnawakilisha Chadema na Ukristu kama mlivyomwelewa Mwaipopo..
Je, kuna mtu humu kweli anawakilisha mawazo ya Chadema kuhusiana na Ukristu au Uchagga, sidhani!..sasa iweje taabu kwenu kuelewa kwamba huyo Mwaipopo ni sawa na nyie wenye kukereka na na udini mlouficha rohoni mwenu..
 

WAUMINI wa dini ya kiislam wamepinga oparesheni sangara inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuws chama hicho na operesheni hiyo, haina manufaa kwa uisalam kwa kuwa imejaa ukabila, ubinafisi na udini


Na CUF ni chama cha dini gani?
 
Miofarakano na migongano ndio huleta maendeleo......usiogope sana mkuu.....wewe gonga kwa hoja utasikika..
 
Genenis,
Na CUF ni chama cha dini gani?
Mkuu wangu siasa za Bongo huziwezi kabisa..
Kwa faida ya watu wote humu nitawakumbusha kitu kimoja..

Mwaka 2002 au 2003 kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005 kuna Sheikh Mmoja sikumbuki jina lake alivumisha habari kuwa Marehemu Prof. Malima, Sheikh Kassim na chama cha CUF wamefanya mkutano wa siri kuhusiana na Ugaidi (After 9/11) na kuwaambiwa wananchi kuwa CUF ni chama cha kiislaam kilichojaa Udini..

Nilipinga hoja hiyo hapa hapa kijiweni kama sio Jamboforum basi itakuwa Bcstimes na kuwafahamisha kwamba mwaka 2000 au 01 ambao ulitajwa kuwa ndio mazungumzo hayo yalifanyika Sheikh Kassim alikuwa hayupo hapa duniani!..

Maneno yangu hayakuaminika, uvumi huo uliwabeba wengi wenu mkaingia ktk wagon hilo, kiasi kwamba leo hii bado mnaamini kabisa kuwa CUF ni chama cha Kiislaam.. na sababu zote zilizotumika ni kutokana na Uongozi wake, wafuasi wake wakitumia Uuwiano kama inavyofanyika sasa hivi kwa Chadema..

Uchaguzi wa mwaka 2005 CUF walitoka watupu na hakuna sababu zaidi ya mbegu hasidi zilizopandikizwa na zikapokelewa na wananchi...Msipochakaza vichwa vyenu kutafuta ukweli na kuuweka wazi tena mapema sana ndugu zangu Mnatzidi kukiua chama Chadema. Majibu ya kihuni hata siku moja hayasaidii..Ukweli mdogo niliouweka mimi hapa JF haukuweza kusambaa Tanzania nzima hivyo wapiga kura walikitenga chama CUF kwa Udini wake meaning Watzania wengi hawapendi kabisa Udini iwe Objective au laa kila mtu hutazama nani adui wa haki.
 

Zero correlation..
 
MtindiowaUbongo,
It's all good...I expected that from U...
 
Mwenzako mwenye utindio wa ubongo kama wewe ameshakubali kuwa yeye ni Goigoi mwenye fikra potofu zenye utandu wa ujinga, nawe badilisha nickname yako na ujiite kama yeye kwa sababu sioni tofauti kati yenu.


Goigoi ni wewe unayeshindwa kujibu hoja za watu na kuanza kushambulia hata pen-names.. this shows how perfect you belong to the group ya walewale.
 
Mkandara,YNIM,Mtindio-wa-Ubongo,Geeque,chinkala,Max...

..hivi haiwezekani kutunziana heshima walau kidogo?

..nadhani hawa kina Mwaipopo,Msopa, na wenzao, wanachezea dini.

..hawa ni tofauti na Mtikila kwasababu mwenzao at least, at least, ameanzisha chama cha siasa-DP.

..siyo kitu cha ajabu kwa mashekhe, mapadri, na wachungaji kushiriki siasa. naomba niwakumbushe wafuatao: Sheikh Idiris Abdul Wakil, Padri Supa--Mbunge wa Dodoma, Padri Yohana Misigalo--Mbunge Tabora, Sheikh Juma Mikidadi -- Mbunge wa Kilwa.

..the common denominator ni kwamba wote walijiunga na vyama vya siasa.

..wanachojaribu kufanya hawa kina Mwaipopo ni kitu hatari sana ktk mazingira ya dunia ya leo. tuliikwepa vita kati ya ukomunisti vs ubepari, sasa tusije tukajitumbukiza ktk vita ya mahafidhina wa Kikristo vs mahafidhina wa Kiislamu.

..hata kama wana madai ya kisiasa sidhani kama ni busara kuwavumilia ukizangatia kwamba wanataka kuyawasilisha kwa kutumia chombo kilichoanzishwa kwa misingi ya dini.

..kwa kifupi naomba Dini zote mbili zisikubali kuchezewa, na kutumbukizwa ktk malumbano ya kisiasa. kama kuna madai ya Kisiasa basi Mashekhe,Mapadri,Wachungaji, wa-LOBBY kwa waheshimiwa Wabunge.

NB:

..watoa maoni wengi ktk mtandao, ambao wanaonekana kuwa Waislamu, wamekuwa wakiikandia na kuikana Bakwata kwamba haiwakilishi Waislamu.

..labda kuna yeyote anayeweza kutuelekeza chombo chochote kile ambacho kikitoa tamko basi tunapaswa kuwachukulia seriously kwamba wanazungumza kwa niaba ya majority ya Waislamu wa Tanzania.

..je, kuna Sheikh,Imamu,...ambaye akitoa tamko hilo tunaweza kuchukulia kwamba linaungwa mkono na majority ya Waislamu wa Tanzania?
 
Divide Et Emperor​
The Romans were able to rule the world for a long time by using the principle of Divide Et Emperor (Divide and Rule). It seems to me that CCM is trying to use the same principle: If you mange to divide Tanzanians then you can lord it over them.

I am aware that not every one will see the hand of CCM in this matter, but it is my considered opinion that this latest outburst bears the hallmark of campaign maneuver by that den of vipers.

I think they are starting with religious divisions. If that does not work then they will exploit tribal affiliations.

It's a lowly technique, but when the majority of the people have hardly seen the inside of a classroom then it just might work.

CUF might also be pursuing this line of action. They have always tried to rely on underground mobilization through the mosques. CUF was born out of UDINI.

CCM has tried to stay away from religious and tribal divisions in the past. I suppose that it is a measure of desperation that even they are now turning to UDINI.
 
Wengi wetu tunafanya kosa la kufananisha mfumo wa uislamu na ule wa kikristo.

Wa-Sunni hawana uongozi wa hierarchy ( Papa, askofu, padri, shemasi, muumini n.k). Kila muislamu anatarajiwa kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Mmungu wake. Kwa hali hiyo hakuna kiongozi wa kumshurutisha (in theory) katika imani yake. Mashehe, maimamu ni walimu tu na si gate keepers. Katika hawa hakuna aliye juu ya mwingine. Ndiyo maana kila msikiti uko independent na shehe wa ule msikiti anawajibika kwa waumini wake. Tatizo linakuja pale ambapo baadhi ya hawa walimu kujichukulia madaraka ya uongozi na kutaka kuusemea umma wa kiislamu. Hii inasaidiwa sana na tabia ya wengi wa waumini wao kutokuwa assertive zaidi na kukaa kimya wakati hawa wajanja wanafanya hivyo kwa imani potofu kuwa hawawezi kumpinga muislamu mwenzao. Hawa wanachanganya uislamu na muislamu.

Waislamu wa-Shia ni tofauti. Wao wana uongozi unaolingana lingana na ule wa wamisheni. Ndiyo maana kwa wao, wakina Ayatollah wana sauti na mamlaka makubwa. Lakini hawa ni wachache sana nyumbani kwetu na wengi wao ni wale wenye asili ya Asia ( waithnasheri, bohora, waismailia n.k.) wa hiyo hawana umuhimu katika mada hii.

Sisi wamisheni ni tofauti. Sisi tuna maboss ambao tumewapa mandate ya kutuwakilisha. Kwa hali hiyo maaskofu wetu wana haki ya kutusemea ili mradi wanafanya hivyo kwa madhehebu yao na si totality ya ukristu. Tofauti nyingine kubwa ni kuwa wakristu hawachelei kumpinga kiongozi wao wanapoona amekosea. Wakristu mara nyingi hawana ile hisia ya kuwa ni lazima wamtetee mkristu mwenzao hata pale anapokosea. Hii pengine imetokana na wao kuwa na access na vitabu na theology inayoongoza dini yao. Kwa waislamu access hiyo ni limited maana ni wachache wanaoelewa kiarabu.

Baada ya kusema hayo yote, kinachojitokeza hapa ni mada nzima kutekwa na hao wanaojiona kuwa ni watetezi wakuu wa imani zao. Kwa vile wanaona hii ni struggle ya hadi kufa basi hawasiti kutumia silaha za kebehi na matusi. Kwa kufanya hivyo wanapotosha muelekeo wa mjadala wenyewe na kuukita kwenye chuki ambayo mfuasi yeyote makini wa imani hizo mbili ange-avoid. Mnatuangusha wote, nyinyi mnaojifanya kuwa watetezi wetu!

Amandla......
 
wakuu nadhani watanzania walio wengi wako kwenye matatizo makubwa ya kuwakilisha ujumbe
1. kama shehe mwaipopo katumiwa kwa nini awazungumzie waislamu wote baada ya kikundi chake anachokiongoza
2. pili nadhani hii taaluma ya uandishi sasa imekosa mwelekeo kabisa,bwana Nyagaro na Bi Zaina wanadiriki kuandika Waislamu waipinga operation sangara na kumbe mpingaji ni Mwaipopo na genge lake,Hivi hawa waandishi kweli Hawajuhi msemaji wa waislamu Tanzania ni nani? (BAKWATA)
AU NAO NI CHAMA KIMOJA NA SHEHE MWAIPOPO?

OLE WAO WAANDISHI NA MAFISADI
 
Waislam 35% ya population ya Tanzania, wakristo 30%, imani za kienyeji 35%; sasa ukiigawa nchi kwa waislam na wakristo wale wengine inakuwaje? Acha uzushi!

Mkuu saikosisi heshima mbele.
Naomba kutofautiana na wewe katika hizo statistics zako sijui umepata wapi hizo data maana hata sensa iliyofanyika Tanzania hakuna kipengele cha dini.
Mkuu tafadhali sana si vizuri kuleta habari za kwenye mabao hapa jamvini.
 
Tumezipandisha chati DINI zetu kupita kiasi. Baadhi yetu tumeziweka DINI hizi kama MAMA. Inafika mahala mtu anaona kuwa na RAIS wa nchi wa DINI/DHEHEBU lake ni muhimu sana. UJINGA mtupu. DINI imsaidie mtu kuabudu/kutambika anavyoona inamfaa na si zaidi ya hapo. Kwangu mimi DINI ni kama MKE. Naweza kuibadili, kuiacha, kuitelekeza, kuipenda na hata kuichukia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…