Ongeza chachu ya mapenzi kwa kufanya yafuatayo

Ongeza chachu ya mapenzi kwa kufanya yafuatayo

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
9,296
Reaction score
7,713
Kawaida ukiwa kwenye uhusiano wa muda mrefu zile chachu za mapenzi hupungua kulingana na muda unavyokwenda.Kuna njia/mbinu tofauti ambazo zinaweza kutumika kurejesha mihemeko ya mahabati
Kukumbatia kwa sekunde 20:
Kukumbatia/ana ni kitendo kinarejesha ukaribu wenza walio na mapenzi yanayofifia.Ukikumbatiana kwa sekunde 20 mwili unaongeza production ya oxytocin ambayo inaongeza ukaribu wenu.
hug.jpg
Usafi na mpangilio chumbani:
Chumbani ni sehemu ambayo wenza wanakuwepo muda mwingi wakihitajiana.Usiweke picha za familia kama mkweo au ndugu zako eneo hili,ni vyema pia ukiepuka kuweka luninga chumbani.Vitu hivyo vinapunguza mihemeko ya mapenzi mfano kama luninga inaweza kutumika kama sababu ya kuepuka ukaribu.
bedroom.png
Tuna ujumbe wa mahaba:
Mtumie ujumbe wa mahaba mwenza wako,kama iwe kwa njia ya barua pepe,au ujumbe mfupi,ujumbe ambao utaamsha mhemeko wa mapenzi na kuonesha hitaji lako kwake.
love note.jpg
Mwambie unachokihitaji:
Ni vyema kama mwenza wako akijua vitu vipi unapenda na usivyopenda na iwapo kama ametenda kitu usichokiridhia mjulishe na mwambie kile unachokihitaji kutoka kwake.
kulishana.jpg
Fanya yale yasiotarajiwa:
Maisha ya mahusiano yamejiegemeza kwenye uaminifu,matarajio fulani kutoka kwa mwenza wako.Ni vitu vizuri vikihusishwa na economy ya familia na utunzaji lakini si kwenye mahusiano.Fanya kile ambacho hutarajiwi kukifanya kama "SURPRISE" mfano watoto wakishalala au asubuhi ukiamka.
bob.jpg
the unexpected.jpg

Weka muda kwaajili yenu tu:
Panga muda utoke wewe na mwenza wako ili muwe faragha pamoja bila bugudhi kutoka kwa watoto au watu wengine.Huu utakuwa ni muda muafaka wa kukumbushia ya zamani.
index.jpg
Mfanye tendo la ndoa bila "tendo lenyewe":
Tendo la ndoa halihusishi mwili tu bali akili pia.Kuwa creative na kumbambiana/kunyegezana na kufanya vitu ambavyo vinawaunga pamoja bila kuhushisha kuingiliana kunaongeza chachu za mapenzi.
playing.jpg
Ugomvi usifike chumbani:
Yale yote yanayofanyika nje ya chumbani yanaathiri yatakayotendeka chumbani.Kama mna ugomvi,malizeni huo ugomvi kabla hamjaenda kulala.Mkumbatie mwenza wako,mtanie au mpe busu la nguvu kama mna mabishano yanayopelekea ugomvi.
kiss.jpg
Chunguza ayapendayo mwenza wako:
Fanya yale ambayo mwenza wako anayapenda kama kumpa compliment ili kuongeza kujiamini kwake,msifie mumeo au mkeo kama ni mdada/mkaka mwenye mvuto wa mahaba.
seduceeee.jpg
Fanya mazoezi au vile vitu unavyopendelea:
Jinsi unavyojitunza na kujijali mwili wako,ndivyo unavyokuwa katika hali ya kujihisi una mvuto wa mahaba.Fanya vile vitu unavyovipenda ili kujihisi una mvuto na kukuongezea kujiamini
View attachment 154717
excercise.jpg
Tembelea tena zile sehemu za fungate:
Kumbushia zile siku za furaha ambapo shamrashamra za mapenzi zilikuwa zimenoga,fanya hayo katika uhusiano wako wa sasa.
date.jpg
 
Kuna haja ya kuweka kwenye katiba suala wenza.kusindikizana kwenye safari za kikazi.
Kama mmoja wenu ni mtu anayekuwa nyumbani au yupo off kusindikizana kunaweza kuwapa nafasi/muda wa faragha wa pamoja au la,kwasababu hio ni "safari ya kikazi" kwahio kuna uwezekano mwenzi wako awe na pirika za kazi angali wewe unataka attention yake na usiipate!
Kama ukimsapraiz mwenzio anapokuwa kwenye safari ni kitu kizuri pia kitakachoongeza chachu ya mapenzi!
 
Kuna haja ya kuweka kwenye katiba suala wenza.kusindikizana kwenye safari za kikazi.

We bana weee unataka wale waliojazana dom wakose hela ya kula.
Ila nakumbuka kipindi fulani walikuwa wanasema waende na familia zao mjengoni sijui iliishiaga wapi.
Lets say dodoma now yaani huko kuanzia dodoma hotel mpaka "utajiju guest houss zimejaa"unajua inakuwaje......
 
hizo picha zingekuwa za waswahili wenye maisha ya kawaida yenye changamoto nyingi ingeeleweka zaidi
 
Back
Top Bottom