SoC01 Ongezeko kubwa la Wasiopiga Kura katika Uchaguzi Mkuu. Nini kifanyike?

Stories of Change - 2021 Competition

ROJA MIRO

Member
Jul 19, 2021
52
56
Haki ya mtu kupiga kura imetajwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwkaa 1997 ambapo sheria ya mwaka 1984 namba 15 ibara ya 6 na sheria ya mwaka 2000 namba 3 ibara ya 4 inatamka wazi kwamba,Kila raia wa Tanzania aliyetimiza miaka 18 anayo haki ya kupiga kura katika uchauzi unaofanywa Tanzania na haki hii itatumiwa kwa kufuata masharti ya ibara ndogo ya 2 pamoja na masharti mengineyo ya katiba hii na sheria inayotumika Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Taifa ya uchaguzi mwaka 2015 idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura ilikuwa ni 23161440 kati yao ambao hawakupiga kura ilikuwa ni watu 7565330 idadi hii ni sawa na 32.6 hivyo ni sawa na kusema kila kwenye watu 100 watu 32 hakupiga kura kwa mwaka 2015.

Kwa uchaguzi wa mwaka 2020, jumla ya watu 29,754,699 walijiandikisha ambapo watu ambao hawakupiga kura walikuwa ni 14,662,749 ambapo ni sawa na 49.2% na hili ni ongezeko la 16.6% ukilinganisha na 32.6 ambao hawakupiga kura mwaka 2015.Wakati watu 32 kati ya 100 hawakupiga kwa mwaka 2015 kwa mwaka 2020 watu 49 kati ya 100 hawakupiga kura ikiwa ni ongezeko la watu 17 kati ya 100 kwa kipindi cha miaka 5.

Kila anayejijua hakupiga kura mwaka 2015 anakuwa ni miongoni mwa watu milioni saba,ambao hawakupiga kura katika uchaguzi mkuu, idadi hiyo ya watu ni wastani wa watu 614 kila kijiji,kutokana na idadi ya vijiji 12319 na wastani watu 117 kila kitongoji kulingana na idadi ya vitongoji 64,384 vilivyopo nchini Tanzania.

Wakati hayo yakijiri kwa mwaka 2015, mwaka 2020 watu 14,662,749 ambao hawakupiga kura katika uchaguzi mkuu ambapo ni sawa na wastani watu 1,190 kwa kila Kijiji, na idadi hiyo ni ongezeko la watu 576 ukilinganisha na wastani wa watu 614 kwa kila kijiji kwa mwaka mwaka 2015.

Tanzania ikiwa na vitongoji 64,384 wastani wa watu 227 hawakupiga kura kwa kila kitongoji kwa mwaka 2020, na hili ni ongezeko la wastani watu 110 ukilinganisha na watu 117 kwa wastani wa mwaka 2015 ambapo watu zaidi ya million 7 hawakupiga mwaka huo.

Matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 yanaonesha idadi ya wanafamilia kwenye kila kaya nchini Tanzania ni 4.5 hivyo ni wastani wa watu 5 kwa kila kaya, na endapo utagawa kwa idadi ya watu millioni 7,565,330 wasiopiga kura kwa mwaka 2015 ni wastani wa kaya 2,340,689 hazijashiriki uchaguzi nazo ni sawa na 24.9% ukilinganisha na idadi ya kaya 9362758 zilizopo.

Idadi hiyo ya wanakaya kwa sensa ya mwaka 2012, ukigawa kwa wasiopiga kura kwa mwaka 2020 ambao ni watu million 14662749 unapata wastani wa kaya 2,932,549 ikiwa ni wastani wa ongezeko la kaya 591,860 kwa kipindi cha miaka 5 na sawa na kaya 118,372 kwa kila mwaka mmoja zilijitoa kwenye mpango wa kushiriki kupiga kura.

Wakati wastani wa 24.9 % ya kaya hazijashiriki uchaguzi kwa mwaka 2015 kwa mwaka huu 2020 ni 31.3 hivyo ikiwa ni ongezeko la 6.4% kwa kila kaya kutoka uchaguzi wa mwaka 2015 hadi wa mwaka 2020.

Kwa mwaka 2015 asasi za kiraia zipatazo 447 zilipatiwa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura kwa uchaguzi kuu tu ambapo ukigawa kwa jumla ya wilaya 169 zilizopo nchini ni wastani wa kila wilaya ilikuwa na asasi 2 za kutoa elimu ya mpiga kura ingawa kwa mwaka 2020 jumla ya asasi 252 zilipatiwa vibali vya kutoa elimu ya mpiga hivyo ukigawa kwa wilaya 169 unapata wastani 1.4 ambapo ni sawa na kusema ni wastani wa asasi moja kila ambapo ni pungufu wa wastani wa asasi 2 kila wilaya kwa idadi ya asasi zilizopewa kibali cha elimu ya mpiga kura kwa mwaka 2015.

Kwa watu million 7,565,330 ambao hawakupiga kura kwa mwaka 2015 ni sawa na wastani wa vijiji 756 kutokana na taratibu za uongozi wa serikali za mitaa ambazo zinataka Kijiji kisizidi watu,10,000 na hii ni sawa 6.14% ukilinganisha na idadi ya vijiji 12319 vilivyopo nchini Tanzania.

Na kwa idadi ya watu 14662749 wasiopiga kura kwa mwaka 2020 ni wastani wa vijiji 1466 kwa utaratibu huo huo wa uongozi wa serikali za mitaa ambazo zinataka Kijiji kisizidi watu,10,000 na wastani wa idadi hii ya vijiji ni sawa na 11.9% ukilinganisha na idadi ya vijiji 12319 vilivyopo nchini Tanzania kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,na hili ni ongezeko la 5.76.

NB:Wastani wa Vijiji 1466 wa mwaka 2020 ni ongezeko la wastani wa vijiji 710 ukilinganisha na wastani wa vijiji 756 kwa wastani wa mwaka 2015.

NINI KIFANYIKE?
Nashauri serikali ifanye utafiti kugundua ni sababu gani ambazo zinapelekea watu wasipige kura ili kuzitatua,na pia napendekeza mada zinazohusu umuhimu wa uchaguzi ziingizwe kwa upana kwenye somo la uraia kuanzia ngazi za chini za elimu ili kuwajenga wanafunzi wakiwa ngazi za chini za elimu,kingine vuiongozi wanaochaguliwa wawajibike ipasavyo kwa wanachi ili isipelekee watu wakahisi labda hakuna uhusiano wa moja kwa moja na maisha yao uchaguzi kama kampeni mbalimbali za uchaguzi zilizvyojinadi,mfano,MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA,HAPA KAZI TU nk.

Ukisoma makala yangu kwa umakini utaona uchache wa asasi zilizopewa nafasi ya kutoa elimu kwa mpiga kura kwa mwaka 2020 zilikuwa chache ukilinganisha na zile za mwaka 2015,hivyo nashauri serikali iwekeze nguvu huko,na pia isikilize manung’uniko ya wananchi kwani baadhi yao huamini kwamba mbali na kupiga kura ila wanaowachagua hawashindi n ahata wakishindwa hawawezi kutangazwa.
 
LAKINI JAMANI HUMU WOTE SI WPAIGA KURA MNAFIKIRI KITU GANI KINAWAFANYA WATU WASIPIE KURA? KARIBUNI KWA MAONI NA KURA YAKO NI MUHIMU.
 
Nikitulia nitatoa majibu kwanini watu hawapigi kura kwa wingi na nini kifanyike.
 
Kwanini watu hawajitokezi kupiga kwa wingi kupiga kura ?

Kutokana na kuwa mfuatiliaji mzuri wa siasa za nchi hii tangu 2000 nitatoa sababu ninazoona mimi zinachangia wananchi kupungua sana kwenye kila uchaguzi kupiga kura nitatoa sababu za jumla kwa chaguzi zote na sababu mahsusi kulingana na uchaguzi husika hasa katika chaguzi za 2015 na 2020.
Sababu za Jumla.
1. Wananchi kushindwa kuhusianisha kura zao na maendeleo maana yake wananchi wanafanya chaguzi lakini wanaowachagua hawafikii malengo ya wananchi ikiwemo ahadi zao nikupe mfano mdogo jimbo la Ismani lina mbunge toka 1995 na miaka yote hiyo mbunge huwa ana ahidi maji lakini hajawahi kutekeleza ahadi hiyo. Hali kama hii iko sehemu nyingi za nchi kila baada ya miaka mitano wanapelekewa hoja zile zile hii inaondoa hamasa ya wananchi kwenda kuchagua watu wale wale kwa hoja zile zile miaka nenda rudi.

2. Uchaguzi kutokuwa Huru na haki wananchi wanamchagua John anatangazwa Bakari hii hali huwachukiza wananchi na kuona chaguzi hazina maana tena bali ni kwajili ya kuwapotezea muda kwa lugha rahisi chaguzi zetu zimekosa Credibility, fairness and freedom. Mfano uchaguzi wa 2019 wa serikali za mitaa ilikuwa kielelezo tosha kuwa uchaguzi kwa wananchi hauna maana ikiwemo na uchaguzi mkuu wa 2020.

3. Mfumo wa uchaguzi mbovu, mfumo wetu unataka mtu apige kura physically mahali alipojiandikishia na kwa kutumia kitambulisho rasmi cha mpiga kura tu hali hii inamapungufu kadhaa.
1. Wananchi wote hawawezi kupata wasaa wa kujiandikisha katika vituo vya kupigia kura. Kwa mfano mimi nilishindwa kujiandikisha 2000 kwa sababu nilikuwa nje ya mkoa wangu nilitaka kupigia kura, nilipojiandikisha 2005 sikuweza kupiga kura kwa sababu nilikuwa nje ya mkoa niliojiandikisha, 2010 sikuweza kupiga kura kwa sababu nilikuwa nje ya mkoa niliojiandikisha, 2015 sikuweza kufika kwenye kituo cha kupigia kura kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, mifano hii inafafanua pia hoja yangu ya pili hapa
2. Watakaojiandikisha siyo wote watakuwa sehemu ya kituo cha kupigia kura wakati huo, hii maana yake kuna kundi kubwa sana hawapigi kura kwa sababu ya kushindwa kufikia vituo vya kupigia kura tu kwa sababu mbalimbali.
3. Mifumo ya uhakiki wa daftari la wapiga kura kuwa na dosari nyingi ikiwemo idadi ya wapiga kura ya kutilia mashaka.
Mathalani uchaguzi wa 2020 waliojiandikisha walikuwa 29+ Milions wakati huo huo idadi ya watanzania mpaka siku ya uchaguzi walikuwa 50+ Millions ndiyo kusema karibia nusu ya watanzania wote walijiandikisha kupiga wakati huo huo pia takwimu zinaonyesha zaidi ya nusu ya watanzania wako chini ya miaka 18 hii maana yake ni kuwa Huenda takwimu za wapiga kura 2020 hazikuwa sawa in all angles of reasonableness. Hoja hii inagusa credibility ya uchaguzi ambayo hata wananchi wanahoja za msingi kutotokea vituoni.
4. Dola kujiingiza moja kwa moja kwenye zoezi la uchaguzi hasa jeshi la polisi na kufanya uchaguzi kuonekana kama threat to national peace hivyo wananchi wengi huwa na hofu juu ya usalama wao wakati wa uchaguzi.

5. Tume kushindwa kutumia teknolojia salama katika uchaguzi ili kila mtanzania aweze kushiriki uchaguzi bila kuathiri shughuli zao za kujipatia kipato.
6. Elimu ya mpiga kura imekuwa ikipungua kutoka uchaguzi mmoja kwenda uchaguzi mwingine, uchaguzi wa 2020 tume ilitunga kanuni zilizozuia vyama vya siasa kutoa elimu ya mpiga kura ikiwemo kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura.
Haya ni madhaifu yaliyopo kwenye mfumo wetu wa uchaguzi.

4. Wagombea wasio na ushawishi kupewa nafasi kugombea na wenye ushawishi kuenguliwa kinyemela. Mfano mzuri katika hili ni uchaguzi wa 2015 pamoja kuwa na hamasa kubwa machoni pa wengi lakini ulikuwa ni uchaguzi usio na chaguo kwa wananchi ndiyo maana turnouts ya wananchi haikuwa ya kuridhisha sana pamoja kubwa kwa wananchi.

5. Mchakato wa uchaguzi kukosa huru na wa haki kwa wadau wote wa uchaguzi.

Hoja Mahsusi kwa uchaguzi wa 2020.
Uchaguzi wa 2020 ndiyo uchaguzi wa hovyo kuwahi kuushuhudia ukanda wa Afrika Mashariki toka karne ya 21 imeanza ukifuatiwa na uchaguzi wa kenya wa 2007.

Kwanini uchaguzi huu idadi ya wapiga kura ilikuwa ndogo sana.

1. Mchakato wa uchaguzi haukuwa huru na wa haki kwa kila kitu mchakato ulianza kuharibika kwenye zoezi la kuandikisha wapiga kura elimu ya mpiga kura haikutolewa vya kutosha na zoezi liliendeshwa kwa muda mfupi sana, sababu inaongeza mashaka juu ya idadi ya wapiga kura walioandikishwa.

2. Wagombea wengi walienguliwa hasa wa udiwani ambako wananchi ndiyo huwa wanamatazamio makubwa zaidi ya kupata viongozi wanaowataka tofauti na ubunge hivyo wananchi walikatishwa tamaa na mchakato wenyewe kabla ya election day.

3. Matukio mengi ya uhalifu yaliyohusisha kuteka wagombea, kunyang'anya fomu ,kuharibu kampeni za vyama vingine hii ilichangia sana wafuasi wa vyama vingine kutokwenda kupiga kura kwa sababu ya hofu ya usalama wao.

4. Zoezi la uchaguzi kuwa na mapungufu mengi ikiwemo majina ya wapiga kura kutoonekana kwenye vituo vya kupigia kura.

5. Kauli za serikali na wagombea wake kuwa hata mkichagua upinzani hawatatangazwa hivyo wananchi hawakuona sababu za kwenda kupiga kura ambayo haitahesabiwa.

Nimalizie kwa Swali je idadi ya wapiga kura iliyopo kwenye daftari la wapiga kura ni halisi ?
 
Sijafanya editing andiko langu natumia simu hivyo kwa yoyote atakayepata tabu aniwie radhi
 
Sasa mkuu wangu kwenye hali kama hii unapigaje kura?!
7654311.png
 
Back
Top Bottom