Ondoka Dar, unapoteza muda!

Ondoka Dar, unapoteza muda!

Dar raia wanaishi maisha magumu,wanaoenjoy ni wachache mno,sasa mtu anaogopa muda uliopotea Dar,na ile mentality ya kiboya kua ukiwa Dar umefanikiwa,Raia wanaogopa kurudi mkoani kuanza upya wataonekana wamechoka.
Ila ndio hivo wafanyaje sasa
Takwimu zinaonesha hapa Tanzania, Dar ndio kuna watu wengi wenye maisha mazuri kuliko mkoa wowote. Masikini wapo kila mahali jitahidi usiwe huyo masikini.
 
Maisha yakikushinda unafikiri watu wote. Kuna jamaa maarufu sana katoka kijijini kwao 2016 sasa hivi yuko vizuri sana. Unafikiri huyu atakuelewa umwambie akimbilie kijijini? Serikali yenyewe imehamia Dodoma ila kila weekend treni zinajaa wanarudi Dar.
Ilikua zamani hio bana,saiv watu wametulia ,Dodoma na mikoani wanapata kila kitu

Serikali iwekeze zaidi mikoani,kupunguza raia kurundikana zaidi Dar
 
Nilidhani ungetushauri twende New York , London, Paris na majiji makubwa we unatuambia turudi maporini tena

Hilo haliwezekani tutapambana hapa hapa mjini and beyond borders
 
Takwimu zinaonesha hapa Tanzania, Dar ndio kuna watu wengi wenye maisha mazuri kuliko mkoa wowote. Masikini wapo kila mahali jitahidi usiwe huyo masikini.

Takwimu zinaonesha hapa Tanzania, Dar ndio kuna watu wengi wenye maisha mazuri kuliko mkoa wowote. Masikini wapo kila mahali jitahidi usiwe huyo masikini.
Hizo takwimu unajua zinapatikanaje?pato la mkoa,linaweza changiwa ukubwa na matajiri wawili tu,likagawanywa kwa Raia wote,ukaonekana na wewe kua upo vizuri kimapato ila huna kitu

Wewe Usijijumuishe kwenye mapato ya akina Mo dewji,ukajiona na wewe unaishi maisha bora 😀
 
Hizo takwimu unajua zinapatokanaje?pato la mkoa,linaweza changiwa ukubwa na matajiri wawili tu,likagawanywa kwa Raia wote,ukaonekana na wewe kua upo vizuri kimapato ila huna kitu

Wewe Usijijumuishe kwenye mapato ya akina Mo dewji,ukajiona na wewe unaishi maisha bora 😀
Sawa.
 
32F7D7BE-F3B8-4C7E-A146-678D732DC7CF.jpeg
 
Mimi baada ya kumaliza chuo tu nilihama dar es salaam kwasababu nilisoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka chuo.

Lengo lilikuwa kubadilisha mazingira nikiamini dar hakuna fursa kama mikoani.

Nilianza na zanzibar maisha ghalii sana ubaguzi wa wazi na kipato asilimia kubwa wanategemea utalii
Zanzibar kujenga inawezekana ila utachukua muda sana

Nikatoka zanzibar nikaenda nyumbani tabora, kule picha linaanza matajiri ni wale wale wa miaka yote na masikini ni wale wale vijana ambao nilisoma na kukua nao niliwakuta vile vile fursa hakuna usafiri changamoto hela ngumu

Watu wanaishi kwa mazoea
Kupeana mimba
Ulevi shughuli kubwa bodaboda.

Nikatoka hapo nikaenda iringa kule ndio yale yale watu mabahiri fursa chache watu wachache maisha mepesi pesa ngumu

Nikatoka iringa nikaenda tunduma kule angalau pesa ipo mzunguko mkubwa kla wizi ushirikina magendo ndio biashara kuu.

Nikatoka nikaenda kagera napo nilikaa mwezi nikakimbia ule mji ni takataka kabisa

Nikatoka nikaenda arusha angalau arusha ila sikupapenda uhuni mwingi fursa sana utalii sipakatai sana arusha

Baada ya hapo nimerudi tena zanzibar mpango ni kufanya kazi miezi miwili tu

Baaada ya hapo narudi dar na siwezi kukaa mkoa nje na dar daima siwezi

Fursa zipo dar
Madili yapo dar
Biashara zipo dar
Connection zipo dar
Wanawake wapo dar


Kwa kijana kama huna dili unaaanza from zero kama mimi dar ndio penyewe

Kitaaaluma
Kiuchumi
Kibiashara
Kimichezo

Kila kitu ni dar
Oya nakuja daaaaaaar
Najuta kuondoka dar


Oyaaaaa nakujaaaaaaa dar
 
Sasa walioko dar wakisikia neno mkoani wanajua ni kijijini

Mnasahau mikoani kuna miji, wilaya, halamshauri, mainispaa

Zote ni sehemu zinakua kwa kasi
mfano mji upi unaokuwa kwa kasi ambao unamfaa kijana anaejitafuta? Miji yote imechangamka kama dar tu.
 
Kijijini ili upate 5000 lazima ukapalilie shamba ekari moja au kung'oa visiki . Mjini unapata kama hiyo na zaidi kwa siku kwa kuuza matikiti jioni au kuchoma mahindi ,kuchoma kuku kupanga ni kuchagua
 
Back
Top Bottom