Habari wana jf,
Kwa kifupi kila nikipata safari ya kikazi, familia au mapumziko na kufika au kupita Dar es Salaam
Huwa na ondoka nikiwa na huzuni sana moyoni mwangu
Kwasababu hizi chache
1. Ndio sehemu ambayo hunikumbusha kwamba ninaweza kuwa bora sana katika shughuli zangu za kiutafutaji au kuonekana ni mtu niliyefanikiwa huko nilipo lakini kila nikiwepo hapa hujiona si lolote wala chochote
2. Ni sehemu ambapo hunipa huzuni kwasababu hunionyesha uhalisia hata nipambane kiasi gani hata niwe na Bil 100 bado kuna Meza au nafasi sitazipata
3. Ni sehemu pekee hunionyesha kwamba naweza kupambana nikatengeneza misingi bora lakini kuna familia kamwe sitaweza kuzifikia hata kizazi kipite
4. Ndio sehemu naona vijana wengi wakiteketea kwa wingi kwasababu yakutaka kuishi au kuendana na life style ambayo iko juu ya uwezo wao
Pia ndio sehemu pekee vijana wengi wa mikoani wakimaliza vyuo hutamani kubakia kupambania kombe mwisho wa siku huishi maisha magumu sana kupita maelezo kumbe wakati mwingine fursa ziko nje ya dar au tanzania.
Kwahyo ni jiji ambalo hunipa huzuni na masikitiko moyoni
Wewe mwana jf mwenzangu unalionaje hili