youngkato
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 3,864
- 3,979
ONDOKA DAR, UNAPOTEZA MUDA!
Vijana wengi tunakimbilia Dar es Salaam tukiamini kwamba ndipo maisha yanapojengwa. Tunatumia miaka mingi kutafuta riziki kwenye jiji ambalo gharama za maisha ni kubwa, huku tukisahau fursa zilizopo mikoani.
Wenzako waliobaki mikoani wanakamata heka za viwanja, wanajenga nyumba, wanawekeza kwenye mashamba na kuanzisha miradi ya muda mrefu.
Wewe umeng'ang'ana Dar, kila siku unapambana kuuza karanga, kulipa kodi, nauli na gharama nyingine za maisha. Miaka inapita, lakini huna hata kipande cha ardhi cha kuwarithisha watoto wako.
Dar es Salaam ni mji mzuri wa kutafuta biashara, kutumia vipaji na kutengeneza connection, lakini si lazima uwe sehemu bora ya kujenga utajiri wa muda mrefu kwa kila mtu.
Jiulize maswali haya:
Ndiyo maana unaona watu wengi wakistaafu wanarudi mikoani. Wengine wakipata changamoto za kifedha wanarudi nyumbani kwa sababu huko wanaweza kuwa na ardhi, familia na gharama nafuu za maisha.
Ukweli ni kwamba, si lazima uishi mjini ili uwe tajiri. Wakati mwingine, utajiri wako unaweza kujengwa sehemu ambayo wengine wanaikimbia.
Vijana, tusikimbilie maisha ya mjini bila mpango wa maisha ya baadaye. Tafuta kipato mjini kama kuna fursa, lakini usisahau kuwekeza nyumbani.
Mimi ni kijana wa mkoani, na naamini fursa za kujenga maisha hazipo Dar es Salaam pekee.
Mkoani pia kuna maisha, ardhi na fursa kubwa za uwekezaji!
NB: MKOANI SIO KIJIJINI mkoani kuna maeneo yanayokua kwa kasi sana ambayo yapo mjini

- Unafanya kazi kwa bidii, lakini unawekeza wapi?
- Miaka 10 ijayo utakuwa na nini cha kuonyesha?
- Watoto wako watarithi nini kutoka kwenye juhudi zako?
- Kwa nini usitumie kipato unachopata mjini kuwekeza mkoani?