Ongezeko la tozo za miamala ya simu na bei ya mafuta ni uthibitisho wa ubutu wa Bunge

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,488
3,263
Kulingana na 'statistics on mobile telecom services in africa- global market', m-pesa, tigo-pesa, na airtel money, jan- mar 2020 zilifanya miamala 93.8bilion sawa na miamala 375.2 bilioni kwa mwaka. Miamala ilihusisha kulipia bills, uhamishaju binafsi wa pesa, kutuma na kutoa pesa. Kwa tozo la sh 30 kwa mwamala serikali ingepata sh 11.25 trn.

Kumbuka kampuni hizi zinaingiza pesa nyingi pia kupitia kuangalia salio, miito ya milio ya simu nk. Kwenye global economic website, mwaka 2018 wastani wa matumizi ya mafuta Tanzania ilikuwa mapipa 18000 kwa siku(pipa la mafuta lina lita 119.24). Huu ni wastani wa 214.6m litres kwa siku, sawa na wastani wa 78. 329 bilioni litres kwa mwaka.

Kwa tozo la sh 30 serikali ingepata sh 2. 35 trn kwa mwaka. Kuna misamaha ya kodi ya mafuta kwa migodi, lakini idadi ya magari 2021 ni kubwa kuliko ya 2018.

Wabunge wetu hawana muda wa kupitia yaliomo kwenye vitabu vya budget, na hata wenye taaluma wamegeukia usawa wa msukuma na kibajaji. Ni Bunge ambalo likifananishwa na rubber stamp, spika anachukia.
 
Back
Top Bottom