Ondoka Dar, unapoteza muda!

Ondoka Dar, unapoteza muda!

ONDOKA DAR, UNAPOTEZA MUDA!

Vijana wengi tunakimbilia Dar es Salaam tukiamini kwamba ndipo maisha yanapojengwa. Tunatumia miaka mingi kutafuta riziki kwenye jiji ambalo gharama za maisha ni kubwa, huku tukisahau fursa zilizopo mikoani.

Wenzako waliobaki mikoani wanakamata heka za viwanja, wanajenga nyumba, wanawekeza kwenye mashamba na kuanzisha miradi ya muda mrefu.

Wewe umeng'ang'ana Dar, kila siku unapambana kuuza karanga, kulipa kodi, nauli na gharama nyingine za maisha. Miaka inapita, lakini huna hata kipande cha ardhi cha kuwarithisha watoto wako.

Dar es Salaam ni mji mzuri wa kutafuta biashara, kutumia vipaji na kutengeneza connection, lakini si lazima uwe sehemu bora ya kujenga utajiri wa muda mrefu kwa kila mtu.

Jiulize maswali haya:

  • Unafanya kazi kwa bidii, lakini unawekeza wapi?
  • Miaka 10 ijayo utakuwa na nini cha kuonyesha?
  • Watoto wako watarithi nini kutoka kwenye juhudi zako?
  • Kwa nini usitumie kipato unachopata mjini kuwekeza mkoani?

Ndiyo maana unaona watu wengi wakistaafu wanarudi mikoani. Wengine wakipata changamoto za kifedha wanarudi nyumbani kwa sababu huko wanaweza kuwa na ardhi, familia na gharama nafuu za maisha.

Ukweli ni kwamba, si lazima uishi mjini ili uwe tajiri. Wakati mwingine, utajiri wako unaweza kujengwa sehemu ambayo wengine wanaikimbia.

Vijana, tusikimbilie maisha ya mjini bila mpango wa maisha ya baadaye. Tafuta kipato mjini kama kuna fursa, lakini usisahau kuwekeza nyumbani.

Mimi ni kijana wa mkoani, na naamini fursa za kujenga maisha hazipo Dar es Salaam pekee.

Mkoani pia kuna maisha, ardhi na fursa kubwa za uwekezaji!

NB: MKOANI SIO KIJIJINI mkoani kuna maeneo yanayokua kwa kasi sana ambayo yapo mjini
Huku nasikia kuna mzunguko wa Matrillioni mengi. Ngoja tuyavune kwanza hayo Matrillioni Mkuu!😀
 
Waliokuwa wanapambana vijijini au wilayani wakipata za kutosha ndio wanakuja Dar kufanya kitu kikubwa zaidi au hata biashara kubwa kulingana na alichokuja nacho.

Kama kijana amekuja mjini bila kitu ni sawa pia maana kama ana malengo mazuri ipo siku atafikia malengo yake
Usiwakatishe watu tamaa kwani kila mmoja na bahati yake
 
Dar ndio jiji lenye maghorofa mengi. Nenda Goba, Mbweni, Kigamboni etc uone watu walivyojipata, kisha linganisha na mikoani, kisha urudi tena hapa.
Maisha yakikushinda unafikiri watu wote. Kuna jamaa maarufu sana katoka kijijini kwao 2016 sasa hivi yuko vizuri sana. Unafikiri huyu atakuelewa umwambie akimbilie kijijini? Serikali yenyewe imehamia Dodoma ila kila weekend treni zinajaa wanarudi Dar.
 
Unachosema ni kweli ila tatizo ni kuanza upya. Si kila mtu anaweza, imagine upo 30+ plus majukumu, utakuwa na uwezo wa kuanza upya

Isitoshe mkuu, Tanzania hii wengi tunaishi maisha ya low mantainance tu na wengine hand to mouth. Sasa mtu anajiuliza, kiwanja hana, nyumba hana ila at least pesa za kutimiza majukumu anazo.

Kutengeneza channel ya hela inahitaji risk na si kila mtu anaweza
 
Watu wanakimbia Bush party wanakimbilia mijini we unashauri mtu arudi huko una jitambua mkuu, kupata ef 50 mfukoni Usha kua motivation speaker sio, tuoneshe unacho miliki kwanza ili tukuamini, yani utoke sehemu amabayo inachangia kariba asilimia 90 ya pato la taifa unaenda mikoani?

Diamond anapiga show kwa billion moja na nusu ulaya huko, anakuja kuzilia hela dar kwake, Ana agiza Michele, unga mafuta, nk hapo dar, simba yang wanacheza mikoaani hela wanakuja kuzilia dar, matajiri wakubwa mikoani huja kuzitumia pesa dar, we unashauri mtu atoke dar aje mikoani yes inawezekana lakin kila mtu na mipango yake.

Top 20 ya matajiri waakubwa Tanzania wote wapo dar na sio huko mikoani his ina maana ukikaza unatoboa

Nikwrli kuna vijna wamepoteza muda dar hamna inshore, mikoani pana wafaa mkuu.

Naomba nikupongeze kwa kujitolea kuwasanua vijna pia
 
Dar raia wanaishi maisha magumu,wanaoenjoy ni wachache mno,sasa mtu anaogopa muda uliopotea Dar,na ile mentality ya kiboya kua ukiwa Dar umefanikiwa,Raia wanaogopa kurudi mkoani kuanza upya wataonekana wamechoka.

Ila ndio hivo wafanyaje sasa,wameshatambishia watu kua wana maisha bora mjini?
 
Back
Top Bottom